Mbunge Lijualikali atoa siri za CHADEMA; akana kumuoa mtoto wa Spika Ndugai

Sally82

Member
Apr 2, 2012
17
45
Lijuakali - Akana kumuoa mtoto wa Spika Ndugai

Lijuakali - Akana kusema kuwa CHADEMA waliiba kura 2015 (Mada iliyoandikwa JamiiForums)

Lijuakali - Akana maneno ya Lissu kuwa hakumlipa hela, adai alimlipa milioni 20

Lijuakali - Amsifia Lissu anapokuwa anafanya kazi zake za uwakili

Lijuakali - Hata kama CCM wakimkataa, hatarudi CHADEMA

Lijuakali - Akizungumzia alichosema Bulaya kuhusu yeye kuwa aweke akiba ya maneno, auliza kuwa Bulaya anaogopa nini Lijuakali asiseme anachojua

Lijuakali - Kuhusu ripoti ya CAG: CHADEMA kilimkopesha sehemu ya ruzuku Mbunge akanunue gari, baada ya gari kununuliwa gari hilo likawa linatumiwa na chama , kwahiyo mbuge alipewa pesa na chama ili anunue gari ili chama kikwepe kodi

Lijuakali - CHADEMA waliwafuata kuwa chama kinataka kununua magari ila hakina hela, kwahiyo chama kikawaomba wabunge ambao hawajatumia exemptions zao kutumia exemptions hizo kununua magari ya chama ili kukwepe kulipa kodi

Ninajaribu kujiuliza sana, yani mfano wake wa Mandela na kusamehe.. Sasa inakuaje rahisi sana kusamehe watu ambao walimfunga na kumtesa na kumbambikizia kesi miaka yote hiyo, halafu asisamehe hawa ambao wamepishana tu mawazo? Hayo mambo ya mwenyekiti na kuteua katibu mkuu then wakurugenzi mbona ni kama kila chama kina fanya hivyo? Kama chama anajua kinategemea nguvu ya wanachapa kukijenga analalamika nini? Na hizo hela za uchaguzi anazo lalamikia, mbona uchaguzi haujafika bado? Pia, si angeweza tu kusubiri muda wake wa ubunge uishe na aombe tu kazi yoyote, kwa hizi wiki zilizobakia kulikua na haja gani ya kujipa haya mausumbufu yote? Hizo wiki 2 wenzake walio toka zina mabadiliko yoyote ya maana katika kuwawakilisha wananchi wake, tofauti na wenzake walio toka? Nna maswali meengi ningetamani kumuuliza kama ningekua mwana habari mmoja wapo.. Lakini itoshe kwa haya baadhi
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,181
2,000
Watu tunaamini mtu ukifikia level ya kutungua sheria yaani Mbunge basi unakomaa kifikra na kimtizamo kumbe utoto mtupu..

Wengine wanasema wanabakwa sijui anatomaswa maziwa..yaani mama mtu mzima kabisa unatunga sheria...unashikwa shikwa maziwa unatakaa miaka 5 kimya useless..useless!!

Sisi tunahangaika na hawa vipepeo wetu under 18, ala kumbe kuna mijipepeo mizee mijinga kabisa...

Hii ni aibu kubwa saana...aibu
Mkuu 'FUSO'

Sijui niandike nini hapa kuweka mkazo kwenye maneno yako haya.

Lakini..., hiyo ndiyo sehemu kubwa ya jamii yetu.

Tupo hivyo. Wewe hata humu JF tu huwezi kuona akili za aina hiyo mkuu?

Na ndio maana wengi wetu tunawapenda sana CCM, na CCM kutupenda sana na kuhimiza tubaki hivyo hivyo ili watawale milele!
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,181
2,000
Ninajaribu kujiuliza sana, yani mfano wake wa Mandela na kusamehe.. Sasa inakuaje rahisi sana kusamehe watu ambao walimfunga na kumtesa na kumbambikizia kesi miaka yote hiyo, halafu asisamehe hawa ambao wamepishana tu mawazo? Hayo mambo ya mwenyekiti na kuteua katibu mkuu then wakurugenzi mbona ni kama kila chama kina fanya hivyo? Kama chama anajua kinategemea nguvu ya wanachapa kukijenga analalamika nini? Na hizo hela za uchaguzi anazo lalamikia, mbona uchaguzi haujafika bado? Pia, si angeweza tu kusubiri muda wake wa ubunge uishe na aombe tu kazi yoyote, kwa hizi wiki zilizobakia kulikua na haja gani ya kujipa haya mausumbufu yote? Hizo wiki 2 wenzake walio toka zina mabadiliko yoyote ya maana katika kuwawakilisha wananchi wake, tofauti na wenzake walio toka? Nna maswali meengi ningetamani kumuuliza kama ningekua mwana habari mmoja wapo.. Lakini itoshe kwa haya baadhi
Inawezekana (nasema inawezekana, kwa sababu ya 'pattern' ya mambo yanavyojitokeza); ukawa ni MKAKATI!

