BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,007
Huyu Mbunge Lugola kwa kweli ni mbunge ambaye anastahili pongezi kwa kuweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania badala ya yale ya chama chake. Kwa miaka mingi amekuwa anaikosoa Serikali kwenye mambo mengi sana. Naomba Mungu hili tishio lake safari hii akishirikiana na Wabunge wengine la kukwamisha bajeti ya Serikali liwe kweli pamoja na kuwa MACCM wanaweza kumfukuza Ubunge kwa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alilithibitishia gazeti hili jana kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge waliopanga kukwamisha bajeti hiyo na yuko tayari kufukuzwa ubunge kwa hilo.
Lugola alisema kuwa pamoja na kuwepo kanuni inayowakataza wabunge wa CCM kukwamisha bajeti na anayefanya hivyo hufukuzwa, yuko tayari afukuzwe ili ayaponye maisha ya Watanzania milioni 45.
"Kila mwaka tunapiga kelele misamaha ya kodi, wanatumia mwanya huo vibaya na matokeo yake bajeti za Serikali mwaka hadi mwaka hazipati fedha kutoka Hazina," alisema Lugola na kuongeza:
"Kama hakuna fedha, halafu tunatoa misamaha kiholela, basi ni afadhali bajeti ya mwaka huu tuzibe hiyo mianya, futa kabisa hiyo misamaha isiyo na tija."
Lugola alisisitiza: "Hatuwezi kuendesha nchi kwa staili hiyo, lazima tufike mahali mambo ya kuwekeana kanuni kuwa tukikwamisha bajeti Bunge litavunjwa, acha livunjwe ili kuliponya taifa."
Lugola alisema kama Serikali haitakuja na mwarobaini wa misamaha ya kodi, ukwepaji wa kodi, matumizi makubwa ya Serikali na kupambana na ufisadi na wizi, bungeni hapatatosha.
Bofya hapa chini kwa habari zaidi.
Bajeti Kuu hatihati - Kitaifa - mwananchi.co.tz