Mbunge Mary Mwanjelwa apata ajali mbaya, watu kadhaa wapoteza maisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Mary Mwanjelwa apata ajali mbaya, watu kadhaa wapoteza maisha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 2, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Wakuu,

  Kuna tetesi nimepata kuwa Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CCM Dr. Mary Mwanjelwa ni mmoja wa waliopata ajali iliyotokea mkoani Mbeya. Habari zaidi itafuata baada ya mda mfupi nazidi kufuatilia.

  Stay tuned!

  ===============UPDATE===============

  Kuna ajali mbaya imetokea maeneo ya darajani Mbalizi Mbeya. Hio ajali imehusisha magari matatu, moja likiwa ni petrol tank mali ya kampuni ya Lake Oil, pamoja na Hiace na Pick up. Watu wamepoteza maisha ila bado idadi kamili haijaeleweka sababu ya hali mbaya ya mlipuko wa moto na ajali yenyewe.

  Hali sasa ilivo hapo hakuna utulivu kabisa, watu polisi na trafiki wapo kwa wingi katika eneo.

  Inasemekana Mbunge wa viti maalum kapelekwa hospitali ya karibu na hapo maeneo ya Ifisi ilipohamishiwa hospitali ya Lena.

  =========================================================
  Habari zaidi ya maelezo kutoka kwa moja wa walioshuhudia ajali hiyo mbaya;
  =========================================================

  Kwa mujibu wa mtoa maelezo haya toka eneo la tukio ni kuwa gari iliyosababisha ajali hiyo mbaya ni gari la mafuta la Lake oil ambalo lilikuwa likitokea Mbeya mjini. Wakati wa kutelemka huo mlima wa Mbalizi darajani lilifeli break na kusababisha dereva kutaka kulipita gari kubwa aina ya Scania lililokuwa mbele yake kwa mwendo mdogo.

  Katika harakati hizo za kutaka kulipita (yani ku overtake) ndipo lilipovaa gari mbili ndogo za Hiace na gari nyingine inayosemekana ni Nissan Patrol iliyokuwa imetokea Songwe.

  Hali ya magari hayo ni mbaya sana na hilo la Nissan Patrol alilokuwepo Mbunge Mwanjelwa limeteketea kabisa na moto na kusababisha kufariki kwa mmoja wa abiria waliokuwa na mbunge huyo. Hadi dakika hii haieleweki hilo gari la Mbunge walikuwa watu wawili ama watatu. Huyo mmoja aliyeonekana kaharibika vibaya, kwa kuungua kabisa kichwa na miguu yote, kwa ufupi ni kuwa marehemu huyo hatambuliki!

  Kwa madai ya shahidi ni kuwa Mh. Mwanjelwa alipona kidogo kuteketea katika huo moto sababu ndio alibahatika kuwa wa kwanza kuokolewa ingawa naye alikuwa na hali mbaya.

  Idadi ya watu wengi waliopoteza maisha na majeruhi ni abiria waliokuwepo kwenye Hiace. Abiria katika hilo gari la Petrol tank ilikuwa 'tandi boy', mwanamke mmoja na dereva. Hali zao bado haijathibitishwa zipo vipi. Katika gari la mizigo kubwa la Scania, abiria wote wamepona.

   
 2. R

  Rayase Member

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni kweli amepata ajali eneo la mbalizi! ila kapona na anaendelea vema! amelazwa hospitali teule ya wilaya mbeya iliyopo ifisi
   
 3. k

  kigu Senior Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mungu amsaidie apone!!
   
 4. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Pole Hon. wa magamba! get well soon
   
 5. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Nilijua yangetokea haya
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,722
  Likes Received: 12,779
  Trophy Points: 280
  Duuuh umejuaje?
   
 7. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  pole wafiwa na majeruhi
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwa taarifa nilizozikia watu 10 wamekufa papo hapo na watu zaidi ya 25 wamejeruhiwa wamelazwa hospitali ya rufaa mbeya. wenye taarifa kamili tunasomba mtujuze
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,722
  Likes Received: 12,779
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa watu 10 wamekufa papo hapo na 25 wamejeruhiwa, mmoja wa majeruhi ni huyu mbunge!
  Chanzo inasemekana ni kufail kwa break za roli la mafuta na kuanza kugonga magari yaliyo kuwa mbele yake!

  Source:ITV
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  RIP waliopoteza maisha!! Sijui hii tabia ya kuuana itakoma lini! tunathamini mno pesa kuliko uhai wa maisha yetu.
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Poleni wote mlioguswa kwa namna moja ama nyingine na ajali hii.
   
 12. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ungesubiri upate taarifa kamili ndio uilete hapa!! Sasa mtu akisoma kichwa cha habari na kilichomo ndani ataelewa nini? Sio ukisikia tetesi tu unaleta hapa!kama wewe uliyesikia hauwezi kupata/kutafuta taarifa kamili je mimi nisiyekuwa na taarifa yoyote?
   
 13. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Umeziskia kwa nani/wapi??
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Huo mlipuko mnaweza kuuelezea zaidi kidogo, ni wa mafuta ama kishindo cha kugongana kimetafsiriwa kama mlipuko.
  Poleni wahanga.
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kweli enough is enough tunaisha jamaani ajari gani kwa siku?
  ni shetani au? Mungu saidia waja wako
   
 16. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh nilidhani kakamatwa na vitauro vya hotelini tena.lol!

  Mungu ampe afya njema na aweze kumjua zaidi kwa kupitia tukio hili.
   
 17. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,534
  Likes Received: 10,452
  Trophy Points: 280
  ngoja nianze kuwatafuta ndugu zangu mbeya kama wazima. Rip,na poleni majerui.!
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kalumbesa acha gubu,,,mbona kuna update hapo mdau!!!!!
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kumbe ndio huyu????mdau una kumbukumbu
   
 20. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mwenyenzi Mungu awe pamoja nao
   
Loading...