Mbunge Mtwara Mjini CCM Hasnein Murji aionya CUF kuacha siasa inayohatarisha Amani na Usalama

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, 06 June 2011 07:55 newsroom



Na Rashid Mussa, Mtwara

MBUNGE wa Mtwara Mjini, Hasnein Murji amekionya chama cha CUF kwa kuendesha siasa chafu dhidi yake na CCM, hali inayohatarisha amani na usalama wa wananchi.Akizungumza juzi katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika mji mkongwe wa Mikindani, mbunge huyo aliwaambia wananchi kuwa tangu CUF imekuwa ikieneza kashfa, matusi na oungo dhidi yake. Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka jana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza kuwa yeye ndiye mbunge halali wa jimbo hilo, na kwamba chama hicho kisieneze uongoz usio na tija kwa wananchi. Alisema kinachofanywa na chgama hicho ni chuki na uhasama binafsi dhidi yake, hivyo alitangaza kupambana nacho hadi ili kudai haki yake katika vyombo vya sheria na si njia za kihuni. Murji alisema CUF wamekuwa wakiendeleza uchochezi kwa wananchi jimboni humo, serikali na CCM kupitia mikutano ya hadhara kwa kumzushia kashfa, kumtukana na mambo ya ushirikina.
Aidha, alisema chama hicho kimekuwa kikizungumzia kesi iliyopo mahakamani kwa kuitolewa hukumu kuwa kimeshinda, na kwamba Mtwara Mjini hakuna mbunge, jambo ambalo ni kuingilia uhuru wa mahakama. Alidai kwa sababu kinazojua, chama hicho pia kimekuwa kikivumisha
kwamba yeye ni mgonjwa wa kansa, kiwete aliyekatwa miguu, jambo ambalo limemsababishia usumbufu mkubwa kutoka kwa wananchi.


Akihutubia umati mkubwa, wananchi walishangaa kumwona akiwa amesimama jukwaani akiwa mzima na mwenye afya njema tofauti na uvumi huo.Murji alikitaka chama hicho kutambua kwamba muda wa kampeni za uchaguzi umepita, na kuonya kuwa hatavumilia kuna CUF ikiendesha propaganda chafu dhidi yake. “Wakati wa kampeni niliwavumilia mno, walinitisha kwa masuala ya uchawi, wakaja nyumbani kwangu wakiwa na mapanga na visu, huku wakinitukana kupitia majukwaa kwa kashfa nyingi,” alisema mbunge huyo.

Alisema CUF imekuwa ikiendesha siasa za kuganga njaa, kwa kuwachangisha wananchi katika mikutano ya hadhara kwa ajili ya mbunge ambaye hayupo, na kwamba hutumia uzushi huo ili kuvuta watu. “Walifanya hivyo kwa kuwachangisha wananchi juzi katika mkutano wao uliyofanyika Chikongola... huu ni utapeli mkubwa unaomsaidia mtu huyo kupata pesa ya kula,” alisema Murji huku akishangaliwa na watu. Katika mkutano huo ambao pia Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Dadi Mbullu alihutubia, alisema katika kipindi cha miaka michache ijayo Mtwara itakuwa kitovu kikubwa cha maendeleo hapa nchini. Alisema kasi ya maendeleo katika mikoa ya Mtwara na Lindi si ya kubezwa, kwani ni ishara kuwa inapanda kwa kiasi kikubwa akitolea mfano wa miundombinu ya barabara ya Dar es Salaam hadi Mtwara na Mtwara - Mbamba Bay hadi Lilongwe, Malawi. Miundombinu mingine ni pamoja na kuunganishwa kwa barabara kati ya Tanzania na Msumbiji kupitia daraja la Umoja, kupatikana kwa umeme wa uhakika wa gesi hiyo kuwa vichocheo vya uhakika vya maendeleo ya mikoa hiyo.
 
Duh hii imekaa vyema...ujue siku zote nikoiona kimya kwamba watu washaridhika, kumbe kunafutuka namna hii...hadi kukatwa miguu,duh viva CUF, mtafuneni hadi kieleweke!!
 
hivi kumbe ndugu zetu walimpa yule gabachori ubunge?aisee tuna safari ndefu sana ya kutembea
 
kazi ipo tz,duu hadi ushirikina ktk chama pinzani dhidi ya ccmagamba,je usibitisho upo???
 
Back
Top Bottom