Mbunge Machali amkinga Mbatia dhidi ya uzi wa buibui | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Machali amkinga Mbatia dhidi ya uzi wa buibui

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Relief, Nov 13, 2011.

 1. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Novemba 5, mwaka huu, Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, ilifanya kikao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili ajenda moja maalum iliyohusu mpasuko ndani ya chama hicho.

  Ajenda ya kikao hicho ilitajwa na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza, kwenye kikao hicho.

  Ajenda hiyo ilifuatia hatua ya Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Tanga, Mbwana Hassan, kwa kushirikiana na Kamishna mwenzake Mkoa wa Arusha, Mzee Sirikwa, kumuomba Mwenyekiti wao, James Mbatia, kutafakari kuhusu uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho.

  Makamishna hao wa NCCR-Mageuzi, walimpa Mbatia sababu moja ya msingi ya ombi lao hilo kwake. Kwamba, wajumbe wengi wa NEC-NCCR-Mageuzi wamepoteza imani naye.

  Inaelezwa kuwa makamishna hao walipowasilisha hoja hiyo kwa Mbatia, aliwauliza walikotoa mawazo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwataka wataje majina ya watu waliowatuma kufanya hivyo. Makamishna hao waligoma kutaja majina.

  Ni katika kikao hicho cha NEC, wajumbe 28 wa halmashauri hiyo walijitokeza hadharani. Hiyo ni baada ya kuthubutu kusaini waraka uliobeba hoja ya makamishna hao ya kutokuwa na imani na Mbatia.

  Hoja hiyo imetoa sababu kuu mbili; ya kwanza ikiwa mwenendo wa Mbatia unaodaiwa kuashiria kuwa anatumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo ni pandikizi (wakala) la CCM ndani ya NCCR-Mageuzi.

  Hali hiyo inadaiwa kusababisha Mbatia kuitwa ‘CCM B' na hivyo kudhoofisha uenezi wa NCCR-Mageuzi.

  Sababu ya pili, inatajwa na wajumbe hao wa NEC kuwa inahusu ustaarabu wa kawaida tu. Kwamba, tangu Mbatia awe mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, hajawahi kushinda uchaguzi hata mmoja wa ubunge katika majimbo aliyogombea.

  Baya zaidi, majimbo yote aliyogombea, umma ulikuwa na imani na upinzani. Lakini haukuwa na imani na Mbatia. Na ndio sababu inaelezwa kuwa wakashinda wapinzani wengine na si Mbatia.

  Majimbo hayo ni pamoja na Vunjo. Huko Mbatia aligombea ubunge mwaka 2000, lakini akaangushwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), Jesse Makundi.

  Jimbo lingine ni la Kawe. Huko Mbatia aligombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, lakini akabwagwa vibaya na Mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee.

  Hivyo, hoja ya wajumbe hao wa NEC-NCCR-Mageuzi ikawa kuwa huo ni ushahidi kwamba, watu hawamwamini Mbatia kama mpinzani.

  Lakini zaidi kwa kushindwa huko, anapoteza uhalali wa kuwa ‘kamanda' wa chama taifa. Yaani, hawezi kutangaza mapambano dhidi ya CCM wala hawezi kuthubutu kusema atapambana na chama hicho kilichoota mizizi sehemu kubwa ya nchi ilhali kwenye jimbo tu ameshindwa.

  Lakini pia wajumbe hao wanadai kuwa Mbatia amepoteza hadhi ya kuweza kunadi hata mgombea yeyote wa NCCR-Mageuzi popote ikitokea uchaguzi. Maana hawezi kuuaminisha umma umwamini mgombea anayemnadi ilhali yeye mwenyewe haaminiki anakogombea mara zote.

  Kwenye kikao hicho cha NEC-NCCR-Mageuzi, wajumbe walikwenda mbali zaidi. Mmoja wao kutoka mkoani Ruvuma, Henry Mapunda, alidai kuwa ana ndugu yake ni afisa usalama wa taifa.

  Mapunda alidai ndugu yake huyo aliwahi kumweleza kuwa Mbatia ni mtu wao na kuhoji sababu za watu wa usalama kutamka hivyo?

  Kwa uchache, hicho ndicho kilichojiri katika kikao hicho cha NEC-NCCR-Mageuzi. Mbatia alihudhuria kikao hicho na yote hayo aliyasikia kwa masikio yake.


  Ambacho kilitarajiwa na wengi, ni kusikia Mbatia amejibu au atajibu nini kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwake na wajumbe hao wa NEC-NCCR-Mageuzi.

  Hiyo ni baada ya yeye mwenyewe (Mbatia) kuomba katika kikao hicho atendewe haki, ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi ya kutosha kujibu tuhuma hizo.

