Mbunge Livingstone Lusinde amtaka Spika Ndugai ajiuzulu, asema hata ombi lake la msamaha lilikuwa la uongo

Mgogo sawa na mmakonde. Msaidie chochote kesho hata sura yako haikumbuki.
Nimekua Dodoma vile vile nimekaa Mtwara na mikoa mingine mingi.
Shy , Toronto, that etc
Toronto kuna huo usnitch pia?
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Mungu wetu ni kijana mnoo.. Kuna alie ua watu sasa nae kesha oza. Ndugai akiona uspika kama Mungu wa mjengoni. Leo ana sulubiwa, Lissu ana kula bata. Yaani, Ccm mtafika motoni mkiwa mmechoka sana.
Watoto wadogo waliokufa nao waliua? Kaka yake Mbowe aliyekufa na Corona naye aliua?
 
Mjumbe hauwawi...
IMG-20220106-WA0030.jpg
 
Mbunge wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde amemtaka Spika Job Ndugai ajiuzulu kufuatia kauli aliyoitoa kupinga serikali kuchukua mikopo. Lusinde amesema alianagalia clip yote ya mazungumzo ya Job Ndugai na hakuna sehemu iliyounganishwa ili kumchonganisha na Rais kama yeye (Ndugai) alivyosema, alieleza zaidi kuwa hayo yalikuwa ni maneno yake na hivyo hata katika uombaji wake wa msamaha hakuwa na sababu ya kukanusha alichokisema. Lusinde amemtaka Spika Ndugai kujiuzulu mara moja ili kuwatendea haki wagogo pamoja na wakazi wa mkoa wa Dodoma ambao ni wanufaika mkubwa wa mkopo uliochukuliwa na serikali.
View attachment 2070646
Wewe kweli unavuta cannabis. Hayo lazima yalikuwa ni makubaliano ya awali. Hata kama hakujadiliana na baraza la mawaziri lakini mawaziri pia ni wabunge kwahiyo walipata nafasi ya kuujadili na kuupigia kura muswada bungeni!
 
Hatari sana, wanavyojua kucheza mchezo mchafu wa kisiasa, Kila mwenye ulimi hujitokeza kujifanya anajua kuongea, huku wakiziteka media na Huku upande wa pili wakilala Usingizi wa Pono, mwishowe huungana na kuwa kitu Kimoja kama vile sio wale mahasimu..
kila pande ya nchi Huu ndy wimbo sasa, Story za Mwamba alieko Jela na wananchi walionewa kipindi cha uchaguz wakiwa jela kwa kesi za kubumba haziongelewi tena.
Ni maajabu sana, wabunge waliochaguliwa na mtu mmoja wanahangaisha vichwa vya watanzania 60m.Huu uhalali ni wa kijuha kabsa. Kwanini kama Spika makosa yake yasiwe kiini cha kutupilia mbali Bunge zima tuanze Upya? Tuchuje makapi yote! Kwanini hili linashindikana? Mkuu wa Nchi anaogopa nini? VUNJA BUNGE TU...TUWAPIME!!

Naona upo obsseced na CHADEMA Sana. Kabla hujaongea Jambo fanya utafiti. Wewe unalaumu bila kupata taarifa za msingi.

Kwanza, fahamu ya kwamba suala la Mbowe kuwa mahabusu bado linaendelea halijaisha. Juzi tu hapa ulitokea ombi la mbowe kuomba msamaha Ili asamehewe CHADEMA ikaktaa. Kwani kuomba msamaha itakuwa kukubali makosa na kujishusha kwa Mwenyekiti wa CCM. Ukumbuke kesi imehairishwa tangu mwezi wa kumi na mbili nadhani itaendelea tarehe 14 January. Tusubiri mahakama itoe maamuzi yake iwe Ni batili au sahihi hiyo ndio utawala wa sheria. Wewe ultaka CHADEMA wavamie mahakama na kumtoa Mh Mbowe?. Pia mahakamani Viongozi wanahudhuria.

Pili, Kuhusu suala la uchaguzi ,CHADEMA walituma barua ikulu kwa ajili ya kuonana na Rais na Rais alijibu ombi lao nankukubali kuonana nao ila hakutoa tarehe rasmi. Hivyo, bado wanasubiri siku ambayo Rais atawalika ikulu wakaeleze dukuduku lao.

Tatu, tujifunze kuangalia Mambo kwa upana wake. Mgogoro Kati ya Speaker na Rais Ni advantage kwa CHADEMA maana speaker amewaumiza Sana bunge lililopita na Bunge la Sasa kwa kutokuheshimu maamuzi yao na kuruhusu wabunge 19 ambao chama hakikuwateua na ambao chama hakiwatambui. Hivyo wanaangalia kwa umakini ya kwamba iwapo speaker atajiudhuru, je anayekuja anaweza kusikiliza madai yao?.
 
Obsessed or obsseced?..ukifuatilia sana hoja yangu kwa tafakuri utaelewa tu.. !!
 
Back
Top Bottom