Mbunge Luhaga Mpina achangia maoni bajeti ya Wizara ya Afya

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
View attachment LUHAGA MPINA WIZARA YA AFYA_2022.pdf

---
MCHANGO WA MAANDISHI WA MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) MBUNGE WA JIMBO LA KISESA (CCM) AKICHANGIA KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 BUNGENI DODOMA TAREHE 16 MEI 2022

Mheshimiwa Spika, Kutokana na changamoto ya muda pamoja na kuchangia kwa kuzungumza hapa bungeni lakini pia nitawasilisha mchango wangu kwa maandishi.

1:1 Pongezi na Shukrani kwa Wizara ya Afya

Mheshimiwa Spika,
Wizara ya Afya inafanya kazi nzuri sana na ni ya kupongezwa, nitoe pongezi nyingi kwa Mhe. Waziri na watendaji wote wa Wizara, Madaktari na Wauguzi wote wa Serikali na sekta binafsi kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kazi kubwa mnayoifanya ya tiba na kutoa nafasi ya pili ya maisha ya watu (you are providing a second chance of life).

Mheshimiwa Spika, Kama Taifa tumepiga hatua kubwa ya utoaji wa huduma za afya nchini, idadi ya madaktari na wauguzi wabobezi, madaktari bingwa na madaktari bingwa wa ubingwa imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kuwepo kwa vifaa vya kisasa kama MRI, CT- Scan, OGD, X-ray, Ultral Sound nk, kuwezesha kuimarisha matibabu ya kibingwa nchini hususan kwa magonjwa ya moyo, masikio, figo, mifupa, ubongo na kansa nk. Pia ujenzi wa miundombinu katika maeneo ya kutolea huduma za afya kama zahanati, vituo vya afya na hospitali unaoendelea kote nchini.

Mheshimiwa Spika, Aidha kampeni ya usambazaji maji safi nchini kote inayofanywa na Wizara ya Maji imeimarisha huduma za afya 2 nchini kwa kiwango kikubwa na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha afya za watanzania.

Mheshimiwa Spika, Kufikia mwaka 2020, rufaa za kwenda nje ya nchi zilipungua kufikia 95% na wagonjwa kutoka mataifa jirani wameanza kuja kutibiwa hapa nchini hususani magonjwa ya Moyo na Figo.

1.2 Changamoto za utoaji wa huduma za afya nchini Mheshimiwa Spika, Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali bado kuna changamoto nyingi zinazokwamisha utoaji huduma za afya nchini na hapa nitazungumzia baadhi ya changamoto chache kama ifuatavyo:-

1.2.1 Ukosefu wa huduma za afya ya msingi nchini Mheshimiwa Spika, Hivi sasa hapa nchini ni takriban vijiji 6,190 havina Zahanati hali inayopelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi kupata huduma ya afya ya msingi kwa kila Kijiji kama tunavyofahamu magonjwa hayana likizo wala wikiendi na kwamba akina mama wajawazito, watoto na wagonjwa wengine wanahitaji kupata huduma za afya zilizokaribu nao. Umuhimu wa Zahanati unathibitishwa na Hotuba ya Waziri wa Afya ambapo kuishia Machi 2022 asilimia 50 ya wagonjwa waliohudhuria katika vituo vya kutolea huduma za afya walikwenda kwenye Zahanati. Zipo changamoto nyingi zinazokwamisha kupatikana kwa huduma ya afya kwa kila Kijiji kama ifuatavyo:-

(i) Huduma za afya vijijini kusubiri mpaka miundombinu ya Zahanati ikamilike yaani OPD, nyumba za watumishi nk. ndio Zahanati ifunguliwe, hivi sasa katika vijiji husika wananchi wanahitaji huduma 3 ya afya kwa maana ya Daktari, Wauguzi, Dawa na vifaa tiba muhimu hata kama ni kwenye nyumba ya kupanga wakati ukamilishaji wa miundombinu ukiendelea.

(ii) Kuchelewa kufunguliwa kwa Zahanati ambazo ujenzi wa miundombinu muhimu ulishakamilika, kumekuwa na ucheleweshaji wa kuanza kutoa huduma bila sababu za msingi hadi majengo yanachakaa na wananchi kukatishwa tamaa, majengo yapo hakuna huduma, ujenzi wa OPD, vyoo, kichomea taka (Incinerator) na shimo la kondo la nyuma (Placenta Pit) umekamilika lakini wananchi wanaambiwa mpaka iwepo nyumba ya watumishi ndio Zahanati ifunguliwe, sehemu zingine miundombinu yote imekamilika Zahanati haifunguliwi.

