Mbunge Musa Azzan Zungu akamatwa kwa tuhuma za Rushwa; TAKUKURU yashindwa kukamata ushahidi

hakuna mbunge wa ccm aliyewahi kukamatwa hata kwa wizi akachukuliwa hatua yoyote, sembuse rushwa?
 
31/10/2012


habari kutoka tbc1 zinahabarisha kuwa mbunge wa jimbo la ilala, dar es salaam, ambaye pia ni mwenyekiti wa bunge la jamhuri ya muungano tanzania, mussa hassan zungu na watu wengine watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika uchaguzi wa jumuiya ya wazazi wa ccm unaofanyika huko dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na kamanda wa takukuru mkoa wa dodoma.




source:
http://www.wavuti.com/4/post/2012/10/mbunge-wa-ilala-azzan-zungu-akamatwa-k
wa-tuhuma-za-rushwa.html#ixzz2auawuvtu
cc: Riziwan, zomba, chama. Tume ya katiba, m.k.were jk, baharia, nepi ya kukojolea watoto, tamuchungu na ni dedication pia kwa magamba na vibaraka vyao vyote ingawa najua mkuu wa magamba atazima hii kitu kama alivyoizima kwa zainabu vullu na yule mbunge wa magamba aliyeshitakiwa bahi kwa rushwa!
 
TAKUKURU wanahalalisha mishahara na posho zao za mwezi Novemba, TANZANIA BANA, A COUNTRY OF JOKE
 
kama kwenye issue ya mbunge wa viti maalum ZAINABU VULLU alikamatwa LIVE anagawa pesa lakini mpaka hii leo ajafikishwa mahakamani jiulize why kwahiyo kama imeshindikana kwa ZAINABU VULLU itawezekana kwa ZUNGU.
Mungu tusaidie nchi hii yaani RULE OF LAW NI ZERO.

Oh yes... Unasema Ukweli na AMESHINDA UWT-CCM-NEC Mwishowe... Ina hatarisha kweli kila mtu ni MWIZI hadi DEREVA wa Wabunge... Nani atashikwa???
 
Oh yes... Unasema Ukweli na AMESHINDA UWT-CCM-NEC Mwishowe... Ina hatarisha kweli kila mtu ni MWIZI hadi DEREVA wa Wabunge... Nani atashikwa???
Niliwahi kusoma hapa pia mayor mmoja Slaa alikamatwa akitoa rushwa hivi iliishia wapi wakuu?
 
Wamemchoka huyo zungu then hayumo kwenye mtandao wa magamba wameamua kumtoa kafara!
 
Sikushangazwa na habari hii kwani ni kawaida ya wana ccmweli.

Ccmweli yajenga nchi!
 
Kama hujui ndio ujue sasa.Watu maarufu nchini kama Wabunge hutumiwa na watawala kukamatwa kwa rushwa. Unashangaa?! Usishangae. Ni hivi,Serikali huwatumia wabunge fulanifulani kama mfano wa kuwashughulikia wala na watoa rushwa ili wananchi waamini kuwa Serikali yao ni makini na kali juu ya vitendo vya rushwa. Sisi tuliopo CCM katika ngazi za juu za chama tena miaka na miaka tunajua vyema.

Ndani ya CCM,hakuna mgombea wa nafasi yoyote asiyetoa rushwa. Wote tunatoa na kupokea rushwa. Kila mwanachama analijua hilo.Lakini,tunazidiana. Huwezi kufananisha fungu la Mama Sitta na lile la Lowassa. Huwezi kufananisha fungu la Nape Nnauye na lile la Ridhiwani Kikwete. Ni tofauti.

Kimsingi,kukamatwa kwa Azzan Zungu kunaweza kuishia kama kwa Mama Sitta.Au,kesi itasukwasukwa kama ya Badwel.Hakutakuwa na jipya.Zungu amekamatwa kweli leo hii mbele ya macho yangu Dodoma katika uchaguzi wetu wa Wazazi. Hata mimi nililetewa bahasha.Guess what? Nilipokea na kuila.

