Mbunge kumaliza mgogoro wa wananchi na shirika la reli

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Leo tarehe 22.08.2016 Mbunge wa mkoa wa Ilala CHADEMA Mh Anatropi Theonest pamoja na uongozi wa kamati inayoshughulikia mgogoro wa wakazi wa Tabata na shirika la reli nchini wamekutana na uongozi wa shirika hilo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo uliodumu kwa kipindi kirefu sasa.

Kiini cha mgogoro huo ni kutokana na shirika la reli nchini kuwawekea alama ya X ili kupisha eneo la reli ambalo wakaazi hao wanataka kulipwa fidia kutokana na maeneo kuwa yameendelezwa tangu waanze kuyamiliki miaka zaidi 30 iliyipita.

Kwa takribani miaka 30 kumekuwepo na jitihada mbalimbali za wananchi hao kutaka kupatiwa ufumbuzi bila mafanikio kutokana na mkanganyiko wa sheria ambapo huko nyumba sheria ilitambua makazi yao kwa wananchi kuwa nje ya eneo la reli kwa mita 15 tofauti na sasa ambapo sheria inataka wananchi kuwa nje ya eneo la reli kwa mita 30.

Katika kile kinachoonekana kama kufunguliwa kwa mlango wa mazunguzo kati ya wananchi hao wanaowakilisha zaidi zaidi ya familia 130 ,baada ya kufika ofisi ya mbunge wa Ilala viti maalum Mh Anatropia Theonest amefanikiwa kukutanisha pande hizo mbili kati wananchi kwa upande mmoja na RAHCO kwa niaba ya shirika la reli nchini kwa ajili ya kupata ufumbuzi.

Ni katika kikao cha leo kulichofanyika ofisi za shirika, Wananchi wamefanikiwa kukutana na katibu mkuu wa RAHCO Dr Musa Mgwata na kuwasilisha kilio chao cha kupatiwa fidia ya maeneo yao kutokana na gharama kubwa walizowekeza katika maeneo yao.

Akijibu hoja za wakaaazi hao wa Tabata, katibu huyo amemshukru mh Mbunge kwa jitahada zake za kumaliza mgigoro huo huku akimwahidi mh Mbunge na wananchi wa eneo hili kurudi ofisini mwake tarehe 25 /08/2016 kwenda kupata majibu na muafaka waliofikia wao kama shirika kwa kuzingatia kilio cha wananchi wa eneo hilo.
Imetolewa na ;

Ofisi ya Mbunge
Anatropia Theonest
August 23,2016
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Sifa za Kijinga tu mgogoro bado haujaisha kwani huwezi juwa jibu la Rahco hiyo tarehe 25
Well, atleast he gave a try and amejaribu kufanya mediation, the same can't be said kwa previous/other people who were in a similar position ambapo wangeweza kuwa msaada kwa hao wananchi
 
Good,Anatropia Theonest.

One of the mostly qualities of a good leader is an ability to solve problems and not to create them.
 
Back
Top Bottom