Mbunge Lugola aichachafya Serikali Bungeni

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Huyu Mbunge Lugola kwa kweli ni mbunge ambaye anastahili pongezi kwa kuweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania badala ya yale ya chama chake. Kwa miaka mingi amekuwa anaikosoa Serikali kwenye mambo mengi sana. Naomba Mungu hili tishio lake safari hii akishirikiana na Wabunge wengine la kukwamisha bajeti ya Serikali liwe kweli pamoja na kuwa MACCM wanaweza kumfukuza Ubunge kwa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alilithibitishia gazeti hili jana kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge waliopanga kukwamisha bajeti hiyo na yuko tayari kufukuzwa ubunge kwa hilo.

Lugola alisema kuwa pamoja na kuwepo kanuni inayowakataza wabunge wa CCM kukwamisha bajeti na anayefanya hivyo hufukuzwa, yuko tayari afukuzwe ili ayaponye maisha ya Watanzania milioni 45.

"Kila mwaka tunapiga kelele misamaha ya kodi, wanatumia mwanya huo vibaya na matokeo yake bajeti za Serikali mwaka hadi mwaka hazipati fedha kutoka Hazina," alisema Lugola na kuongeza:

"Kama hakuna fedha, halafu tunatoa misamaha kiholela, basi ni afadhali bajeti ya mwaka huu tuzibe hiyo mianya, futa kabisa hiyo misamaha isiyo na tija."

Lugola alisisitiza: "Hatuwezi kuendesha nchi kwa staili hiyo, lazima tufike mahali mambo ya kuwekeana kanuni kuwa tukikwamisha bajeti Bunge litavunjwa, acha livunjwe ili kuliponya taifa."

Lugola alisema kama Serikali haitakuja na mwarobaini wa misamaha ya kodi, ukwepaji wa kodi, matumizi makubwa ya Serikali na kupambana na ufisadi na wizi, bungeni hapatatosha.

Bofya hapa chini kwa habari zaidi.

Bajeti Kuu hatihati - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Timu lugola viva!
Timu filikunjombe viva!
Timu mpina viva!
Timu lembeli viva!
 
Lugola tunamsubiri UKAWA kwa ham kubwa sana tumpe majukumu yake 2015. mgombea atakuwa 1 tu ana hiyari kujiunga na CUF, CDM ama NCCR Mageuzi.
 
Huyu Mbunge Lugola kwa kweli ni mbunge ambaye anastahili pongezi kwa kuweka mbele maslahi ya Tanzania na Watanzania badala ya yale ya chama chake. Kwa miaka mingi amekuwa anaikosoa Serikali kwenye mambo mengi sana. Naomba Mungu hili tishio lake safari hii akishirikiana na Wabunge wengine la kukwamisha bajeti ya Serikali liwe kweli pamoja na kuwa MACCM wanaweza kumfukuza Ubunge kwa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~

Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alilithibitishia gazeti hili jana kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge waliopanga kukwamisha bajeti hiyo na yuko tayari kufukuzwa ubunge kwa hilo.

Lugola alisema kuwa pamoja na kuwepo kanuni inayowakataza wabunge wa CCM kukwamisha bajeti na anayefanya hivyo hufukuzwa, yuko tayari afukuzwe ili ayaponye maisha ya Watanzania milioni 45.

"Kila mwaka tunapiga kelele misamaha ya kodi, wanatumia mwanya huo vibaya na matokeo yake bajeti za Serikali mwaka hadi mwaka hazipati fedha kutoka Hazina," alisema Lugola na kuongeza:

"Kama hakuna fedha, halafu tunatoa misamaha kiholela, basi ni afadhali bajeti ya mwaka huu tuzibe hiyo mianya, futa kabisa hiyo misamaha isiyo na tija."

Lugola alisisitiza: "Hatuwezi kuendesha nchi kwa staili hiyo, lazima tufike mahali mambo ya kuwekeana kanuni kuwa tukikwamisha bajeti Bunge litavunjwa, acha livunjwe ili kuliponya taifa."

