Mbunge mmoja wa CHADEMA sawa na Wabunge 20 wa CCM

Status
Not open for further replies.
Hauko Tanzania, kama uko Tanzania chadema wana wabunge wa 5 CUF wanawabunge 19...is 19>5? ushabiki mwingine aibu kuwa great thinker???

Talk of the absurd !

  • Kulingana na takwimu za uchaguzi 2005, wabunge 5 wa Chadema walichaguliwa na jumla ya wapiga kura karibu 900,000 kwa wastani wa wapiga kura karibu 200,000 kwa kila mbunge.

  • Wabunge 19 wa CUF walichaguliwa na wapiga kura karibu 200,000 kwa wastani wa wapiga kura elfu kumi kwa kila mbunge.
 
HIvi hamjachoka na hizi hotuba zao na haya ya Operesheni Sangara na Sato? Hivi Operesheni hii imezaa matunda kiasi gani kule kanda ya ziwa:

Matawi mangapi yameanzishwa?
Wanachama wangapi wamepatikana?
Kiasi gani kimepatikana na michango kwa chama?

Naungana na wewe mzee Mwanakijiji. Impact ya hizo sijui operation Sangara wala haionekani. Tulitegemea baada ya haya yote tuone japo mabadiliko kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa mambo ni yale yale. Halafu huyu anayesema Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na 20 wa CCM. sijui kama lina ukweli wowote. Kwa kuwa hata hao CHADEMA, wabunge waongeaji na wenye point za maana bungeni si zaidi ya watatu. Na waongeaji kwa upande wa CCM ni zaidi ya 40, machachari kabisa ni zaidi ya 10, sasa huo uwiano wameutoa wapi?
Na la mwisho, mimi siikatai CHADEMA, naweza kusema ni second best part in Tanzania (msiniulize first) lakini bado siwaelewi focus yao ipo wapi? Maana kila siku stori zao ni ufisadi tu. Wakiingia madarakani watawafanyia nini watanzania, kivipi?
 
Kibaya zaidi wanaongelea agenda moja ufisadi ufisadi??

Ninavyoelewa mambo mengi wanayaongelewa kwenye hiyo mikutano lakini waandishi kwa sababu zao wanalipa swala la ufisadi umuhimu zaidi.

Elimu vipi? afya vipi? barabara na makazi vipi? mishahara na pension vipi? kilimo vipi?

Nakuomba uhudhurie mikutano ya Operation Sangara usikilize sera zinavyochambuliwa toka elimu hadi maji, toka afya hadi barabara to toka ajira hadi kilimo. Tatizo ni kuwa mipango yote ya maendeleo yahitaji pesa na pesa zinaliwa na panya.
wanatumia party resources (mikopo) for one agenda for four years? sipati picha wanachama kama wanaelewa na kama kuna justification ya allowances, perdiem kwa viongozi dull kama hawa.
Kama nilivyosema hapo juu hudhuria hiyo mikutano - nina hakika siku hiyo utaachana na CUF na utatafuta kadi ya chama makini. Ndugu yangu, mfuko wa hazina ya taifa umetoboka na hakuna kitachowezekana bila kwanza kuwaangamiza panya wanaotoboa mfuko kisha kuziba tobo.
 
Hiki kipimo cha Mh Mbunge Mmoja wa CHADEMA kuwa sawa na wabunge 20/50 wa CCM kimepatikana vipi? Nisaidieni. Kwa mchango wa mtoa mada hapo juu, bado sijafunguliwa kichwa changu. Nahitaji kulishwa zaidi hapa!.

Nadhani kama nitapata majibu yanayopimika (qualitative measures) kwa kigezo cha maendeleo ya kwenye majimbo, hicho kitakuwa ok. Tunaweza kupata quantitative measures pia; lakini siyo kwa kuangalia idadi ya kuchonga sana bungeni!
 
HIvi hamjachoka na hizi hotuba zao na haya ya Operesheni Sangara na Sato? Hivi Operesheni hii imezaa matunda kiasi gani kule kanda ya ziwa:

Matawi mangapi yameanzishwa?
Wanachama wangapi wamepatikana?
Kiasi gani kimepatikana na michango kwa chama?

Asate MM, Ila kumbuka vuguvugu la ukombozi haliji siku moja na hiyo ndiyo key kwa CHADEMA.
 