(iii) Ucheleweshaji wa ukamilishaji wa maboma ya Zahanati, wananchi wamekuwa wakiibua na kuanza ujenzi wa miradi ya Zahanati kwa shangwe na hamasa kubwa na kujenga kufikia hatua hanamu kama maelekezo na mwongozo wa wizara unavyosema lakini inachukua miaka mingi kukamilisha maboma hayo hali inayowakatisha tamaa wananchi na kuchelewesha huduma stahiki. Mwaka 2021/2022 kupitia TAMISEMI zilitengwa fedha za kukamilisha zahanati 564 na Mwaka 2022/2023 zimetengwa fedha za kukamilisha Zahanati 300 tu hii kasi ni ndogo kulingana na uhitaji katika Taifa. Serikali inashauriwa kutenga fedha za kutosha ili kuendana na uhitaji.

(iv) Upungufu wa watumishi wa kada ya Afya ngazi ya Zahanati, tatizo ambalo halijapata suluhu kwa muda mrefu na wananchi wakiendelea kukosa huduma hitajika katika vijiji. Serikali ilipaswa kuweka utaratibu mzuri wa ajira na kutumia njia mbadala ya kuingia 4 mkataba na vijana waliohitimu mafunzo mbalimbali ya Afya ambao hawaja ajiriwa ili kusaidia utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, Kwenye Jimbo langu la Kisesa nina Zahanati 10 zilizokamilika muda mrefu lakini huduma hazitolewi, Mfano Zahanati ya Kijiji cha Semu, Mwandu Kisesa, Makomangwa, Mwageni, Mwagayi, Isangijo, Ikigijo, Mwakisandu, Malwilo na Tindabuligi, lakini pia tuna maboma ya muda mrefu 10 ya Kijiji cha Inonelwa, Mwamhongo, Nzanza, Matale, Masanga, Mwakipugila, Ntobo, Ng’hanga, Mwakasumbi na Lubiga.

Mheshimiwa Spika, Hotuba ya Waziri wa TAMISEMI ilitueleza kuwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 30.15 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati na ununuzi wa vifaa tiba kwa Zahanati mpya ni matumaini yangu kuwa Wizara ya Afya na TAMISEMI wanaenda kufungua Zahanati zangu 10 zilizokamilika na kumalizia maboma 10 ya Zahanati yaliyopo katika Jimbo la Kisesa. Hata hivyo niipongeze sana Serikali kwa kutoa fedha Shilingi Milioni 500 kujenga Kituo cha Afya Mwasengela ambacho kitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo.

1.2.2 Kuharibika na kutelekezwa kwa vifaa Tiba na mashine za uchunguzi wa Magonjwa

Mheshimiwa Spika,
Katika ziara ya kustukiza aliyoifanya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Tarehe 11 Mei 2022 alibaini kuwa katika Taasisi ya MOI Mashine za CT-Scan na MRI zimeharibika kutokana na kukatikakatika kwa umeme na hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, Uharibifu wa Mashine za CT-Scan na MRI katika Taasisi ya MOI ni kielelezo cha uharibifu mkubwa na 5 kutelekezwa kwa Vifaa Tiba mbalimbali katika maeneo ya kutolea huduma za Afya kote Nchini, Vifaa Tiba vilivyonunuliwa kwa gharama kubwa kutokana na kodi za watanzania leo vimetelekezwa na havitoi huduma.

Mheshimiwa Spika, Hiki ni kilio kikubwa sana kwa wananchi kwa kukosa huduma muhimu na wengine kulazimika kutafuta rufaa nje ya Nchi na Hospitali binafsi ambazo gharama zake ni kubwa na wengi kushindwa kuzimudu. Mfano gharama za kipimo cha MRI Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni Tsh 210,000 wakati Hospitali za binafsi inaanzia Tsh 500,000 na kwa kipimo cha CT-Scan Muhimbili ni Tsh 150,00 na Hospitali binafsi inaanzia Tsh 350,000.

Mheshimiwa Spika, Maswali ya kujiuliza kwanini turuhusu umeme ukatikekatike mpaka kwenye maeneo muhimu kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na maeneo mengine ya kutolea huduma za Afya, inawezekanaje Mashine muhimu kama hizo zifungwe bila kuwepo Back-up System? na kwanini Vifaa Tiba hivyo muhimu vikae kwa muda mrefu bila matengenezo? Ni muhimu tutafakari upya umadhubuti wa mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa Vifaa Tiba katika maeneo mbalimbali Nchini, kubaini na kudhibiti njama zinazoweza kufanywa na baadhi ya watumishi wasio waadilifu kuhujumu Vifaa Tiba vya umma kwa maslahi binafsi.