Jamani watanzania,tunawaomba tena na tena,tutoeni madarakani haraka iwezekanavyo ili nasi tupumzike kutoa na kupokea rushwa.Hivi,hamjisikii vibaya kuona sisi peke yetu tunamiliki uchumi wa nchi hii na kuutafuna tutakavyo? Mnapenda sisi wezi na wenye roho za kinyama tuendelee kuwaongoza kwa maslahi yetu wenyewe. Tupo tutakaoyaunga mkono mabadiliko ili tupate nafasi ya kutubu. Watanzania amueni sasa!
 
Sasa CCM rushwa kama mawingu na mvua. Musa Azzan Zungu, Mwenyekiti wa Bunge la JMT ndani ya Hati hati ya kujihusisha na vitendo vya rushwa. Namhurumia JK sijui atafuta chaguzi ngapi za taasisi za CCM?
Zungu yupo kambi ya nani kuelekea 2015??
 
Hapo Ngoma imeiva, Jk alishatangaza sasa Uongozi ndani CCM ni kwa Rushwa tu, Tuendeleeeeeee kuwa shangilia hiyo ndio silaha pekee kwa Upinzani kuwaondolea CCM madarakani
 
31/10/2012


Habari kutoka TBC1 zinahabarisha kuwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mussa Hassan Zungu na watu wengine watatu wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na rushwa katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM unaofanyika huko Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma.




Source:
http://www.wavuti.com/4/post/2012/10/mbunge-wa-ilala-azzan-zungu-akamatwa-k
wa-tuhuma-za-rushwa.html#ixzz2AuAWuVTU

mm nimeona TBC tv yule Mama wa TAKUKURU kasema hawajamkuta na cash ila mitego yao na simu inaeleza alikuwa anaenda kutoa rushwa usiku wa manane alipokamatwa hakukutwa nayo ila wanadhani hela zilikuwa kwenye Gari iliyokimbia ya RAV 4
Hii Rushwa imeanzia mbali na hasa tukikumbuka Jimbo la Arumeru Mashariki walikamatwa LIVE sasa km mlolongo wote ni mpaka kwa wazazi Basi CCM imekwisha maana hawataki kufuata hata ule Usemi wa Mh Nyimbo

“Mfano wewe ukipokea rushwa na kuamua kufanya tofauti na aliyekuhonga kwa kuwa baadaye atakuwa hajapata kile alichotaka kukinunua toka kwako, unafikiri kesho atarudia”.
"Thomas Nyimbo aliyekuwa Mbunge wa CCM na Mlezi wa CDM Iringa Mbeya na Njombe"
 
Kama ulikuwa hujui,TAKUKURU ni TAasisi ya KUzuia KUpambana na RUshwa.
Kazi yake kuu ni kuzuia mapambano dhidi ya rushwa na ndiyo maana iliisafisha richmond na ikamsafisha Chenge.
Hiyo ni janja ya kuwapumbaza wananchi tu ili wenyenchi waendelee kuila na kuifilisi.
kwa kifupi, TAasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa ingeitwa TAYAKUNAKURU.
 
kama kwenye issue ya mbunge wa viti maalum ZAINABU VULLU alikamatwa LIVE anagawa pesa lakini mpaka hii leo ajafikishwa mahakamani jiulize why kwahiyo kama imeshindikana kwa ZAINABU VULLU itawezekana kwa ZUNGU.
Mungu tusaidie nchi hii yaani RULE OF LAW NI ZERO.

Umesahau na yule wa BAHI hadi leo kimya na yupo Bungeni anaendelea kutesa tu, na ili kuthoofisha mwenendo wa kesi wamemuhamishia Tabora yule Mkurugenzi.
 
Back
Top Bottom