  NEC ilimpa siku 21 kufanya hivyo, kuanzia tarehe ya kikao hicho.

  Lakusikitisha wakati umma wa Watanzania ukisubiri majibu ya Mbatia, Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, kwa mlango wa nyuma, ameibuka na kubadili somo.

  Machali anasema tatizo la NCCR-Mageuzi si Mbatia. Ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

  Anadai kwamba, Kafulila, ambaye ni Mkurugenzi wa Uenezi wa NCCR-Mageuzi Taifa, ndiye kinara wa harakati za kumng'oa Mbatia. Anataka uenyekiti wake ili apate fursa nzuri ya kumtengenezea swahiba wake, Zitto njia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 kupitia NCCR-Mageuzi!

  Ni dhahiri kuwa kinachotengenezwa sasa na Machali hapa, ni mkakati wa kutaka kubadili mjadala kutoka kwenye hoja ya msingi iliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi na wajumbe wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na Mbatia kama mpinzani.

  Machali anataka mjadala sasa uwe ni vita ya tamaa na uroho wa kutaka uenyekiti wa Mbatia ndani ya NCCR-Mageuzi na kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015!

  Bahati mbaya mimi kama mtazamaji ni miongoni mwa watu, ambao sikutegemea kama Machali ninayemfahamu angeweza kudiriki kufanya hivyo.

  Nasema hivyo kwa sababu. Bahati nzuri, Kafulila mara nyingi amesikika akitamka kwamba, hatarijii kugombea uenyekiti na wala hajawahi kutangaza kugombea nafasi hiyo.

  Amesikika akisema kwamba, waliotangaza kuwa watagombea uenyekiti kwa kuwa wamekosa imani na Mbatia kama mpinzani, ni Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Hashim Rungwe.

  Machali anajenga dhana nyingine ya kutaka kumgombanisha Kafulila na Chadema. Kwamba, Kafulila anataka uenyekiti ili kuidhoofisha Chadema.

  Anasahau kwamba, yeye (Machali), Kafulila pamoja na Mkosamali, majimbo ya uchaguzi waliyoshinda mkoani Kigoma, ni yale yaliyokuwa yakiwakilishwa na wabunge kupitia CCM tu.

  Zaidi ya hivyo, kuna habari kwamba, Kafulila alihakikisha NCCR-Mageuzi haisimamishi mgombea ubunge katika majimbo, ambayo Chadema ina nguvu.

  Ndio sababu NCCR-Mageuzi haikuweka mgombea katika jimbo la Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini.

  Machali hawezi kuwazuga na kuwapotosha watu wote. Na wala bado hajamsaidia kitu Mbatia. Bali anachokifanya ni kuzidi kumgaragaza Mbatia kwenye matope.

  Nasema hivyo, kwa sababu. Katika kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi, ushahidi mwiingi ulitolewa na wajumbe wa halmashauri hiyo kuthibitisha hoja yao ya kumkataa Mbatia kuwa mwenyekiti.

  Miongoni mwa sababu hizo, ni pamoja na ile inyoahusu kesi ya matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa naye (Mbatia) katika jimbo la Kawe. Wajumbe wanadai kuwa Mbatia ameigeuza kesi hiyo kuwa ya NCCR-Mageuzi.

  Si wajumbe hao tu, bali hilo limekuwa likisikika pia likisemwa na Ruhuza. Kwamba, kesi hiyo siyo ya chama. Bali ni suala la mtu binafsi.

  Hiyo inatokana na wajumbe wa NEC-NCCR-Mageuzi kukataa kufungua kesi kwenye jimbo, ambalo aliyeshinda ni mpinzani kwa vile lengo la wapinzani linatakiwa liwe ni kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani katika Bunge.

  Mbatia anadai kuwa amefungua kesi hiyo kwa kuwa alichafuliwa kwenye kampeni.

  Rungwe, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, amekuwa akisikika akimshauri Mbatia kuwa kama suala ni kuchafuliwa, basi afungue kesi ya kuchafuliwa jina sio kupinga matokeo ya uchaguzi.

  Pamoja na kushauriwa hivyo, Mbatia anadaiwa kutokubaliana na Rungwe. Wajumbe wanadai kwamba, lengo la Mbatia ni kutaka Chadema wapoteze jimbo hilo kwa CCM. Hivyo, suala hilo limeachwa kubaki kuwa la Mbatia mwenyewe.

  Swali la msingi wanalojiuliza wajumbe wa NEC-NCCR-Mageuzi, ni kwamba kama chama hakitaki kuwafungulia kesi wapinzani, lakini mwenyekiti wake anafanya hivyo, je, anastahili kuendelea kuongoza chama hicho?

  Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao wakidai kuwa ni uthibitisho wao kwamba, Mbatia anatumiwa na CCM, unahusu kumkataza aliyekuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi, Rungwe mwaka jana, kuichafua CCM alipohutubia katika Jimbo la Kawe.

  Rungwe aliwahi kulithibitishia gazeti dada la NIPASHE JUMAPILI, NIPASHE kuwa alipata kumshtaki Mbatia kwenye kikao cha NEC kuhusu kumkataza kufanya hivyo.

  Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao ni kwamba, mwaka 2007, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, baada ya kutangaza orodha ya mafisadi, Mbatia aliibuka na kusema Watanzania wote ni mafisadi, wanatofautiana viwango tu.

  Kauli hiyo inadaiwa kuwa iliashiria kuwa na lengo la kupunguza hasira za umma kwa vigogo wa serikali waliokuwamo kwenye orodha ile.

  Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao wanadai kwamba, wakati wa Bunge la Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/2012, wabunge vijana wa upinzani walionyesha uwezo mkubwa wa kuibana serikali bila aibu.

  CCM wakawa wanalalamika kuwa wabunge hao vijana hawajui kanuni na wanaleta fujo. Mbatia wanadai kuwa alitoa tamko kuunga mkono propaganda za CCM kwa kudai wabunge vijana hawajui kilichowapeleka bungeni kwa kuwa hawana uzoefu.

  Ushahidi mwingine unatolewa na wajumbe hao kuwa Mbatia anatuhumiwa kushawishi wajumbe wa NEC siku zote kuepuka kutoa kauli kali za kupambana na dola kwa madai kuwa yeye anao uzoefu wa namna dola inavyoweza kubomoa chama.

  Wanadai Mbatia anatoa mifano; mmojawapo ukiwa unaomhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwamba alishughulikia NCCR-Mageuzi kutokana na kauli kali.

  Kutokana na hilo, wajumbe wanauliza kama wataogopa kupambana na dola, watakuwaje wapinzani? Mbona Chadema wanapambana na dola na wanafanikiwa?

  Ushahidi mwingine uliowekwa bayana na wajumbe hao, ni kwamba Mbatia anatuhumiwa kujisifu mara zote kwenye vikao vya NEC kuwa yeye huongea na watu wakubwa serikalini na wote wanamhakikishia kuwa NCCR-Mageuzi ndio chama mbadala, kina sifa muhimu za kizalendo.

  Hapa wajumbe wanahoji. Inawezekanaje mtawala unayetaka kumwondoa madarakani akusifie?

  Ushahidi mwingine, ambao umewekwa bayana na wajumbe hao, unaeleza kuwa mwaka 2000 wakati Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutumia kaulimbiu yao ya ‘Ngangari', kilikataa kumtambua Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume kwa kuwa uchaguzi ule ulipingwa hata na Jumuiya ya Kimataifa kwa madai kwamba, haukuwa huru na wa haki.

  Baada ya CUF kuweka bayana msimamo wao huo dhidi ya ushindi wa Karume, wajumbe hao wanadai kuwa Mbatia alitoa tamko kuwa kutomtambua Karume ni uhaini. Akachukua uamuzi wa kwenda kuweka pingamizi kwa wagombea sita Zanzibar na kusababisha umma wa visiwani humo kupiga kura za maruhani.

  Wajumbe hao wanasema mambo yote hayo ni mjadala uliojiri ndani ya kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi, baada ya Mbatia kubanwa sana.

  Mwisho, kwa mujibu wa kanuni za chama, Mbatia amepewa siku 21 kujitetea dhidi ya tuhuma hizo, ndipo NEC ifanye maamuzi ama kumsamehe au kumsimamisha uongozi na kuitisha uchaguzi ndani ya miezi sita. Mamlaka ya NEC kumsimamisha yanatokana na Ibara ya 21 ya Katiba ya chama.

  Machali alipaswa kumsaidia Mbatia kujibu tuhuma hizo ili kumnusuru. Na si kutafuta visingizio (scapegoat)! Anachokifanya Machali ni sawa na kumsitiri Mbatia dhidi ya baridi kwa kumkinga na uzi wa buibui!  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=35369
   
 2. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Lo! Huyu mwandishi Muhibu Said kweli ameingia ' master bedroom' ya chama.
   
 3. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu Mbatia amejimaliza mwenyewe kisiasa na matokeo yake sasa hivi hata akigombea udiwani hawezi kushinda.ni bora aachane na siasa
   
 4. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Nawashukuru sana Wana-NCCR-MAGEUZI kwa kuweka wazi kila kitu. lile wazo la yule mbunge pia lililenga kuleta mtafaruku ndani ya CHADEMA, kwani lililenga kumgombanisha ZITTO na baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema. NCCR, kwa maelezo hayo hapo juu jibu liko wazi kwamba Mbatia si kiongozi safi na hivyo anapaswa kuondoka. Napenda niwape tahadhari mmoja tu; kwamba kwa hizo fact za Mbatia, nyinyi NCCR si wapinzani bali ni wenzetu CCM. Hilo la Mbatia kuwa wetu wala halihitaji hata kuuliza Usalama wa Taifa, kwani hata mchanga wa siasa zetu analijua hilo. Hata sisi tungependa tuone mko imara, kwani mtatusaidia kuwapunguza kasi hawa Chadema.
   
 5. K

  Kigoma 2015 JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Machali hafai kuwa kiongozi kamwe na amshukuru Zitto.
   
 6. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Muhibu Said na Zitto Zubery Kabwe ni tope na maji, hawatenganishiki. Namaanisha hii ni hoja ya kujibu mshambulizi ya Mwanahalisi kwa Zitto. Hadi tufike 2015 tutaona na kusikia mengi.
   
 7. Wateule

  Wateule JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  [​IMG]Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndg. James Mbatia


  Na Muhibu Said

  Novemba 5, mwaka huu, Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya Chama cha NCCR-Mageuzi, ilifanya kikao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili ajenda moja maalum iliyohusu mpasuko ndani ya chama hicho. Ajenda ya kikao hicho ilitajwa na Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samuel Ruhuza, kwenye kikao hicho.


  Ajenda hiyo ilifuatia hatua ya Kamishna wa NCCR-Mageuzi Mkoa wa Tanga, Mbwana Hassan, kwa kushirikiana na Kamishna mwenzake Mkoa wa Arusha, Mzee Sirikwa, kumuomba Mwenyekiti wao, James Mbatia, kutafakari kuhusu uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho.

  Makamishna hao wa NCCR-Mageuzi, walimpa Mbatia sababu moja ya msingi ya ombi lao hilo kwake. Kwamba, wajumbe wengi wa NEC-NCCR-Mageuzi wamepoteza imani naye.

  Inaelezwa kuwa makamishna hao walipowasilisha hoja hiyo kwa Mbatia, aliwauliza walikotoa mawazo hayo, ikiwa ni pamoja na kuwataka wataje majina ya watu waliowatuma kufanya hivyo. Makamishna hao waligoma kutaja majina. Ni katika kikao hicho cha NEC, wajumbe 28 wa halmashauri hiyo walijitokeza hadharani. Hiyo ni baada ya kuthubutu kusaini waraka uliobeba hoja ya makamishna hao ya kutokuwa na imani na Mbatia.


  Hoja hiyo imetoa sababu kuu mbili; ya kwanza ikiwa mwenendo wa Mbatia unaodaiwa kuashiria kuwa anatumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo ni pandikizi (wakala) la CCM ndani ya NCCR-Mageuzi.


  Hali hiyo inadaiwa kusababisha Mbatia kuitwa ‘CCM B’ na hivyo kudhoofisha uenezi wa NCCR-Mageuzi. Sababu ya pili, inatajwa na wajumbe hao wa NEC kuwa inahusu ustaarabu wa kawaida tu. Kwamba, tangu Mbatia awe mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, hajawahi kushinda uchaguzi hata mmoja wa ubunge katika majimbo aliyogombea.


  Baya zaidi, majimbo yote aliyogombea, umma ulikuwa na imani na upinzani. Lakini haukuwa na imani na Mbatia. Na ndio sababu inaelezwa kuwa wakashinda wapinzani wengine na si Mbatia.Majimbo hayo ni pamoja na Vunjo. Huko Mbatia aligombea ubunge mwaka 2000, lakini akaangushwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), Jesse Makundi.


  Jimbo lingine ni la Kawe. Huko Mbatia aligombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, lakini akabwagwa vibaya na Mbunge wa sasa wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee. Hivyo, hoja ya wajumbe hao wa NEC-NCCR-Mageuzi ikawa kuwa huo ni ushahidi kwamba, watu hawamwamini Mbatia kama mpinzani.


  Lakini zaidi kwa kushindwa huko, anapoteza uhalali wa kuwa ‘kamanda’ wa chama taifa. Yaani, hawezi kutangaza mapambano dhidi ya CCM wala hawezi kuthubutu kusema atapambana na chama hicho kilichoota mizizi sehemu kubwa ya nchi ilhali kwenye jimbo tu ameshindwa.

  Lakini pia wajumbe hao wanadai kuwa Mbatia amepoteza hadhi ya kuweza kunadi hata mgombea yeyote wa NCCR-Mageuzi popote ikitokea uchaguzi. Maana hawezi kuuaminisha umma umwamini mgombea anayemnadi ilhali yeye mwenyewe haaminiki anakogombea mara zote.
  Kwenye kikao hicho cha NEC-NCCR-Mageuzi, wajumbe walikwenda mbali zaidi. Mmoja wao kutoka mkoani Ruvuma, Henry Mapunda, alidai kuwa ana ndugu yake ni afisa usalama wa taifa.

  Mapunda alidai ndugu yake huyo aliwahi kumweleza kuwa Mbatia ni mtu wao na kuhoji sababu za watu wa usalama kutamka hivyo?

  Kwa uchache, hicho ndicho kilichojiri katika kikao hicho cha NEC-NCCR-Mageuzi. Mbatia alihudhuria kikao hicho na yote hayo aliyasikia kwa masikio yake. Ambacho kilitarajiwa na wengi, ni kusikia Mbatia amejibu au atajibu nini kuhusu tuhuma zilizoelekezwa kwake na wajumbe hao wa NEC-NCCR-Mageuzi.


  Hiyo ni baada ya yeye mwenyewe (Mbatia) kuomba katika kikao hicho atendewe haki, ikiwa ni pamoja na kupewa nafasi ya kutosha kujibu tuhuma hizo. NEC ilimpa siku 21 kufanya hivyo, kuanzia tarehe ya kikao hicho.

  Lakusikitisha wakati umma wa Watanzania ukisubiri majibu ya Mbatia, Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, kwa mlango wa nyuma, ameibuka na kubadili somo.

  Machali anasema tatizo la NCCR-Mageuzi si Mbatia. Ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. Anadai kwamba, Kafulila, ambaye ni Mkurugenzi wa Uenezi wa NCCR-Mageuzi Taifa, ndiye kinara wa harakati za kumng’oa Mbatia. Anataka uenyekiti wake ili apate fursa nzuri ya kumtengenezea swahiba wake, Zitto njia ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2015 kupitia NCCR-Mageuzi!


  Ni dhahiri kuwa kinachotengenezwa sasa na Machali hapa, ni mkakati wa kutaka kubadili mjadala kutoka kwenye hoja ya msingi iliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi na wajumbe wa halmashauri hiyo ya kutokuwa na imani na Mbatia kama mpinzani.

  Machali anataka mjadala sasa uwe ni vita ya tamaa na uroho wa kutaka uenyekiti wa Mbatia ndani ya NCCR-Mageuzi na kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2015!

  Bahati mbaya mimi kama mtazamaji ni miongoni mwa watu, ambao sikutegemea kama Machali ninayemfahamu angeweza kudiriki kufanya hivyo. Nasema hivyo kwa sababu. Bahati nzuri, Kafulila mara nyingi amesikika akitamka kwamba, hatarijii kugombea uenyekiti na wala hajawahi kutangaza kugombea nafasi hiyo. Amesikika akisema kwamba, waliotangaza kuwa watagombea uenyekiti kwa kuwa wamekosa imani na Mbatia kama mpinzani, ni Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali na aliyekuwa mgombea urais kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Hashim Rungwe.


  Machali anajenga dhana nyingine ya kutaka kumgombanisha Kafulila na Chadema. Kwamba, Kafulila anataka uenyekiti ili kuidhoofisha Chadema.

  Anasahau kwamba, yeye (Machali), Kafulila pamoja na Mkosamali, majimbo ya uchaguzi waliyoshinda mkoani Kigoma, ni yale yaliyokuwa yakiwakilishwa na wabunge kupitia CCM tu. Zaidi ya hivyo, kuna habari kwamba, Kafulila alihakikisha NCCR-Mageuzi haisimamishi mgombea ubunge katika majimbo, ambayo Chadema ina nguvu.


  Ndio sababu NCCR-Mageuzi haikuweka mgombea katika jimbo la Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini. Machali hawezi kuwazuga na kuwapotosha watu wote. Na wala bado hajamsaidia kitu Mbatia. Bali anachokifanya ni kuzidi kumgaragaza Mbatia kwenye matope. Nasema hivyo, kwa sababu. Katika kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi, ushahidi mwiingi ulitolewa na wajumbe wa halmashauri hiyo kuthibitisha hoja yao ya kumkataa Mbatia kuwa mwenyekiti.