1.2.3 Uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji

Mheshimiwa Spika,
Ni muhimu sana kuchukua hatua za kuzuia kuenea kwa magonjwa badala ya kusubiri tiba, afya bora inategemea kwa kiwango kikubwa usafi wa mazingira na kuzuia uchafuzi wa vyanzo vya maji. Eneo hili lisiposimamiwa na kudhibitiwa vizuri afya za watanzania zitaendelea kuwa mashakani. 6 Baadhi ya sababu zinazosababisha uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji kuendelea kushamiri ni kama ifuatavyo:-

(a) Uwekezaji mdogo katika mifumo ya kutibu, kuhifadhi na kuondosha maji taka, Fedha zinazotengwa katika eneo hili ni ndogo na uwezo wa Wizara ya Maji kuondosha maji taka ni 13.5% tu kwa sasa hali inayopelekea baadhi ya watu, mahoteli, viwanda na migodi kumwaga na kutiririsha hovyo majitaka yasiyotibiwa na kupelekea uchafuzi mkubwa wa mazingira na vyanzo vya maji. Hali ambayo inasababisha kuenea kwa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza kwa binadamu ikiwemo Saratani. Mwenendo wa utengaji fedha katika eneo la miundombinu ya maji taka haileti matumaini na wala haioneshi kama tuna nia ya dhati kuondoa tatizo hili ambalo linatugharimu kwa kiasi kikubwa, ni muhimu sana Serikali kutenga fedha za kutosha kujenga mifumo ya miundombinu ya majitaka kila maeneo yenye uhitaji, kusisitiza na kujenga vyoo vya kisasa hususani katika taasisi zenye watu watu wengi kama shule, kuhakikisha kuwa viwanda vyote vina mifumo ya kutibu maji taka (ETP) na migodi kuweka mifumo mizuri ya kuhifadhi majitaka (TSF).

(b) Usimamizi dhaifu wa Sheria ikiwemo Sheria ya Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004 na kampeni za kitaifa za usafi wa mazingira ambazo zimewekwa kisheria.

(i) Kampeni za usafi wa mazingira zimefifia na hazisimamiwi kikamilifu hali iliyopelekea kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji maeneo mbalimbali nchini. Licha ya kampeni hizi kuwepo kisheria na zinasimamiwa chini ya mwongozo wa usafi wa 7 mazingira wa Mwaka 2016, Environmental Management (Designation of National Cleanliness Day) Gudelines 2016.

(ii) Kutochukua hatua madhubuti kwa watu, viwanda na migodi inayochafua mazingira, Serikali imekuwa ikichelewa kuchukua hatua kwa wachafuzi wa mazingira na hata hatua zinapochukuliwa haziendani na athari zilizojitokeza, hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji kuwa mkubwa na kuendelea kuleta madhara makubwa ya kiafya kwa wananchi.

Mfano wa hivi karibuni ambapo Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) liliupiga faini ya shilingi bilioni 1, Mgodi wa Barrick North Mara baada ya kutiririsha maji taka yenye kemikali kutoka kwenye mabwawa (Tailings Storage Facilicy-TSF) kwa zaidi ya saa 4 kwenda kwenye mazingira na makazi ya watu na kufanya uharibifu mkubwa wa mazingira na kuhatarisha maisha ya watu, mifugo na viumbe hai vingine, kinyume cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004.

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Mazingira na Waziri wa Afya wamechelewa kuchukua hatua na kwamba adhabu iliyotolewa ni faini peke yake, wakati kwa mujibu wa sheria ilipaswa kufanyika tathmini ya kina ya athari za mazingira zilizosababishwa na uchafuzi huo, Mgodi wa Barrick North Mara ulitakiwa kuyasafisha mazingira waliyoyachafua kwa gharama zao na pia ili kuzuia hali hii kutokujirudia mgodi ulitakiwa kufungwa kwa muda kupisha ukarabati wa mabwawa na miundombinu ya majitaka yenye kemikali (TSF).

Mheshimiwa Spika, Hapa yako maswali mengi ya kujiuliza kwanini mgodi uliamua kutiririsha maji yenye kemikali kinyume cha sheria na 8 kwanini mamlaka husika zimeshindwa kuchukua hatua stahiki, Kwanini mgodi wa Barrick North Mara unakingiwa kifua kiwango hicho huku wananchi wetu wakiathirika kiafya.

1.2.4 Utegemezi wa Dawa na Vifaa Tiba kutoka Nje ya Nchi

Mheshimiwa Spika,
Utegemezi wa Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba kutoka Nje ya Nchi unasababisha ugumu wa upatikanaji, gharama kubwa na ucheleweshaji wa bidhaa za afya kuwafikia wagonjwa.

Mheshimiwa Spika, Tanzania inatumia fedha nyingi za kigeni kuagiza dawa, vifaa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi kwa kuwa viwanda vya vya ndani vinatosheleza kwa 11% tu ya mahitaji ya nchi, sehemu inayobaki tunategemea kutoka nje ya nchi, wakati wenzetu nchi jirani ya Kenya wanajitosheleza soko la ndani kwa 30% na wanaongoza kuuza nje ya nchi katika ukanda wa nchi za EAC na COMESA na pia ni nchi ya tatu Afrika kwa kuuza dawa na vifaa tiba nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Viwanda vya ndani vya kuzalisha bidhaa za afya tunavihujumu sisi wenyewe na hakuna utashi wa kweli wa kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo, mfano ujenzi wa kiwanda cha vifaa tiba Simiyu licha ya uwepo wa fedha na mwekezaji lakini leo ni zaidi ya miaka mitatu kibali cha ujenzi wa kiwanda hicho hakijatolewa na Serikali. Na kwa upande mwingine viwanda vilivyopo vimewekewa kodi katika vifungashio, vitendanishi na malighafi pamoja na vipuri vya mashine hali inayopelekea kuzalisha bidhaa za afya kwa gharama kubwa na kushindwa kushindana na bidhaa za afya kutoka nje ya nchi, wakati huo bidhaa za afya zote kutoka nje ya nchi zimesamehewa kodi na Serikali.

1.2.5 Changamoto ya Sheria ya Manunuzi katika upatikanaji wa Dawa.

Mheshimiwa Spika,
Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa kipindi kirefu na kwa namna yalivyo majukumu yake imekuwa ikikwazwa na Sheria ya manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 na kanuni zake za Mwaka 2013 (na marekebisho yake ya Mwaka 2016) hali inayopelekea ucheleweshaji wa upatikanaji wa dawa, gharama kubwa na kufanikisha njama za wizi katika mfumo wa manunuzi ya bidhaa za afya, baadhi ya vikwazo hivyo vya kisheria ni kama ifuatavyo:-

(i) Sheria inataka itumike njia ya ushindani kwenye manunuzi, njia hii ya ushindani hutumia muda mrefu sana kukamilisha hatua za manunuzi, baadhi ya kampuni zinazoshiriki zabuni zinamilikiwa na mtu mmoja au zina mahusiano na mtu mmoja na hivyo kutengeneza mazingira ya kupanga bei (Bid Rigging) na kupunguza ushindani wa kweli.

(ii) Sheria inataka kutoa zabuni kwa mzabuni mwenye bei nafuu kuliko wengine hata kama bei hiyo ni kubwa kuliko bei ya soko, kigezo hiki kimekuwa kikipelekea MSD kununua bidhaa za afya kwa bei kubwa ikilinganishwa na thamani halisi ya fedha (Value for Money) na pengine hulazimika kurudia kutangaza zabuni mara kwa mara.

(iii) Sheria ya Manunuzi kulazimisha wajumbe wa bodi ya zabuni kufanya maamuzi ya kila aina ya zabuni huku uteuzi wao ni wa majina ambao hauruhusu uwakilishi na ni watumishi wa umma ambao wana majukumu mengine hivyo kupelekea vikao vya bodi 10 kuahirishwa mara kwa mara kutokana na kukosekana kwa akidi na kuchelewesha manunuzi ya dawa.

Mheshimiwa Spika, MSD na wadau wengine wameshalalamikia kwa muda mrefu vipengele hivyo vya kisheria bila mafanikio, kutokana na unyeti na aina ya manunuzi yanayofanywa na MSD ni nini kilichotufanya tushindwe kuutizama upya mfumo wa manunuzi wa MSD kwa kina na kufanya marekebisho ya kisheria yatakayoleta tija kwa manufaa ya umma. Kinachofanyika hivi sasa ni kupeleka adhabu na kuiwajibisha taasisi ya MSD kwa kasoro ambazo tayari walishazitolea taarifa kwa muda mrefu.

1.2.6 Ukosefu wa mtaji wa MSD

Mheshimiwa Spika
, Licha ya umuhimu na unyeti wa Taasisi ya MSD katika utoaji wa huduma za afya nchini, Serikali haijaipa mtaji wa kutosha kutekeleza majukumu yake ambapo MSD ilishawasilisha maombi ya Tsh. Bilioni 420 kwa muda mrefu bila utekelezaji na mbaya zaidi, Serikali imelimbikiza madeni ya Tsh. Bilioni 256. 92 na kuifanya taasisi hiyo kukosa uwezo wa kutimiza wajibu wake wa msingi wa kununua na kusambaza bidhaa za afya nchini. Wakati wenzetu wa Kenya wakiwekeza 8% ya pato la taifa katika afya sisi tunatenga fedha kidogo katika sekta ya afya huku tukifanya hujuma kwa taasisi kama MSD na kuvuruga utoaji wa huduma za afya nchini.

Mheshimiwa Spika, Katika hotuba ya Waziri anakiri kuwa MSD imeweza kusambaza aina 290 za dawa, Vifaa Tiba na vitendanishi muhimu kwa 51% tu bila kueleza nini kilichopelekea taasisi hiyo kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa 100%.

1.2.7 Wizi wa Dawa na Vifaa Tiba

Mheshimiwa Spika,
Novemba 2021, Serikali ilifanya tathmini ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu na kutoa taarifa ya ufuatiliaji wa bidhaa za Afya kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya Nchini na kubainisha mtandao mzima wa ‘Wizi’ wa dawa na vifaa tiba. Ripoti hiyo inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za uagizaji wa dawa, ununuzi, upokeaji, usambazaji na utumiaji wa dawa ikiwemo bidhaa za afya kukosa ushahidi wa kufika kwa wagonjwa kwenye vitengo vya kutolea huduma. Jumla ya ukiukwaji huo unafikia kiasi cha Tsh. Bilioni 83 katika mawanda ya Hospitali 28 za rufaa za mikoa na Hospitali/ vituo vya afya 183 katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG ya kuishia 30 Juni 2021 inaonyesha kuwa madai yanayokataliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yamekuwa yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 2.18 Juni 2020 hadi kufikia Tsh. Bilioni 3.18 Juni 2021. Hali hii inaonyesha kuna udanganyifu mkubwa katika huduma ya bima inayotolewa na NHIF kwa wanachama wake.

Mheshimiwa Spika, Jambo la kusikitisha licha ya taarifa hizo zinazoonyesha ukiukwaji mkubwa sheria, kanuni na taratibu za uagizaji, uzalishaji, usambazaji na utumiaji wa dawa na vifaa tiba hapa nchini lakini huoni hatua madhubuti ambazo zimechukuliwa na Serikali. Naomba kuonyesha maeneo machache kama ifuatavyo:-

(a) Wizara ya Afya imekuwa haifanyi ukaguzi na ufuatiliaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ambapo matokeo yake dawa zinapotea kabla ya kuwafikia wagonjwa na kupelekea ukosefu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma nchini, Aidha wizara haijajiimarisha kimuundo na kimfumo kutekeleza jukumu hili ikiwemo kuwepo kwa taasisi imara ya ukaguzi wa ndani ambayo ni mtambuka na ushirikishwaji wa wazi uliojumuishi wa wadau.

(b) Uchukuaji dhaifu wa hatua kwa wezi wa dawa na vifaa tiba pale wanapobainika kutokana na kaguzi na tathmini, mfano tathimini ya kwanza iliyofanywa na aliyekuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Dorothy Onesphoro Gwajima Novemba 2021 hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahalifu waliobanishwa katika tathmini hiyo. Leo tena tunapitisha bajeti ili tuwapelekee hao hao waliotuibia dawa, hivi tatizo ni nini na kwanini huu wizi tunaulea. Kitendo cha kutochukua hatua kina halalisha wizi wa dawa kuendelea nchini.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na taarifa za CAG na eneo dogo lililofanyiwa tathmini na Waziri wa Afya limeonyesha ukiukwaji mkubwa wa sheria, najiuliza je usalama wa dawa na vifaa tiba uko wapi? Mkakati gani uliowekwa na Serikali kudhibiti hali hiyo, Je fedha tunazoidhinisha leo kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba hazitaenda kuibiwa? Kama taarifa za uchunguzi na ukaguzi zimekuwa zikibaini wezi na mtandao wao ni nini kinachosabisha kigugumizi kwa Serikali kuwachukulia hatua wahusika wa wizi huo na kuutokomeza kabisa mtandao huo haramu.

Nawasilisha,
Luhaga Joelson Mpina
Mbunge wa Jimbo la Kisesa (CCM)​
 
View attachment 2227715

ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom