Mbunge Msabaha (CHADEMA): Baadhi ya wabunge vijana ni Mateja

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Akichangia katika bajeti ya wizara ya ulinzi Mariam Msabaha amefyatuka akidai kuwa baadhi ya wabunge vijana wanatumia madawa ya kulevya na hivyo kumuomba Raisi Dr.Magufuli kuamuru wabunge hao wapelekwe JKT kufundishwa nidhamu.

Rai yangu kwa wabunge mambo ya "baby","bangi","shanga" hayajengi na yanahalalisha hoja ya kutoonyesha bunge "live".

===================

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ametoa tuhuma nzito kuwa ndani ya Bunge kuna wabunge vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za kulevya.

Mbunge huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo ambao hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kufundishwa nidhamu.

Msabaha ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.

“Wabunge nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana wengine ambao ni mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine wanawavua mama zao nguo,” amesema Msabaha.

“Wengine mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi wao. Kwa hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana nidhamu waende JKT,” alisisitiza.

Mbunge huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya kuzungumza ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema waende JKT ili wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.

Ingawa hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango ulioibua mtafaruku bungeni ni wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti maalumu Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.

Tafsiri ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima wafanye mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka ndani ya chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.
 
Akichangia katika bajeti ya wizara ya ulinzi Mariam Msabaha amefyatuka akidai kuwa baadhi ya wabunge vijana wanatumia madawa ya kulevya na hivyo kumuomba Raisi Dr.Magufuli kuamuru wabunge hao wapelekwe JKT kufundishwa nidhamu.

Rai yangu kwa wabunge mambo ya "baby","bangi","shanga" hayajengi na yanahalalisha hoja ya kutoonyesha bunge "live".
Huyo mbunge wa upinzani anayemuomba rais awaadabishe wabunge anaelewa kazi ya bunge na mipaka ya rais?

Alishawahi kusoma katiba au ndio wale wabunge wa kupata ubunge kwa uhawara?
 
Huyo mbunge wa upinzani anayemuomba rais awaadabishe wabunge anaelewa kazi ya bunge na mipaka ya rais?

Alishawahi kusoma katiba au ndio wale wabunge wa kupata ubunge kwa uhawara?
Mkuu hawaiti uhawara wao wenyewe wana msemo wao pale mjengoni.

Wanapata ubunge kibaby baby
 
Halafu hapo hapo Upinzani wanalaumu Magufuli kuingilia Bunge, wakati huo huo wanamwomba awatumbue.....
Ndiyo maana nikasema huyu mbunge hata katiba kashawahi kusoma? Anaelewa concept ya checks and balances? Anawasikiliza hata viongozi wa chama chake wanasemaje?

Huyu mbunge kwa kweli kawaaibisha sana CHADEMA na Zaidi ya hapo kaliaibisha sana bunge.
 
Yupo bungeni lakini hajui wajibu na kazi za bunge na wabunge. ndiyo maana Mzee Warioba alipendekeza kuondoa viti maalum.
Siku wabunge wenye nguvu bungeni (wabunge wa CCM) wakikubali pendekezo hilo nifahamishe tafadhali.

Tunang'ang'ania viti maalum kwa minajili ya kusema 50-50 yaani usawa wa kijinsi. Wakati nchi zinazopigia chapuo hiyo 50-50 zenyewe hazina mambo kama hayo. Wanawake wao wapo liberated, lakini kwenye vyombo vya maamuzi hakuna usawa hata punje. Sasa sisi vinchi maskini tumeshikilia bango la 50-50 kwa sababu nafasi hizo ni za kupeana. Angalau zingekuwa zinatolewa kwa merits ningeona afadhali.
 
inawezekana kuna ukweli hao ni mateja kama wana akili Timamu kuna baadhi ya vitu haviwezi kupitishwa na yule alitaka bangi ihalalishwe kuvuta...
 
nadhani alikuwa anazungumzia lilie teja la Ulanga Mashariki.
BUNGENI: Mbunge viti maalum Mariam Msabaha (CHADEMA) asema baadhi ya wabunge vijana ni Mateja.

Siyo teja usitake kubadilisha kauli ya mbunge wetu.
 
Back
Top Bottom