Naungana na wewe mzee Mwanakijiji. Impact ya hizo sijui operation Sangara wala haionekani. Tulitegemea baada ya haya yote tuone japo mabadiliko kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa mambo ni yale yale. Halafu huyu anayesema Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na 20 wa CCM. sijui kama lina ukweli wowote. Kwa kuwa hata hao CHADEMA, wabunge waongeaji na wenye point za maana bungeni si zaidi ya watatu. Na waongeaji kwa upande wa CCM ni zaidi ya 40, machachari kabisa ni zaidi ya 10, sasa huo uwiano wameutoa wapi?
Na la mwisho, mimi siikatai CHADEMA, naweza kusema ni second best part in Tanzania (msiniulize first) lakini bado siwaelewi focus yao ipo wapi? Maana kila siku stori zao ni ufisadi tu. Wakiingia madarakani watawafanyia nini watanzania, kivipi?

tatizo la kutoelewa kwako siyo la chadema na siyo letu pia.
 
Ufisadi ndio ajenda...pekee lol

hapo ndipo mnaboa wananchi, ufisadi hauondolewi jukwaani ...na nchi haichukuliwi kwa ajenda moja???

Kama wananchi hawatawapa nchi ufisadi utaondokaje?...kama mdau (mwananchi) nahitaji kusikia areas kama afya, elimu, barabara, biashara, zinazungumza vipi? ili niwape kura??

besides si CCM nao wanasema wanapinga ufisadi? na mafisadi? sioni mantiki ya kuongelea miaka minne agenda moja...na wala hakuna tija zaidi ya kupoteza media air time/space, resources (scarce) ...badala kutoa alternatives wanaimba ngojera..lol
Sikiliza ndugu yangu, tunakatwa kodi ili hiyo pesa iende kwenye elimu, shule, hospitali, to mention just a few. Pesa hiyo ya kodi inafanyiwa ufisadi haifanyi hiyo kazi...hebu nambie sasa utaongelea nini kama sio ufisadi?
 
Nafikiri CHADEMA kuna kitu wana kioverlook hapa, pamoja na umakini unozungumziwa wanawezaje kukubali kuingia kwenye chaguzi bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, je wanategemea miracles itokee au vipi? Honestly i cant comprehend this, nafikiri pamoja na Operation Sangara nadhani wangespearhead swala la tume huru kwa nguvu zote, naona NCCR wanahangaika peke yao tu mahakamani, CHADEMA hawalioni hilo? Kama ni kuungana basi vyama vyote vya upinzani vingefanya kazi pamoja ili in the end ipatikane tume huru, vinginevyo kwa jinsi tulivyo watanzania CCM na mfumo wao wa kifisadi haung'oki. Kwa nchi kama Kenya au Zambia wananchi can decide to remove a poorly performing party madarakani through the power of ballot cos they have the ability to link poor governance and their misery, but majority of Tanzanians cannot...vyama vya upinzani tafuteni ukombozi kwenye tume huru, please!
 
Haya tuendeleze mapambano..Hebu naimabieni ni wabunge wa chama gani wengine waliofanya kazi kama hawa wa CHADEMA?Mpaka sasa?
 
Kauli kama hii niliisikia nilipokuwa JKT. Koplo mmoja ni sawa na kuruta tisa. Waambieni CHADEMA watengeneze documentaries za maajabu kama yale ya hospitali ya Mwananyamala ambako akina mama waliojifungua wanalala chini. Wazionyeshe kwa wananchi kwa mfumo wa sinema zikiwa na maelezo mazuri, rahisi ya kina bila kutia chumvi. Hii agenda ya ufisadi haitawafikisha kokote.
 
- Yale yake ya Yanga na Simba, huku wananchi wanazidi kuwa masikini wakati wabunge wote wa CCM na Chadema, wakikusanya marupurupuya ajabu sana, wakihudhuria vikao Dodoma, na kurudi Dar for the weekend kabla ya kurudi tena Dodoma kuendela na vikao huku wote waki-pollute hewa yetu bigtime na mshangingi mengi ya reconditioned, ambayo kwa majuu ni written off kwa sababu hayako efficient kwenye emissions,

- I mean we can go on and on, kuhusu kufanana kwao huyo Kiwelu si kuna wakati huwa anasafiri na lile kundi la Muungwana, hivi nini cha maana amewahi kufanya kwenye hizo safari na Muungwana kwa taifa hili?

- Ndio maana sometimes huwa ninasema it is about time sasa tuka do away na vyama vyote vya siasa nchini na kuanza upya, maana inaudhi sana!

Respect.

FMEs!

Kaka umekata tamaa, hakika siku zote mpigani hakati tamaa huwa anapigana hadi risasi yake ya mwisho.
 
Chadema wakiendelea na Sangara bila kuimarisha mfumo a chini watakuwa wanatwanga maji kwenye kinu,kinachotakiwa ni matawi ya kuanzia ngazi ya chini na sasa hivi wakazie vijijini miji midogo na mijini masomo ya mapinduzi ya kisiasa yanawapata pata vijijini mbako ndiko watanzania wengi wapiga kura ambao wengine hawajui kusoma na kuandika wamejaa,waende huku.
Lingine ni lile na kuhamasishwa wale wasio na vyama kuwaunga wao mkono kwa kuhakikisha agenda yao ya msingi inaeleweka vizuri,vinginevyo upepo sasa hivi uko kwao na CUF wakitumia karata yao vizuri,yaani ulinizi wa Kura ni muhimu sana kuuwekea mkakati,mambo mengi nchi hii imejaa vijana chadema wakiwaonyesha ni jinsi gani wanapunjwa haki yao kama wakazi halisi wa nchi kwani ndio wao watakuwepo baada ya miaka hamsini ijayo na ndio watakao lipa madeni makubwa makubwa ambayo serikali inayatengeneza,na ndio watadhurika na uharibifu wa mazingira na ukosefu wa ardhi kutokana na wageni kunufaika,
waandae vipindi vya uamsho kwenye radio na television lenga zaidi vijana
 
Kauli kama hii niliisikia nilipokuwa JKT. Koplo mmoja ni sawa na kuruta tisa. Waambieni CHADEMA watengeneze documentaries za maajabu kama yale ya hospitali ya Mwananyamala ambako akina mama waliojifungua wanalala chini. Wazionyeshe kwa wananchi kwa mfumo wa sinema zikiwa na maelezo mazuri, rahisi ya kina bila kutia chumvi. Hii agenda ya ufisadi haitawafikisha kokote.

Mkuu unafikiri,haya yanyoteka Mwananyamala hosp ni matokeo ya nini,si ya ufisadi na uongozi mbovu,kama kungekuwa hakuna matumizi mbaya ya fedha hivi hospitali hizi zingekosa huduma bora?come on man,mbona ujicontradict mweyewe?
 
Chadema wakiendelea na Sangara bila kuimarisha mfumo a chini watakuwa wanatwanga maji kwenye kinu,kinachotakiwa ni matawi ya kuanzia ngazi ya chini na sasa hivi wakazie vijijini miji midogo na mijini masomo ya mapinduzi ya kisiasa yanawapata pata vijijini mbako ndiko watanzania wengi wapiga kura ambao wengine hawajui kusoma na kuandika wamejaa,waende huku.
Lingine ni lile na kuhamasishwa wale wasio na vyama kuwaunga wao mkono kwa kuhakikisha agenda yao ya msingi inaeleweka vizuri,vinginevyo upepo sasa hivi uko kwao na CUF wakitumia karata yao vizuri,yaani ulinizi wa Kura ni muhimu sana kuuwekea mkakati,mambo mengi nchi hii imejaa vijana chadema wakiwaonyesha ni jinsi gani wanapunjwa haki yao kama wakazi halisi wa nchi kwani ndio wao watakuwepo baada ya miaka hamsini ijayo na ndio watakao lipa madeni makubwa makubwa ambayo serikali inayatengeneza,na ndio watadhurika na uharibifu wa mazingira na ukosefu wa ardhi kutokana na wageni kunufaika,
waandae vipindi vya uamsho kwenye radio na television lenga zaidi vijana

Unajua Operesheni Sangara inafanya kazi gani au unajisema tu?jamani hili jukwaa ni huru but unatakiwa kuwa na facts kwanza kabla hujatoka.Kazi mojawapo ya Operesheni Sangara ni kuhakikisha chama kinakuwa na matawi katika kila sehemu ambako Sangara inapita na hakuna matawi..Hivi huji kuwa Sangara inatoba mpaka vijijini?pole wee huna hata habari...Sangara inapita katika Kata zote za kila jimbo tunakopita...Unajingine?
 
Wakuu kwanza niombe radhi kwa kutokuwa hewani kwa muda kidogo.Nisingependa nitoe sababu za kutokuwa kwangu hewani. Kwa sasa niko likizo mkoani Tanga.Nikiwa huku Tanga nimepata bahati ya kuhudhuria Operesheni Sangara ya CHADEMA,kwakweli CHADEMA wanajitahidi kuchanja mbuga.Katika speeches nilizovutiwa nazo katika operesheni hii ni hii ya Mbunge Grace Kiwelu,yeye alisema kwamba Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 20 wa CCM kwa utendaji,akadai kwamba wabunge wengi wa ccm sio watendaji kazi yao ni kupiga makofi tu wanapokuwa bungeni.Nakubalina na kauli ya Mbunge huyu kwamba CHADEMA imejaliwa kuwa na wabun ge vichwa na CCM imejaza makapi.Ila mimi naongeza kwamba mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 50 wa CCM

Saaaafi sana, tatizo la Chadema ni kwamba baada ya kujitambulisha wamepotea.... hakuna presence kwenye maisha ya watu
 
Ndio maana niliuliza kwenye ile makala wapiganaji CCM wanapigania nini? Hadi leo sijapata jibu la kuridhisha.

Hili ni kweli.. ndio maana hutasikia wapiganaji wetu wakipigana kuubadilisha mfumo wa utawala wa kifisadi (MUK); wanachotaka wao ni kubadilisha mafisadi wa sasa ili wao waingie na kwa vile mashine ya kukoboa mafisadi inafanya kazi yake bila kukoma basi utaona watakaoingia uadilifu wao utakobolewa na wao wataibuka kama mafisadi wapya.. bila ya kubadili mfumo vita ya ufisadi haina maana ni geresha tu!

Ebwana umemujibu. Tatizo hapa ni mfumo na bila kuubadilisha 2nafanya kazi bure kabisa
 
Unajua Operesheni Sangara inafanya kazi gani au unajisema tu?jamani hili jukwaa ni huru but unatakiwa kuwa na facts kwanza kabla hujatoka.Kazi mojawapo ya Operesheni Sangara ni kuhakikisha chama kinakuwa na matawi katika kila sehemu ambako Sangara inapita na hakuna matawi..Hivi huji kuwa Sangara inatoba mpaka vijijini?pole wee huna hata habari...Sangara inapita katika Kata zote za kila jimbo tunakopita...Unajingine?
Huna sababu ya kuhamaki ule ulikuwa ni mchango wangu mimi si mwana sangara kama unahitaji maoni kwa kuanzisha hii thread ungenielewesha sio kunizobodoa vipi wewe ,unakurupuka hasira ya nini umeanzisha mjadala acha tuchangie usilete za kuleta ,matawi mangapi katika vijiji vya nchi hii,karibu zaidi ya na kata ndio swali letu
Kichwa kibovu nini kama wana CCM
 
Mimi kwa mtazamo wangu nadhani tatizo sio Chadema ila sisi wenyewe. Kusema kweli Tanzania ninchi ya Wajinga na Malimbukeni ambao wanajifanya kufahamu sana vitu hali hatufahamu kitu kabisa.

Chukulia mfano wa Ufisadi, watu wengi wanafikiri sio big deal la kutukwaza, ila ati Chadema watafanya nini wakichukua nchi.. Akili yao zaidi imegota ktk kuboresha maisha ya watu, lakini wanasahau kwamba huwezi kujaza maji pakacha lililotoboka na kuvuja maji kwa maana kwamba Huwezi kuboresha uchumi wa nchi ikiwa kuna mirija inayoharibu uchumi huo. Hakuna Itikadi inayoweza kufanya kazi pasipo kwanza kuziba tobo za hili pakacha.

Sasa ukiweza kuelewa kina cha Ufisadi nchini na jinsi kinavyoathiri uzalishaji na pato la serikali itakurahisishia mtu kuelewa Chadema wataweza kufanya nini na hizo fedha ambazo leo zinapotea bure. Ikiwa Chadema wataliwezesha pakacha letu kujaa pasipo kuvuja, hapo ndipo unaweza kuwauliza Chadema watafanya nini.. wanachosema Chadema ni rahisi kabisa kwamba - Tusipoziba Ufa leo tutakuja jenga Ukuta, watanzania wanataka kuona jengo limesimama ktk ukuta ulokuwa na ufa... makubwa haya jamani!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom