MBUNGE Mh. Anatropia amjibu Mh. Godluck wa Ulanga

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,162
794
Akizungumza na EATV kuhusu tuhuma hizo Mbunge Anatropia amesema ''Nilikuwa natembea haraka kwenda kwenye kikao na kofia yake iliguswa na mkono kwa kusukumana na kuokotwa na ndiyo maana alivyotoka binafsi nilimsaidia kutafuta aliyeiokota''.

Aidha Mbunge huyo amesema kwamba bado wanazidi kuwasiliana ili kujua mtu aliyeiokota na baraghashia hiyo na kuondoka nayo.
 
Hii ni ishara ya mwelekeo mbaya wa waheshimiwa wetu, wasiojua nini maana ya kuwa MP. ni vema kuelewa kuwa watu wenye mizaha kama hawa sio wazalendo, amepoteza dakika nyingi

amelitia Taifa hasara kujadili mambo ambayo yangewaokoa watazania wenye matatizo mengi.

Kwa sasa rais ametufafanulia kuhusu kusitisha ajira, watanzania wengi wanapata usumbufu kwa taarifa zilizozagaa mtaani vipi wasijadili kutoa hofu watanzania ambapo Bunge ni chombo cha sahihi kutoa fafanuzi hizi.

Wbunge hawa aina ya Godluck ni wengi wanaopotezea taifa muda na kulitia hasara.

Lazima awepo spika wa kumaliza majipu haya.
 
Kwikwikwi. Kofia itadondokea vipi kwenye mkono? Sijawahi ona. Huyu mama analake jambo. Huenda posho zina yoyoma kwa hiyo lazima lufanya maarifa flani flani. Ili mkutane wakati wa kutafuta hiyo kofia.

Unajua kofia sio sindano.
 
Akizungumza na EATV kuhusu tuhuma hizo Mbunge Anatropia amesema ''Nilikuwa natembea haraka kwenda kwenye kikao na kofia yake iliguswa na mkono kwa kusukumana na kuokotwa na ndiyo maana alivyotoka binafsi nilimsaidia kutafuta aliyeiokota''.

Aidha Mbunge huyo amesema kwamba bado wanazidi kuwasiliana ili kujua mtu aliyeiokota na baraghashia hiyo na kuondoka nayo.

Hivi Mbunge huyu naye vipi??? Hii ilikuwa ni hoja ya kutojibu...siamini kama kweli ni maelezo ya Mbunge huyo...maana maelezo haya ni sawa na kukiri...sijui, wabunge wengine wakoje!!!!????
 
Hawa wote hawana hadhi ya kuwa wabunge. Mtu akikuletea hoja ya kipuuzi na wewe ukashindwa kumpuuza basi wote mnakuwa wapuuzi. Mbunge anaitwa Goodluck, ana mtoto anaitwa Glory halafu ana-pretend kuwa muislam. Hii ni kejeli kwa waislamu. Anafanya comedy ndani ya bunge na bunge linampa airtime ya kutosha!
 
Huyu mh. Goodluck amekosea kumuumbua, yeye baada ya mjadala wa bunge angemtafuta kiaina, mh. Anatropia alitoa ishara waonane.......... Huyu kalianika lazima akanushe
 
Antropia dont make it a big deal, ukiulizwa tena jibu kifupi kuwa, sidhani kama hizo ni hoja za kuzungumza bungeni, wananchi wana mahitaji mengi kwa sasa hasa wakati huu tunapodai demokrasia ya kweli na unafuu wa maisha kwa kila mwananchi.
Kwamba nilimtamani muulizeni yeye anaweza jibu vizuri, ahsante.
Antropia you may play smarter than this, go take some free points from that.....#@&%$r
 
Hivi Mbunge huyu naye vipi??? Hii ilikuwa ni hoja ya kutojibu...siamini kama kweli ni maelezo ya Mbunge huyo...maana maelezo haya ni sawa na kukiri...sijui, wabunge wengine wakoje!!!!????
Na hapo kajitahidi kuuficha ukweli.
 
asingemjibu ni upuuzi kumjibu upuuzi kama huo........
Asingemjibu wakati Mwenzie kaomba muongozo! Huwezi kuvaa kanzu bungeni bila kusingiziwa na kibandiko (barghashia)
Ikithibitika kamvua kibandiko anakula adhabu nyingine, kumbuka vikao kumi vinakaribia kuisha.
 
Nini reaction ya mbunge wakati anavuliwa kofia. Nani aliona kitendo hicho na mvuaji alinyosha mkono kweli na kuivua? Na hiyo inahusiana vopi na kutamani. Kwa nn spika atoe maezo kupitia sauti ya upande mmoja bila kumsikia mtuhumiwa? Unadhani yatakuwa ya haki?
 
pamoja na lawama kwa naibu spika,
mimi kanisaidia kulifahamu bunge katika new dimension.

1: mbunge upinzani kudanganya kizembe huku anarudi mtaani kutafuta huruma. Sio sawa.

2:Wabunge wa ccm walivyo wepesi kihoja kiasi kwamba wengi akiwemo na huyu jamaa wa ulanga.

Wamekula posho na muda wa wananchi bure akiwemo na wa Mtera badala ya kuchangia budget wao walichangia ukawa kutoka. naibu nae akiferi aliporuhusu wawakilishi wetu kutumia muda wa thamani kujadili vitu vilivyo nje ya budget hata kama walikuwa wanamtetea.
 
Akizungumza na EATV kuhusu tuhuma hizo Mbunge Anatropia amesema ''Nilikuwa natembea haraka kwenda kwenye kikao na kofia yake iliguswa na mkono kwa kusukumana na kuokotwa na ndiyo maana alivyotoka binafsi nilimsaidia kutafuta aliyeiokota''.

Aidha Mbunge huyo amesema kwamba bado wanazidi kuwasiliana ili kujua mtu aliyeiokota na baraghashia hiyo na kuondoka nayo.
Wabunge wa ccm ni zaidi ya wana futuhi
 
Asingemjibu wakati Mwenzie kaomba muongozo! Huwezi kuvaa kanzu bungeni bila kusingiziwa na kibandiko (barghashia)
Ikithibitika kamvua kibandiko anakula adhabu nyingine, kumbuka vikao kumi vinakaribia kuisha.
kwani huyo anatropia anaingia bungeni??hata akiongezewa adhabu hana cha kupoteza maana wote wa ukawa wameamua kukaa nje
 
Back
Top Bottom