  Miongoni mwa sababu hizo, ni pamoja na ile inyoahusu kesi ya matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa naye (Mbatia) katika jimbo la Kawe. Wajumbe wanadai kuwa Mbatia ameigeuza kesi hiyo kuwa ya NCCR-Mageuzi. Si wajumbe hao tu, bali hilo limekuwa likisikika pia likisemwa na Ruhuza. Kwamba, kesi hiyo siyo ya chama. Bali ni suala la mtu binafsi.


  Hiyo inatokana na wajumbe wa NEC-NCCR-Mageuzi kukataa kufungua kesi kwenye jimbo, ambalo aliyeshinda ni mpinzani kwa vile lengo la wapinzani linatakiwa liwe ni kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani katika Bunge. Mbatia anadai kuwa amefungua kesi hiyo kwa kuwa alichafuliwa kwenye kampeni.


  Rungwe, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, amekuwa akisikika akimshauri Mbatia kuwa kama suala ni kuchafuliwa, basi afungue kesi ya kuchafuliwa jina sio kupinga matokeo ya uchaguzi. Pamoja na kushauriwa hivyo, Mbatia anadaiwa kutokubaliana na Rungwe. Wajumbe wanadai kwamba, lengo la Mbatia ni kutaka Chadema wapoteze jimbo hilo kwa CCM. Hivyo, suala hilo limeachwa kubaki kuwa la Mbatia mwenyewe.


  Swali la msingi wanalojiuliza wajumbe wa NEC-NCCR-Mageuzi, ni kwamba kama chama hakitaki kuwafungulia kesi wapinzani, lakini mwenyekiti wake anafanya hivyo, je, anastahili kuendelea kuongoza chama hicho? Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao wakidai kuwa ni uthibitisho wao kwamba, Mbatia anatumiwa na CCM, unahusu kumkataza aliyekuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi, Rungwe mwaka jana, kuichafua CCM alipohutubia katika Jimbo la Kawe.


  Rungwe aliwahi kulithibitishia gazeti dada la NIPASHE JUMAPILI, NIPASHE kuwa alipata kumshtaki Mbatia kwenye kikao cha NEC kuhusu kumkataza kufanya hivyo. Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao ni kwamba, mwaka 2007, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, baada ya kutangaza orodha ya mafisadi, Mbatia aliibuka na kusema Watanzania wote ni mafisadi, wanatofautiana viwango tu.

  Kauli hiyo inadaiwa kuwa iliashiria kuwa na lengo la kupunguza hasira za umma kwa vigogo wa serikali waliokuwamo kwenye orodha ile.
  Ushahidi mwingine unaotolewa na wajumbe hao wanadai kwamba, wakati wa Bunge la Bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/2012, wabunge vijana wa upinzani walionyesha uwezo mkubwa wa kuibana serikali bila aibu.

  CCM wakawa wanalalamika kuwa wabunge hao vijana hawajui kanuni na wanaleta fujo. Mbatia wanadai kuwa alitoa tamko kuunga mkono propaganda za CCM kwa kudai wabunge vijana hawajui kilichowapeleka bungeni kwa kuwa hawana uzoefu. Ushahidi mwingine unatolewa na wajumbe hao kuwa Mbatia anatuhumiwa kushawishi wajumbe wa NEC siku zote kuepuka kutoa kauli kali za kupambana na dola kwa madai kuwa yeye anao uzoefu wa namna dola inavyoweza kubomoa chama.


  Wanadai Mbatia anatoa mifano; mmojawapo ukiwa unaomhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwamba alishughulikia NCCR-Mageuzi kutokana na kauli kali. Kutokana na hilo, wajumbe wanauliza kama wataogopa kupambana na dola, watakuwaje wapinzani? Mbona Chadema wanapambana na dola na wanafanikiwa?


  Ushahidi mwingine uliowekwa bayana na wajumbe hao, ni kwamba Mbatia anatuhumiwa kujisifu mara zote kwenye vikao vya NEC kuwa yeye huongea na watu wakubwa serikalini na wote wanamhakikishia kuwa NCCR-Mageuzi ndio chama mbadala, kina sifa muhimu za kizalendo.

  Hapa wajumbe wanahoji. Inawezekanaje mtawala unayetaka kumwondoa madarakani akusifie?

  Ushahidi mwingine, ambao umewekwa bayana na wajumbe hao, unaeleza kuwa mwaka 2000 wakati Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutumia kaulimbiu yao ya ‘Ngangari’, kilikataa kumtambua Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amani Abeid Karume kwa kuwa uchaguzi ule ulipingwa hata na Jumuiya ya Kimataifa kwa madai kwamba, haukuwa huru na wa haki. Baada ya CUF kuweka bayana msimamo wao huo dhidi ya ushindi wa Karume, wajumbe hao wanadai kuwa Mbatia alitoa tamko kuwa kutomtambua Karume ni uhaini. Akachukua uamuzi wa kwenda kuweka pingamizi kwa wagombea sita Zanzibar na kusababisha umma wa visiwani humo kupiga kura za maruhani.


  Wajumbe hao wanasema mambo yote hayo ni mjadala uliojiri ndani ya kikao cha NEC-NCCR-Mageuzi, baada ya Mbatia kubanwa sana.

  Mwisho, kwa mujibu wa kanuni za chama, Mbatia amepewa siku 21 kujitetea dhidi ya tuhuma hizo, ndipo NEC ifanye maamuzi ama kumsamehe au kumsimamisha uongozi na kuitisha uchaguzi ndani ya miezi sita. Mamlaka ya NEC kumsimamisha yanatokana na Ibara ya 21 ya Katiba ya chama.

  Machali alipaswa kumsaidia Mbatia kujibu tuhuma hizo ili kumnusuru. Na si kutafuta visingizio (scapegoat)! Anachokifanya Machali ni sawa na kumsitiri Mbatia dhidi ya baridi kwa kumkinga na uzi wa buibui!

  Chanzo: Nipashe
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dirty people in a dirty game
   
 9. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Wataichoma itatoa harufu tu wote tutasikia.
   
 10. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  KAAAZI KWELI KWELI! na hii je?
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]NCCR refutes reports of ultimatum to Mbatia [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 13 November 2011 22:33 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]digg

  By Frank Aman
  The Citizen Correspondent
  Dar es Salaam. The NCCR-Mageuzi has refuted reports that its national chairman, Mr James Mbatia, was given 21 days by the party's National Executive Council to defend himself against mismanagement allegations.

  Recent media reports said that some NCCR-Mageuzxi NEC members had accused their chairman of poor leadership and asked him to step down.The reports indicated that Mr Mbatia defended himself during the meeting, but he was given 21 days to come up with convincing reasons why he should retain his post.

  But the opposition party secretary general, Mr Samuel Ruhuza, said yesterday that the meeting held on November 5, this year did not discuss what is termed as allegations against Mr Mbatia.

  Addressing a press conference at party headquarters in Dar es Salaam, Mr Ruhuza also refuted reports that the party draws Sh130-million subsidy each month."These reports are not true and it's obvious that such information aims at tarnishing our party image.

  Treasury is usually giving the subsidy through the office of the Registrar of Political Parties. And if anyone wants to know the amount should ask the Registrar instead of speculating," he added.

  Mr Ruhuza said those who are blaming Mr Mbaria for losing the Kawe parliamentary seat race should take note that he has filed a case against the results, in which Halima Mdee (Chadema) won the seat.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  NA HUKU!! MWANANCHI
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]NCCR yahaha kuzima uasi kwa James Mbatia [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 13 November 2011 21:08 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Aidan Mhando
  CHAMA cha NCCR- Mageuzi kimetoa tamko rasmi kikisema hakuna mpango wowote wa kichama wenye lengo la kumuondoa madarakani mwenyekiti wake James Mbatia.Tamko hilo rasmi la NCCR limekuja siku chache baada ya kuibuka kundi la baadhi ya wanachama lililoelezwa kuwa na lengo la kufanya mapinduzi dhidi ya Mbatia kabla ya muda wake kikatiba kumalizika.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza alisema kuwa katika siku za hivi karibuni kumeibuka taarifa mbali mbali za uzushi zinazoeleza kwamba ndani ya NCCR kuna baadhi ya watu wanaotaka kumng'oa mwenyekiti wa chama hicho.

  Genge linalotaka kumpindua Mbatia linatajwa kuongozwa na wabunge wawili wa chama hicho, ambao wanatoa hoja mbalimbali ikiwemo rekodi ya matokeo mabovu ya mwenyekiti huyo ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu katika majimbo ya Kawe na Vunjo, hivyo kukosa nguvu, ushawishi na uhalali wa kuongoza chama taifa.

  Wasukaji hao wa mpango wa mapinduzi dhidi ya Mbatia wanatajwa kufanikisha ajenda hiyo katika kikao cha Nec ya chama hicho wiki iliyopita, ambapo wajumbe 28 walijiorodhesha na kujipanga kuweka vema mpango mkakati huo wa kujiuzulu kwa Mbatia au kusimamishwa.

  Lakini, Ruhuza jana alisema kuwa Mbatia ni kiongozi halali aliyewekwa madarakani na wanachama wa chama hicho kupitia Katiba ya NCCR na kwamba, hakuna yoyote anayeweza kumtoa katika nafasi hiyo kwa sababu chama kinaongozwa na katiba.

  "Kumeibuka taarifa ambazo zinadai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa NCCR, wana mpango wa kutaka kumng'oa madarakani mwenyekiti. Lakini ukweli ni kwamba, hakuna kitu kama hicho na taarifa zinazosambazwa na watu hao zina lengo la kukichafua chama chetu," alisema Ruhuza.

  Ruhuza alifafanua kwamba, Novemba tano mwaka huu NCCR ilifanya kikao cha ndani kujadili mambo muhimu ya chama huku moja ya ajenda ikiwa ni kuangalia muelekeo wa chama baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na hali ilivyo kwa sasa.

  "Tulifanya Kikao cha ndani, kilikuwa ni maalumu kwa kuangalia mwenendo wa chama chetu baada ya uchaguzi, lakini tunashangazwa na kitendo cha baadhi ya watu kusambaza taarifa za uzushi zinazodai kikao hicho kilikuwa na ajenda ya kutaka kumuondoa madarakani mwenyekiti wetu," alisema Ruhuza.
  Kesi ya Mdee


  Akizungumzia kesi ilopo mahakamni kati ya Mbunge wa Jimbo la Kawe na Mbatia, Ruhuza alisema NCCR ndiyo imemtuma mwenyekiti huyo kumfungulia kesi mbunge wa jimbo hilo baada ya kuona maneno yaliotolewa dhidi ya Mbatia yanagusa hata chama.

  "Kesi iliyopo mahakamani ni kesi ambayo chama cha NCCR kimemtuma Mbatia kuifungua baada ya kuona maneno yanatolewa na Mdee dhidi ya Mwenyekiti wetu wa chama yanagusa chama chetu,"alisema.

  Ruhuza alibainisha kwamba Mbunge wa Jimbo la Kawe anamtuhumu Mwenyekiti Mbatia kwamba ni kibaraka wa CCM hali ambayo imetugusa na kuamua kumtuma Mbatia kufungua kesi mahakamani dhidi ya mbunge huyo.

  "Mwenyekiti wetu anaambiwa ni kibaraka wa CCM, huku akiwa analipwa fedha ili kukibomoa chama madai ambayo tuna kesi ambayo ipo mahakamani," Alisema.

  Ruzuku
  Kuhusu ruzuku Ruhuza aliwataka watu wanaotaka kufahamu chama kinapata ruzuku kiasi gani waende kwa msajili wa vyama, ili kufahamu ukweli na siyo kuhoji kwa watu wasiohusika na mambo ya NCCR.

  "Kuna madai yanayoeleza kwamba chama kinapata ruzuku ya Sh130 milioni jambo ambalo sio la kweli na linasabaisha chama kukosa misaada kutoka kwa wafadhili. Sasa tunaomba mtu yoyote anayetaka kufahamu kuhusu ruzuku ya chama aende kwa msajili wa vyama," alisema.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 12. z

  zakazaka Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbatia ni kiongozi imara yote yaliyoandikwa na muhibu ni uongo mtupu hakuna ukweli hata chembe, kesi ya mbatia imemng'ang'ania mdee, nampongeza mbatia kwa kusimamia sheria za uchaguzi bila kujali wanaovunja ni wapinzani au wa chama tawala.
   
 13. G

  Godfrey GODI Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapungufu yote ya Mbatia, yaliyoainishwa, yanalegebishika, lakini wanaoona Mbatia hawezi kujirekebisha ni wale wenye hidden agenda. Siamini kama Machali anaweza kuropoka bila kujua undani wa jambo hili. Time will tell
   
 14. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Sure! Mkuu hapo umenena, kinachoonekana hapa ni ajenda ya kuutaka uenyekiti tu...
  Hata kama Mbatia ana mapungufu ambayo hata mimi nayaona lakini si kwa kiwango
  hiki kinachoelezwa na hawa jamaa...
   
 15. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Na huyo Sam Ruhuza yeye kama mtendaji mkuu wa chama amefanya nini kuhakikisha chama chake kinarejesha makali ya zamani tangu aukwae ukatibu mkuu?Mi namuona yupo kisoka zaidi siasa wala haimo ndani yake...!
   
 16. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,473
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180

  Acheni kutetea ujinga, Mbatia ajitokeze atwambie ukweli katumwa na nani kufungua kesi ya kupinga matokeo ya Mdee! Haiwezekani mtu aliyekua wa tatu afungue kesi ya kupinga matokeo kama hajatumwa na mtu yeyote. Kafulila ana mapungufu yake lakini hayahalalishi ukibaraka wa mbatia wa wazi wazi wa kutaka kubatilisha matokeo halali ya mpambanaji wetu.
   
 17. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  ukome uzushi wako, sisi sio wenzenu!
   
Loading...