Lugola alisema kama Serikali haitakuja na mwarobaini wa misamaha ya kodi, ukwepaji wa kodi, matumizi makubwa ya Serikali na kupambana na ufisadi na wizi, bungeni hapatatosha.

Bofya hapa chini kwa habari zaidi.

Bajeti Kuu hatihati - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Kama yeye na wenzake wanaweza kusimama na kuigomea bajeti, kama wanaweza kuikosoa kwa kuzingatia udhaifu na nisikie mwishoni mtu anasema " kwa sababu ya kasoro hizo, siungi mkono bajeti hii mpaka irekebishwe" kama itaelekea huko...huenda ntakuwa nakaribia kufikiria kujiunga na CCM!

Vinginevyo hawa watu hawaaminiki hata kidogo!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nachelea sana kuwaamini wabunge wa CCM ... Mwakyembe alivyoweza kukana Thesis yake ilinikatisha tama sana ...wote nimewaweka kwenye list of "Guilt till proven innocent"...Otherwise anachokipigania ndicho ambacho Watanzania tunakitaka lakini ukweli ni kuwa tayari technocrats from WB na IMF wameshaidhinisha hiyo bajeti kwa niaba ya watu wa Marekani! Waziri wa Fedha alishapeleka najeti US na tayari imeshapitishwa!... Sad kujua kuwa jumla ya Misamaha ya kodi tunayotoa ni sawa na kiasi cha Misaada tunayopokea achilia mbali kodi na mirabaha inayolipiwa kwenye a/c za wachache ambao kati yao ni wastaafu walioshika madaraka makubwa ktk nchi hii na kuishia kufanya biashara wakiwa Ikulu! namlaumu sana JKN kutuaminisha eti Mkapa ni Mr Clean...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Elly B na RockSpider mnayosema ni kweli kabisa, ndiyo sababu pale juu nikamuomba Mungu ili watimize dhamira yao. Madudu yamekuwa mengi sana ndani ya hii Serikali dhalimu ufisadi wa kutisha miaka nenda miaka rudi, na yule CAG anakuwa kama anaimba mashairi kila mwaka anapotangaza madudu ndani ya Serikali huku kukiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya watendaji maovu. Imefikia mpaka Mawizara kupewa 17% to 71% ya bajeti waliyoomba lakini Wabunge wameuchuna tu. Kwa kweli Wabunge wa MACCM wamechangia sana katika uozo wote unaoendelea ndani ya hii Serikali dhalimu miaka nenda miaka rudi.

Kama yeye na wenzake wanaweza kusimama na kuigomea bajeti, kama wanaweza kuikosoa kwa kuzingatia udhaifu na nisikie mwishoni mtu anasema " kwa sababu ya kasoro hizo, siungi mkono bajeti hii mpaka irekebishwe" kama itaelekea huko...huenda ntakuwa nakaribia kufikiria kujiunga na CCM!

Vinginevyo hawa watu hawaaminiki hata kidogo!
 
Last edited by a moderator:
Hilo la kupinga bajeti kwa wabunge wa chama tawala halipo kabisa kwa kuwa maslahiyao ni ya muhimu zaidi ya maslahi ya nchi.Kumbuka alichofanyiwa lugola kwenye bajeti ya kilimo alipoomba wabunge wamuunge mkono kumbana waziri juu ya pembejeo feki na mbegu feki kwa wakulima, hakuna mbunge hata 1 ccm aliemuunga mkono na wao walioanza kumshambulia kana kwamba amelinajisi bunge na serikali.Hii ilikuwa ni ishara tosha kwa wakulima kuwa wanafanywa mradi kisiasa huko wakizidi kuumizwa na wanasiasa haohao na bahati mbaya sana bado wakulima wanalalama kwa sauti ya chini chini bila kuchukua hatua
 
Back
Top Bottom