Mbunge Mpina: Spika Tulia unda tume ya bunge, hutakuja kunisahau maishani

Bikirajohola

JF-Expert Member
Jun 11, 2022
356
632
Dodoma. Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameendelea kuing'ang'ania Wizara ya Nishati kuhusu mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Julius Nyerere safari hii alitaka iundwe tume ya kuchunguza.

Mpina ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 20, 2022 bungeni wakati akichangia hoja ya bajeti kuu ya serikali.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kuzungumzia ujenzi wa bwawa hilo akidai kutoridhishwa na mwenendo wake.

Mbali na uchunguzi wa ujenzi wa bwawa i ameomba Bunge liunde tume kuchunguza kupanda mwa bei ya mafuta na mbolea.

Katika mchango bungeni leo, waziri huyo wa zamani wa Mifugo na Uvuvi amemwambia Spika, Dk Tulia Ackson kuwa akiunda tume kuchunguza mambo hayo, hatamsahau kabisa katika maisha yake.

"Naomba kukupa ushauri ambao hutakaa unisahau Katika maisha yote, naomba uunde tume kuchunguza ucheleweshaji wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere. Unda tume ichunguze kupanda Kwa bei za mafuta pamoja na sababu za vita, unda tume ichunguze kupanda bei ya mbolea, utakuja kunikumbuka," amesema Mpina.

Katika mchango wake mbunge huyo amezungumzia uamuzi wa serikali kutaka kubadilisha matumizi ya shamba la mifugo la lanchi ya Kongwa kuwa shamba la alizeti kwamba hayaonyeshi umuhimu wa kuwajali wafugaji.

Amebainisha kuwa maeneo mengi ikiwemo Mkoa wa Tabora ambako wangeweza kufyeka na kulima lakini kuing'ang'ania Kongwa ni uamuzi unaopaswa kupingwa na wabunge wote.
 
Kweli na HAKI hujisimamia. Asante Kwa ushauri Kwa Spika.

Mungu akubariki ndugu Mpina. Amen
 
Mpaka chumvi imepanda ukiukiza unaambiwa Vita ya Russia. Hatari sana. Ndugu Mpina Mungu akulinde Majizi yanafanya yanavyotaka.
 
Atakuwa ametumwa na ndugai ...maana ndugai hataki Ranchi ya kongwa iwe shamba...huyu ndo anatangulizwa front kwenye lile kundi maarufu "SUKUMA GANG"...ngoja tuone kama watashinda maana muda ni mwamuzi mzuri
 
Dodoma. Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ameendelea kuing'ang'ania Wizara ya Nishati kuhusu mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Julius Nyerere safari hii alitaka iundwe tume ya kuchunguza.

Mpina ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Juni 20, 2022 bungeni wakati akichangia hoja ya bajeti kuu ya serikali.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kuzungumzia ujenzi wa bwawa hilo akidai kutoridhishwa na mwenendo wake.

Mbali na uchunguzi wa ujenzi wa bwawa i ameomba Bunge liunde tume kuchunguza kupanda mwa bei ya mafuta na mbolea.

Katika mchango bungeni leo, waziri huyo wa zamani wa Mifugo na Uvuvi amemwambia Spika, Dk Tulia Ackson kuwa akiunda tume kuchunguza mambo hayo, hatamsahau kabisa katika maisha yake.

"Naomba kukupa ushauri ambao hutakaa unisahau Katika maisha yote, naomba uunde tume kuchunguza ucheleweshaji wa ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere. Unda tume ichunguze kupanda Kwa bei za mafuta pamoja na sababu za vita, unda tume ichunguze kupanda bei ya mbolea, utakuja kunikumbuka," amesema Mpina.

Katika mchango wake mbunge huyo amezungumzia uamuzi wa serikali kutaka kubadilisha matumizi ya shamba la mifugo la lanchi ya Kongwa kuwa shamba la alizeti kwamba hayaonyeshi umuhimu wa kuwajali wafugaji.

Amebainisha kuwa maeneo mengi ikiwemo Mkoa wa Tabora ambako wangeweza kufyeka na kulima lakini kuing'ang'ania Kongwa ni uamuzi unaopaswa kupingwa na wabunge wote.
Usukuma unamsumbua. Tangu shetani kufariki hawajatulia hawaamini kama zama zao zimekwisha
 
Back
Top Bottom