Hawa wabunge wanaomaliza muda wao wamepewa jukumu la kufanya hii kazi wakati huu?

Huoni 'pattern' inavyojirudiarudia kwa kila mmoja wao?

Alianza Mwita...
 
cotyledon

Senior Member
Aug 25, 2018
103
225
Huyu mtu ana uelewa mdogo sana, kazungumzia mengi, kawataja kina Msigwa na wengine watajibu wenyewe.

Hapa niongelee hili la yeye kuipinga hoja ya Chadema imemtoa mbali, anadai yeye na Chadema wote wametoana mbali, anasahau wakati Chadema imeanza harakati, yeye alikuwa hafahamiki popote na yeyote.

Nimuulize tu; kwanini aliamua kugombea ubunge wa jimbo lake kupitia Chadema na kuviacha vyama vingine vya upinzani?

Kama kweli anajiona yeye na Chadema ni nguvu sawa, kwanini asingegombea ubunge wa jimbo lake kupitia TLP au NCCR?

Na kama anajiamini ana nguvu, kwanini sasa hivi amekimbilia CCM akawe hata mfagizi, kwanini asiende kufagia TLP au Chaumma?!

Utaona wazi tu hapa kwamba, huyu jamaa anapenda kujitutumua, ila kwa kifupi ni mtu asie na shukrani, na asiejiamini, anajiona mwenye nguvu, ila anapenda kujiegemeza kwa ambavyo vimeshajengwa tayari na kusimama.

Kama kweli ana nguvu anazojinasibu anazo, atoke, aanzishe chama chake, halafu agombee ubunge tumuone.

Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema yenyewe haina shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
2,693
2,000
Hakuwa na sababu ya kuichafua CHADEMA angesema nimeamua kuunga juhudi kutokana na kasi ya maendeleo yanayofanywa na awamu hii.
Kusema njaa tunakosea ,ukosefu wa hekima,Busara unahusika.
+utoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ameahidi kuwa akiguswa tena, basi ile formular ya fizikia (nimeisahau) ataitumia. Amewapiga mkwara akina Mbowe na Company.

Kijana anatisha huyu, kweli LUMUMBA watampa cheo tu. Kamwe nyanya haendi kulima.
 
JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
944
1,000
Duh, namfikiria kibaraka Yeriko Nyerere aliyesema kwa sauti kubwa kwamba Lijualikali kamuoa mtoto wa Spika! Kumbe naye ni pololo
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,980
2,000
Ninajaribu kujiuliza sana, yani mfano wake wa Mandela na kusamehe.. Sasa inakuaje rahisi sana kusamehe watu ambao walimfunga na kumtesa na kumbambikizia kesi miaka yote hiyo, halafu asisamehe hawa ambao wamepishana tu mawazo? Hayo mambo ya mwenyekiti na kuteua katibu mkuu then wakurugenzi mbona ni kama kila chama kina fanya hivyo? Kama chama anajua kinategemea nguvu ya wanachapa kukijenga analalamika nini? Na hizo hela za uchaguzi anazo lalamikia, mbona uchaguzi haujafika bado? Pia, si angeweza tu kusubiri muda wake wa ubunge uishe na aombe tu kazi yoyote, kwa hizi wiki zilizobakia kulikua na haja gani ya kujipa haya mausumbufu yote? Hizo wiki 2 wenzake walio toka zina mabadiliko yoyote ya maana katika kuwawakilisha wananchi wake, tofauti na wenzake walio toka? Nna maswali meengi ningetamani kumuuliza kama ningekua mwana habari mmoja wapo.. Lakini itoshe kwa haya baadhi
Huu mfano haukuwa sahihi. Mandela aliwasamehe maafisa jela lakini sio serikali ya makaburi. Ndio maana hakujiunga na chama cha The National Party baada ya kuachiwa na alisimamia uundwaji wa the Truth and Reconciliation Committee ili ukweli ujulikane. Ndio maana Bulaya alimshauri aweke akiba ya maneno. Sio kwamba afiche madudu lakini asijisemee tu ili mradi anataka kukichafua chama chake cha awali.

Amandla....
 
Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
4,980
2,000
Mimi nawashangaa hawa vijana. Hapakuwa na haja ya kugeuza suala lao kuwa mpambano wao binafsi na Mwenyekiti. Wao wangetoka tu kama walivyojiunga na kuanza kupigia debe sera za chama chao kipya. Hii ya kushinda kurudia shutuma ambazo zimekuweko kwa miaka mingi hakuwasaidii kitu. Na kama kweli Mheshimiwa hakuandika ile taarifa ya kukiri kuwa alishinda ubunge wake kwa kuiba kura basi ajue hata huko anakoenda tayari ana watu wasiomtakia mema.

Amandla...
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,227
2,000
Hii kashfa TAKUKURU impandishe mbowe mahakamani

Top Bottom