Mbunge mtarajiwa kupitia CHADEMA aliyenaswa na mguu wa mtu aliza makanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge mtarajiwa kupitia CHADEMA aliyenaswa na mguu wa mtu aliza makanisa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pengo, Jul 25, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wetu, Mbeya

  Baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali mkoani hapa, wako katika kilio kufuatia kitendo cha mgombea Ubunge wa CHADEMA aliyerudisha fomu, George Mtasha (50) kudakwa na jeshi la Polisi wilayani Chunya akiwa na mguu wa kushoto wa binadamu, Risasi Jumamosi linashuka kikamilifu.

  Wakiongea na Mwandishi Wetu, baadhi ya waumini hao walisema kuwa, wanaamini kitendo hicho ni ishara ya mwanzo wa vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikiukumba mkoa wa Mbeya miaka ya karibuni.


  Josephat Mwaibabile ambaye ni Mzee wa Kanisa la Kiroho la Jerusalem Temple, alisema kuwa mkoa wa Mbeya una skendo ya watu kuchunwa ngozi, waumini wakalia kwa Mungu kwa maombi na kufunga mpaka mambo yakakaa sawa, “Sasa hili la mtu kukutwa na mguu wa binadamu mwenzake, nalo limetuliza, Mungu apishie mbali jamani,” alisema mzee huyo.


  George Mwangata, muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (chini ya Askofu Mkuu, Alex Malasusa) Soko Matola, jijini humu, alisema kitendo cha mtuhumiwa kukutwa na kiungo hicho ni pigo kwa makanisa, kwani Mbeya ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makanisa mengi nchini Tanzania.


  Mama Nitike, muumini wa Roman Catholic (chini ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo), Mwanjelwa, Manispaa ya Mbeya, alisema alishtuka kusikia habari hizo na hajaamini kama kweli kiungo hicho kilikuwa ni cha binadamu.


  “Kwa kweli sijaamini, he! Kweli binadamu unatembea na kiungo cha binadamu mwenzako, mh!” Alishangaa sana mama Nitike.

  Aidha, Risasi Jumamosi lilipata bahati ya kuongea na Paulina Mwakifwamba, muumini wa Kanisa la Anglican (chini ya Askofu Costantine Mokiwa pichani), Rungwe ambapo alisema kuna haja ya umoja wa makanisa mkoani humo kukaa haraka na kufanya maombi ya kufunga siku tatu ili kumwomba Mungu aondoe roho inayotaka kuinuka, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.


  Naye muumini wa kanisa la Full Gospel&Bible Fellowship (FGBF) ambalo lipo chini ya Askofu Mkuu, Zacharia Kakobe, aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank, tawi la Mbeya alisema maombi ya kufunga yanatakiwa kwa ajili ya mwelekeo mzima wa uchaguzi mkoani humo, mbali na suala la mgombea huyo kukutwa na mguu wa binadamu.


  George Mtasha ni mgombea Ubunge jimbo jipya la Makongorosi, wilayani Chunya na mwenzake, Paul Mnyambwa, walikutwa na kiungo hicho saa 12.50 alfajiri ya Jumatano, Julai 21, 2010 na kushikiliwa na jeshi la polisi.


  Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema, uchunguzi mkali unaendelea.
   
 2. mawazotu

  mawazotu Senior Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 27, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uchaguzi umeanza

  *Mgombea akutwa na mguu wa mtu Mbeya
  *Ni wa Chadema aliuficha uani, akamatwa

  Na Maregesi Paul

  MGOMBEA ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Jimbo Jipya la Makongorosi lililoko Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, George Mtasha (50), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya baada ya kukutwa na mguu wa mtu.

  Katika tukio hilo, Mtasha ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, amekamatwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Paul Mnyambwa (43).

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Adcocate Nyombi, aliiambia MTANZANIA kwa njia ya simu jana kuwa, Mtasha na Mnyambwa walikamatwa jana saa 12.50 alfajiri baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema, kwamba watu hao wanamiliki mguu wa mtu.
  “Ni kweli kuna watu wawili wakazi Bwawani, Makongorosi Chunya ambao wote ni wafanyabiashara wa madini ya dhahabu, tunawashikilia hapa. Kabla ya kuwatia mbaroni, awali tulipata taarifa kutoka kwa raia wema ambao walitwambia kwamba, watu hao wanamiliki mguu wa mtu kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

  “Tulipopata taarifa hizo, vijana wetu kutoka hapa mkoani, walikwenda huko na kufanya upekuzi katika nyumba ya Mtasha ambapo walikuta mguu wa kushoto ukiwa umefukiwa kwenye takataka ndani ya ua wa nyumba yake. Kwa hiyo, hivi tunavyozungumza watuhumiwa wote wameshafikishwa hapa mkoani, tunaendelea kuwahoji ili tujue ni kwa nini wanamiliki mguu huo na wameutoa wapi,” alisema Kamanda Nyombi.

  Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa polisi, mguu huo ni wa kushoto na ni kipande kilichoanzia gotini hadi kwenye nyayo.

  Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Shambwee Shitambala, alisema kukamatwa kwa Mtasha ni pigo kwa chama hicho kwa kuwa alikuwa ameahidi kukisaidia chama wakati wa uchaguzi mkuu.

  “Taarifa za kukamatwa kwa Mtasha ninazo ila inaonekana kuna mazingira ya kisiasa kwa sababu ni juzi tu amerudisha fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Makongorosi. Katika tukio hili nasikia mtoa taarifa alimpigia simu RPC badala ya OCD wa Chunya, kisha askari polisi wakatoka Mbeya Mjini kuja kuwakamata watuhumiwa Chunya wakati hata hapo Chunya kuna polisi,” alisema Shitambala ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

  Mtasha amekuwa Mwenyekiti wa Chadema tangu chama hicho kilipoanza kujulikana mkoani Mbeya miaka mingi iliyopita. Aliondolewa katika wadhifa huo Machi mwaka huu baada ya kushindwa katika uchaguzi uliomweka madarakani, Sambwee Shitambala.

  Source: mtanzania
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Source: mtanzania =RA
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kweli uchaguzi umeanza, na tuangalie habari hizi zinaletwa na magazeti ya nani.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  NAdhani kama ni habari ya kweli haina madhila ya nani katoa habari.
  Kama sisi tunawananga sana mafisadi basi tuwaache watunange endapo na sisi tunafanya madudu.

  Tuwe makini ktk kila hatua tuipigayo
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  kwa staili hii hatuwezi kufika kamwe............
   
 7. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  :pray2::hail:........:amen:
   
 8. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 999
  Trophy Points: 280
  Hii inawezekana niya kweli lakini mazingira ya upatikanaji wa huo mguu yana walakini.Upatikanaji wa huo mguu nje ya nyumba kwenye takakata unatia mashaka makubwa.Kitu gani kimeshinda mtuhumiwa kuuficha ndani ya nyumba au kuuchimbia chini na badala yake aliyekuwa mwenyekiti wa chama na mgombea mtarajiwa ameona sehemu ya muhafaka ni kwenye takataka ambapo mfanyakazi wa nyumbani anaweza kuuona.

  Kwa sababu huo mguu umepatikana kwenye takataka nawala sio ndani ya nyumba au chini ya ardhi, mpigaji simu ana maswali ya kujibu.
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  aliyepiga simu ndiye anajua kinachoendelea. Advocate Nyombi ambane naye pia
   
 10. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Hii habari ni ya kweli, ila kuna walakini mkubwa sana kwa polisi!, haiwezekani mtu katika mazingira ya kawaida uamke asubuhi ukute kwako kuna mguu wa mtu jalalani!, fitina ya siasa ni mbaya sana! wenyeji wanamjua hata aliyeweka mguu kuwa ni mpinzani wake wa kisiasa! sasa mix with yours
   
 11. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,424
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Rais alizungumza vizuri sana hivi karibuni kwamba atavishughulikia vyombo vya habari vyenye kuzua taarifa kwa nia ya kugawa taifa. Mwanzo wa taarifa hii ulinishtua sana, na imenichukua muda kujikusanya lakini picha inayokuja sasa ni pengine kilichotokea, kutegeshewa kiungo cha binadamu!!! NOooooooo haiji, whatever happened whether ni wapinzani wa mchadema au la, kweli tumefika hapo, kiungo cha binadamu kwa ajili ya siasa...kuna nini kwenye siasa? Kwa nini wasingemtegeshea hata paka basi?
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  YYaani CHADEMA ni washirikina ?
   
 13. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yawezekana wakabambikiwa kama ni tishio kwa chama chawala
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Alisema MAKAMBA
  dhambi ya mtu mmoja usikihusiche CHAMA.
  so do the same
   
 15. H

  Haika JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mwandishi kaniacha hoi alipokuwa anahoji watu kwa kufuata dini zao na viongozi wao, kweli amefanya utafiti, ila utafiti umetoka nje ya mada!!!
  habari ni nzito ila unandishi unaifanya ikose maana!!
  Mguu wa mtu! jamani nadhani polisi watatupa jibu la kueleweka manake sio jambo dogo hata kidogo.
  hakuna siasa ya hivyo. huo ni uhalifu.
  kama kasingiziwa au kauweka tungeshukuru sana kama waheshimiwa waandishi mkutufahamisha kwa kituo, habari yenyewe.
   
Loading...