Mbunge Mchafu: Wanaume Tanzania wanajadili zaidi Simba na Yanga kuliko afya zao

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Hawa Mchafu amedai baadhi ya wanaume wa Tanzania wanatumia nguvu kubwa kujadili habari za timu za Simba na Yanga zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kuliko hata kujadili afya zao.

Hawa amesema kama nguvu hiyo ingetumika kujadili masuala ya afya ikiwemo kupima Ukimwi, huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 11, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2021/22.

Amesema wanaume wakikutana maeneo yote wanazungumzia timu hizo zenye upinzani wa jadi nchini badala ya kujadili masuala mengine ya msingi zikiwemo afya zao.

"Wanaume wa Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi virusi vya Ukimwi na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima afya zao si tungeshinda," amehoji Mchafu.

Mei 8, 2021 mchezo kati ya miamba hiyo ya soka nchini uliahirishwa baada ya kutokea mkanganyiko uliosababishwa na ratiba kubadilishwa kutoka saa 11 jioni na kusogezwa mbele hadi saa 1 usiku jambo lililozua sintofahamu huku kila shabiki wa soka nchini akizungumza lake.
Nadhani angeanza kujijadili mwenyewe kwanini yeye ni mchafu
 
Wabunge wengine, basi tu brain zao zimeburn. Simba na Yanga kwa jicho la kawaida anaona Kama timu za kawaida. Simba na Yanga ni hisia za wanaume walio wengi. Ni afya ya akili mahali penye msongo. Mara ngapi amesikia watu wakifa eti sababu CCM imekosa ushindi Jimbo fulani? Lakini watu hufa kwa mshituko pale, Simba au yanga inapoleta matokeo yasiyotarajiwa. Aachane na sisi aendelee na kula posho bila kuwaza sana
 
Yeye mwenyewe majuzi kashindwa kujiandikisha kumuuliza maswali waziri mkuu wakati hapa nchini changamoto kibao...
 
Hajui kitu hobby.

Hisia za furaha zinaboresha afya.
Mkuu hobby ndo ujadili siku nzima?
andalia maana ya hobby-a pursuit outside one's regular occupation engaged in especially for relaxation.
 
"Wanaume wa Tanzania wanatumia muda mwingi kujadili Usimba na Uyanga, hawapimi virusi vya Ukimwi na hawataki kupima, hivi ingetumika muda huo kuzungumza masuala ya kupima afya zao si tungeshinda," amehoji Mchafu.
Moja ya njia ya kupambana na UKIMWI ni ninyi wenyewe wabunge kuacha uchafu na mnyimane kwanza
 
Back
Top Bottom