Mbunge Mteule wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan (CHADEMA) atoa tamko kuhusu ushindi wake

Anataka kususa ubunge? Kwa hiyo ktk shule darasa lako zima limefeli mtihani, mmoja tu kafaulu, na yule aliyefaulu anakataa matokeo na kususa kuungana na wenzake walio feli? Duh, basi afanye hivyo
Mfano wa kitoto usioendana na hali halisi. Kama wenzake walifelishwa kwa makusudi kwanini yeye afurahie kufaulu peke yake?
 
Huyu dada ni bora aachie tu huo ubunge dunia ione wazi kuwa hii nchi inaendeshwa kidikteta.

Kuna mambo natabiri yatatokea baada ya huu uchaguzi na nina uhakika wa 100%.

1. Sasa waliokuwa wabunge na madiwani wa CHADEMA hawana kazi, Magufuli atataka kutumia hali yao duni ya kifedha ili awarubuni kwa kazi halafu wahamie CCM. Hatofanya hivyo kwa kuwapenda bali ni propaganda ya kuficha madhambi yake na kuionyesha dunia kwamba watu wanamuunga mkono.

2. Tundu Lissu kama kawaida yake hawezi kuhongeka kwa kazi au fedha. Hata ukiacha mambo ya maslahi Tundu Lissu siyo rahisi kukubali kuwa chini ya mtu aliyemzidi sana kwa akili na maarifa.

3. Tegemea watanzania wengi na mataifa ya nje ukiacha nchi za kiafrika kutomuunga mkono Magufuli. Mataifa ya Ulaya na Marekani watakwenda mbali zaidi na kuiwekea vikwazo "serikali" ya Magufuli.

Kwa kifupi Magufuli ni sawa na mtu anayekuchomea shamba lako moto halafu anakwambia mimi ni mtu mwema, njoo unilimie shamba langu nikupe chakula!
 
So, Aidah na wenzie wa viti maalumu wasikubali kwenda Bungeni then wahamie Twitter na JF kufanya uharakati? Wrong move. Na tutajuta.
Narudia kukwambia tena, wacha uoga, usifikirie kwa kutumia tumbo, wacha kichwa kifanye kazi, km hiyo twitter isingekuwa na nguvu wasingehangaishwa na Kigogo mpaka leo.

Bora twitter kuliko lile bunge la spika anaekuzimia "mic" ukitaka kuwapinga.
 
Leo wana CCM wamekuwa sympathizers wa Chadema, eti wanataka wapinzani waingie bungeni, ajabu sana.
πŸ˜ƒπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Hatari kweli. Tulizeni akili and think objectively.

Harafu huwezi kumbrand mtu kuwa mwana CCM kwa sababu tu mtazamo wake upo tofauti na wa kwako. Maturity is agreeing to disagree.
 
Huwezi kuwaachia ngedere shamba. Utavuna mabua!

CHADEMA on the verge of repeating the same mistake. Hii strategy ya kususa mwisho wake huwa ni mbaya - almost always!

Yaliyo kwisha kutokea kwa kusababishwa na CCM ni zaidi ya huyu mwana Mama kuachana na Ubunge wa kupewa na CCM.
 
Huyu kwake chama ni bora kuliko wananchi waliomwamini kuwawakilisha. Halafu huyu alikuwa mmoja wa vitu maalum kwa Mwenyekiti so ni uamuzi uliotegemewa.

Kwani akijiuzulu Sheria si inahitaji Jimbo kupata Mbunge mwingine wa kuwa wakilisha Wananchi !?.Ubaya upo wapi hapo !?.
 
πŸ˜ƒπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚. Hatari kweli. Tulizeni akili and think objectively.

Harafu huwezi kumbrand mtu kuwa mwana CCM kwa sababu tu mtazamo wake upo tofauti na wa kwako. Maturity is agreeing to disagree.
Kwahiyo maturity ni kumlazimisha aingie bungeni awaache wapigakura wake na viongozi waliompigania wakizikana na kuuguza majeruhi.
 
Huyu kwake chama ni bora kuliko wananchi waliomwamini kuwawakilisha. Halafu huyu alikuwa mmoja wa vitu maalum kwa Mwenyekiti so ni uamuzi uliotegemewa.
Hana adabu huyu mama, anawakosea heshima walio mpa hiyo nafasi. Bora aachie ngazi kieleweke.
 
53 Reactions
Reply
Back
Top Bottom