Mbunge Mlinga: BoT wanatibiwa nje ya nchi sababu wao ni idara nyeti

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mlinga aliituhumu BOT kujifanya kuwa ni idara nyeti sana kuliko usalama wa taifa na idara nyingine za Serikali hivyo wao kutibiwa nje.

Spika amesema kam kuna ukweli ataishauri mamlaka kuchukua hatua stahiki dhidi ya Bodi na menejimenti ya Benki Kuu (BOT).

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kukaa Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Shirikia la Taifa la Bima ya Afya (NHIF) kuchunguza hoja iliyoibuliwa na Mbunge Gooluck Mlinga kwamba BOT hawajajiunga na NHIF na wao wanatibiwa nje ya nchi.
 
TRA waokusanya pesa wanalazimishwa NHIF, hao wanaotunza wao wanatibiwa nje? Kama ni kweli kuna walakini
 
Ndugai yeye huwa anatibiwa ndani ya nchi??
Tuanzie hapo kwanza.
Mpaka sasa pesa zilizotumika kwa matibabu ya Ndugai ni siri kubwa inayolindwa mithili ya ukuta wa Mererani. Tetesi za kimya kimya zinadai ni kiasi kikubwa ambacho kikitamkwa wananchi wengi wanaweza wakazimia kwa mshtuko!
 
Mbona hajatoa agizo kama hilo kuhusu ile 1.5 trilioni?

Baada ya muda hii issue unaweza usiisikie tena.

Nasikia hata watumishi TRA nao hawapo kwenye mpango wa bima ya afya sasa kama ni kweli nao vile vile ni idara nyeti?
 
TRA waokusanya pesa wanalazimishwa NHIF, hao wanaotunza wao wanatibiwa nje? Kama ni kweli kuna walakini


Wanaovuja jasho kuipa serikali wakifa wote je hao wanaotibiwa nje itakuwaje

Nilidhani mazingira ya matibabu ndani ya nchi yangeboreshwa ili sote tutibiwe ndani ili kukamilisha mzunguko wa kutegemeana ...mtunza frdha awe hai ili apokee fedha toka kwa mkusanyaji hai anyekusanya kutoka kwa mtafutaji hai
 
Sekta nyeti mnazistress sijui mnataka nini?Kimsingi TRA,BOT zinaitaji special treatment kwenye maslahi yao na huduma kama za matibabu.Afisa wa TRA anayekusanyia serikali Billioni 10 kwa mwezi hastahili kukaa siku nzima kwenye foleni za NHIF,pia mishahara sitarajii kama TRA na BOT kuna afisa wakulipwa chini ya Mil 5.Tukitaka kuwa salama tusicheze na sekta zinazoendesha nchi jamani.Tukajifunze kwa nchi za wenzetu tusiendekeze wivu wa kike kama che MKapa alivyokua anasema,tuendane na reality.
 
sasa mlitaka na sisi tutibiwe ktk hivi vi-hospitali vya ndani ya nchi km ninyi? acheni masihara bwana.
 
Back
Top Bottom