Mbunge mstaafu: Hili suala la CAG ingekuwa enzi za Spika Sitta angelimaliza kwa dakika 5 tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,883
141,815
Aliyekuwa mbunge wa Kahama mzee Lembeli akijibu swali la mtangazaji Hassani Ngoma kuhusu mgogoro wa CAG na Spika amesema mgogoro uliopo ni jambo dogo sana linalohusisha tafsiri ya neno Dhaifu.

Angekuwa Spika Sitta suala hili angelitatua ndani ya dakika 5 kwani kwa busara zake asingeruhusu watu wazima wawili wagombane kwa sababu ya tafsiri.

Lembeli anasema Sitta alikuwa ni chuma cha pua na hakuiogopa Serikali hata siku moja bali Serikali ndio ilimuogopa Spika na bunge kwa ujumla.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ni kweli kabisa. Kama JK alivyomaliza mgogoro wa Zanzibar ni nchi au sio nchi kwa sekunde 30 tu.
Aliingia pale Bungeni akasema, 'kuna mambo mengine yanahusu nchi ya Z'bar na mengine yanahusu nchi ya Tz'... Akarudia tena kusisitiza. Toka hapo mgogoro ukayeyuka kama Ice cream ya Azam.
 
Ndugai mpaka amfukuzishe kazi CAG ndiyo atajisikia raha, kama alimchapa fimbo ccm mwezake nusura ya kumuua na bado ccm wakamuacha unategemea nini, na bado akaja bungeni mbele ya hadhara akajisifu na kutamba kuwa alilichapa liccm lenzake nusura ya kuliua utasema huyo ni mtu
 
Sitta alijitahidi (ukiacha Bunge la Katiba) na ndiyo sababu iliyomnyima nafasi kwa mara nyingine,Mijadala ilikua moto, Lowasa alijiuzulu, ila baada ya kuitwa vikao vya ndani akawa mpole, Alivyopigwa chini akataka kujiunga CDM lakini JK akamuwahi akampa Uwaziri.
Spika wa sasa ni Dhaifu.
 
Job safari hii kayakanyaga sijawah ona mtu jeuri kama Assad

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua kuna vijineno vidogo vidogo
Example; Love minus Truth is literary referred to Cruelty.
Then, Truth minus Love is merely the hypocrisy

Kuna haja ya kuobserve hiyo inshu clearly both sides.

Ila hili haliondoi ukweli kuwa udhaifu ni dhaifu
 
Aliyekuwa mbunge wa Kahama mzee Lembeli akijibu swali la mtangazaji Hassani Ngoma kuhusu mgogoro wa CAG na Spika amesema mgogoro uliopo ni jambo dogo sana linalohusisha tafsiri ya neno Dhaifu.
Angekuwa Spika Sitta suala hili angelitatua ndani ya dakika 5 kwani kwa busara zake asingeruhusu watu wazima wawili wagombane kwa sababu ya tafsiri.
Lembeli anasema Sitta alikuwa ni chuma cha pua na hakuiogopa Serikali hata siku moja bali Serikali ndio ilimuogopa Spika na bunge kwa ujumla.
Maendeleo hayana vyama!
Ukionana naye mwambie aache mbwembwe.Yeye ni mbunge aliyekwama kwenye kura za maoni.Siyo "mbunge mstaafu"! Msisitizie hilo.
 
Ni kweli kabisa. Kama JK alivyomaliza mgogoro wa Zanzibar ni nchi au sio nchi kwa sekunde 30 tu.
Aliingia pale Bungeni akasema, 'kuna mambo mengine yanahusu nchi ya Z'bar na mengine yanahusu nchi ya Tz'... Akarudia tena kusisitiza. Toka hapo mgogoro ukayeyuka kama Ice cream ya Azam.

Ni kweli kabisa hata wapemba baada ya pale waliipenda sana Ccm na hata 2015 maalimu seif hakuchakachuliwa ila alishindndwa kihalali kabisa.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo Mzee lembeli aangalie maana Jiwe na Ndugai sio watu asije akashtukia anarudishiwa deni lake la benki ambalo alifutiwa baada ya kurudi ccm .
 
Back
Top Bottom