Mbunge kutakiwa kujua tu kusoma na kuandika inahitaji mabadiliko. Angalau mbunge awe amemaliza form six au awe na digrii moja

Yenga08

JF-Expert Member
Jul 7, 2019
464
891
Kama tuna wabunge lukuki waliopata ubunge kwa kigezo cha kujua kusoma na kuandika, sis kama raia tunategemea nin juu ya hawa wabunge, ni sawa na kipofu kumuongoza njia anayeona. Unaona kabisa anayekuongoza njia anakupoteza ila kwa kuwa umempa mamlaka ya kukuongoza umvumilie tu kupotezwa eti huna namna, hii hapana tunapaswa sas tuwakatalie tena kwa juhudi zetu zote.

Mwanasheria anasomea mambo ya sheria miaka minne, halafu anayetunga sheria ni Bunge, na moja yakigezo cha kuwa mbunge(mtunga sheria) ni kujua kusoma na kuandika.

Hapa Watanzania inatakiwa tuwe serious tena sana., hii kitu inatakiwa mabadiliko angalau kuwa mbunge uwe umemaliza form six au uwe na degree moja.

Yaani ukiangalia bado tupo nyuma sana, sheria ya kigezo cha kusoma na kuandika iliwekwa enzi zile wasomi walikuwa wachache sana, na sas tuna wasomi wengi tu kila sehem vijijini na mjini.

Watawala wangekuwa wanalitakia mema Taifa hili, wangesubutu kufanya mabadiliko ya katiba ili vigezo vya Ubunge, na mamlaka ya Rais vibadilike na tuanze navyo uchaguzi wa 2025.

Ila kwa kuwa watawala wanaona haina haja ya kufanya mabadiliko ya katiba, sis raia wanatuaminisha kuwa wao niwanufaika wakubwa wa Katiba iliyopo, ila wakae wakijuwa raia nao wanaelimika kila kukicha. Ipo siku mabadiliko yatakuja na watawala watashangaa sana maana hawategemei hata siku moja mabadiliko kutokea katika Taifa hili.
 
lisikika sauti kutoka nyikani yani AKILI NDOGO KUONGOZA AKILI KUBWA usisahau dereva wa mbunge anatakiwa awe msomi hapa ndopale umuhimu wakatiba unapoongezeka"
 
Back
Top Bottom