Mbunge kortini kwa kumkashifu Kikwete

.....kwa kumppeleka mahakamani wamempa umaarufu..na hata wale wananchi waliokuwa hawajuwi kuwa jk ...ana jina lingine la "mchekajichekaji"...kama de.... basi wamejuwa...., bora wangekaaga kimya ....maana kila anapofikishwa mahakamani tutakumbushwa kuwa anafikishwa kwa kosa la kusema ukweli kuwa rais wetu amezidi kuchekacheka !!![[hata kwa issues serious]...ndio tatizo la kuchagua watu ambao muda wote wanafikiri wanatongoza!!

kwa kiinglish hii inaitwaje,ili tupate jina fupi la presida wetu...kiswahili kimekuwa kirefu mno..
 
...Hiyo mbona ni tisa, kumi soon utasikia katokea mtu kampiga na yai viza!!! watu wamedata mazee!!

ndio maana watu wengi wanaamini siku alipoongea na wananchi live ..zile simu watu waliokuwa wakipiga walikuwa wanakuwa monitored na usalama ..kwani mimi hofu kubwa niliyokuwa nayo siku ile ni ya uwezekano wa jk kutukanwa na wananchi waliopinda...nadhani wangeachia zile simu wazi bila udhibiti haingekuwa ajabu mtu kumtukana na akaingia mitini!!!..sijui tido angefanyaje....
 
Wakili huyo wa serikali aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walisababisha usumbufu kwa majirani waliokuwapo katika eneo hilo.
watakuwa ni watu wa CCM tu hao majirani wenyewe.!

Wakizungumza na gazeti hili nje ya mahakama ya hiyo, wafuasi hao walieleza kuwa kukamatwa kwa viongozi hao hakumaanishi kuwa ndio mwisho wa kufanya mikutano na walilifananisha tukio hilo kama ni vita ya kisiasa hasa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Wanatakiwa wananchi wakomae KI UKWELI mpaka haki yao ipatikane
 
Anachekacheka kama Kanumba alipokua big bro house au???

hivi kwa namna rais wetu anavyopenda ku smile smile.....anaweza kukaa kati kati ya Huku CHEVES ..huku AHMEDENAJAD..HUKU..ghadafi..huku..MORALES.. huku..KIM JONG IL...

au mmepata kumuona putin ..au ...medeyev wakicheka...

kwa majirani mmepata kuona kagame,museveni,kibaki au bingu wanacheka..???..viongozi ambao wanaweza kumkaribia jk kwa kucheka na kutake issues ize ni kama zuma,mswati ....sikumbuki mwingine....

hawa marais sijapata kuwaona wakicheka hata mara moja...sijui labda wakiwa chemba na wenziwao[ambao wala sijapata kuwaona ..kuacha cheves ambaye naomi campbell alijipeleka akalambwa...akaachwa]...nahisi jk akikaa kati kati ya hawa mabazazi wanaweza wakajaribu kutest zali..kama vipi!!
 
Mimi ningependa kujua hiyo sheria inayomlinda rais na kashfa/matusi! Ivi yule aliyempiga Mwinyi kibao si ilikuwa ni assault?
 
Nyerere aliitwa mchonga meno ( na kweli meno yake yalikuwa yamechongwa) mbona hakutinga mtu mahakamani kwa kumkejeli Rais? Huyu Mbunge wa CUF kasema JK anacheka cheka ( na ni kweli anafanya hivyo) kwa nini apelekwe mahakamani? Kumfurahisha bwana mkubwa? Mimi nadhani sasa hivi ni: KILIMO KWANZA!! RAIS ATAFURAHI SANA.
 
Upuuzi hawishi nchi hii mijizi na mijambazi inaachwa inatembea wasema kweli ndo wanabanwa.

kwa ajili mijizi na mijambazi yote inachekacheka, hatutaki watu serious TZ.
lidumu tabasabu, lidumuuuuu
 
waliochukua hatua wana nia mbaya na Rais kwa upande mmoja lakini huyu mama naye ajifunze kuchagua maneno, yukohovyohovyo kwa kauli.
 
  • Adaiwa kusema kazi ya rais ni kuchekacheka, ameshindwa kuongoza na anakumbatia mafisadi
Na Benedict Kaguo,Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu-CUF, Bi. Nuru Awadh Bafadhili na viongozi wengine waandimizi wa Chama hicho wilaya ya Tanga wamekamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.

Mbunge huyo na wenzake walifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga mbele ya Hakimu Mkazi, Bw.Laurent Mbuya na kusomewa mashtaka matatu ya kula njama za kutenda kosa, kukusanyika bila kibali na kutumia lugha ya kashfa kinyume cha sheria.

Wakili wa Serikali, Bi.Doroth Massawe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa 10 hadi 12 jioni eneo la Chuda jijini
Tanga, mbunge huyo ambaye ni mshitakiwa wa kwanza na wenzake walifanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Kikwete kuwa na kazi yake ni kuchekacheka na ameshindwa kuongoza na kukumbatia
mafisadi hali iliyosababisha uvunjifu wa amani.

Wakili huyo wa serikali aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walisababisha usumbufu kwa majirani waliokuwapo katika eneo hilo.

Mbunge huyo na wenzake, Rashid Jumbe, Diwani wa Kata ya Mwanzange (CUF), Mussa Mbarouk, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini (CUF), Abdarhman Hassan Mkurugenzi wa haki za Binadamu wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Amina Yusuph na Mohamed Asilia kwa pamoja wamekana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana hadi Oktoba 12 mwaka huu kesi yao itakapojatwa tena.

Mamia ya wafuasi wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo wengi wao kutoka maeneo ya vijijini wakitaka kujua hatma ya viongozi wao kushikiliwa.

Wakizungumza na gazeti hili nje ya mahakama ya hiyo, wafuasi hao walieleza kuwa kukamatwa kwa viongozi hao hakumaanishi kuwa ndio mwisho wa kufanya mikutano na walilifananisha tukio hilo kama ni vita ya kisiasa hasa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa CUF ambao hawakutaka kutajwa majina yao walieleza kuwa pamoja na tukio hilo bado wataendelea kufanya mikutano ya hadhara ili kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.

Hiyo kwenye red imenimaliza kabisa nguvu. Huyu mama yuko wapi nimpe zawadi kwa kusema kile ambacho watu wengine wanakisema sirini kwa kuogopa "kuvunja amani".
 
Hivi mbunge kweli anakamatwa kwa kufanya mkutano bila kibali,tunakwenda wapi?Mimi nachofahamu mkutano hauna kibali kwani kinachofanyika ni kutoa taarifa polisi ndani ya saa 48 kwa mujibu wa Police force ordinance as amended from time to time.Sasa kibali kilichotakiwa ni kipi?cha kuruhusiwa kumtukana rais au nini?
 
Polisi wanaolinda mafisadi na mahakama za kifisadi sasa zinaanza kutisha watu kuhusu kutoa kauli za kweli kabisa kuhusu Kikwete. Alichosema huyo Mama ni kweli tupu hakuna kashfa hapo hata moja.
 
siku zote hakuna kitu kibaya kama kusema ukweli......mi nawambia ukweli unauma jamami!!!!!!!!!!!!!11
 
.....kwa kumppeleka mahakamani wamempa umaarufu..na hata wale wananchi waliokuwa hawajuwi kuwa jk ...ana jina lingine la "mchekajichekaji"...kama de.... basi wamejuwa...., bora wangekaaga kimya ....maana kila anapofikishwa mahakamani tutakumbushwa kuwa anafikishwa kwa kosa la kusema ukweli kuwa rais wetu amezidi kuchekacheka !!![[hata kwa issues serious]...ndio tatizo la kuchagua watu ambao muda wote wanafikiri wanatongoza!!
PM ! Habari nzito hiyo. tehe tehe tehe!
 
Sasa na watu hawa wanaotoa mawazo yao kwa uwazi nao siku moja wajiandae kukamwatwa pia na ndio huko tunakokwenda
 
1. Bad precedent

2. Hakika kama kashfa zenyewe ndizo hizi basi hii ni kesi ya kisiasa tu. Namuunga mkono huyu mbunge na hili swala ni vigumu kuliprove either way kwa sababu mambo mengi ni disputable and subject to interpretation, lakini mimi naona mbunge kasema kweli.

Kama wanataka kumfanya martyr wamfunge

Wakili wa Serikali, Bi.Doroth Massawe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa 10 hadi 12 jioni eneo la Chuda jijini
Tanga, mbunge huyo ambaye ni mshitakiwa wa kwanza na wenzake walifanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Kikwete kuwa na kazi yake ni kuchekacheka na ameshindwa kuongoza na kukumbatia
mafisadi hali iliyosababisha uvunjifu wa amani.
 
Hivi Siku hizi ukimcheka Mkuu unashitakiwa? Au ukisema kwamba yeye anapenda kucheka cheka cheka opia ni kosa? Mbona ni kweli kwamba kikwete akifurahi hucheka na hcheka sana tu sasa kosa loko wapi?

Hakimu atakaye entertain kesi hii naye atakuwa hazimo maana kila mtu wakati mwingine hucheka cheka kama ana fulaha moyoni.. hata hapa nilipo nacheka cheka tu kwa kuisoma habari hii... na mKUU ni binadamu kama wengine kucheka kwake ni jambo la kawaida ingawaje wakati mwingine huwa serious...Hakuna shida ni kweli mkuu na wengineo akiwemo mimi hucheka... itakuwa vituko kwa watu kufunguliwa mashitaka kwa kusema kwamba mkuu hucheka cheka wakati ni kweli akiwa ana furaha hucheka hata yeye akiulizwa atakakubali tu... hebu moderator tafuta namna ya kumwuuliza tuone kama hakubali...
 
  • Adaiwa kusema kazi ya rais ni kuchekacheka, ameshindwa kuongoza na anakumbatia mafisadi
Na Benedict Kaguo,Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu-CUF, Bi. Nuru Awadh Bafadhili na viongozi wengine waandimizi wa Chama hicho wilaya ya Tanga wamekamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.

Mbunge huyo na wenzake walifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga mbele ya Hakimu Mkazi, Bw.Laurent Mbuya na kusomewa mashtaka matatu ya kula njama za kutenda kosa, kukusanyika bila kibali na kutumia lugha ya kashfa kinyume cha sheria.

Wakili wa Serikali, Bi.Doroth Massawe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa 10 hadi 12 jioni eneo la Chuda jijini
Tanga, mbunge huyo ambaye ni mshitakiwa wa kwanza na wenzake walifanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Kikwete kuwa na kazi yake ni kuchekacheka na ameshindwa kuongoza na kukumbatia
mafisadi hali iliyosababisha uvunjifu wa amani.

Wakili huyo wa serikali aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walisababisha usumbufu kwa majirani waliokuwapo katika eneo hilo.

Mbunge huyo na wenzake, Rashid Jumbe, Diwani wa Kata ya Mwanzange (CUF), Mussa Mbarouk, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini (CUF), Abdarhman Hassan Mkurugenzi wa haki za Binadamu wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Amina Yusuph na Mohamed Asilia kwa pamoja wamekana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana hadi Oktoba 12 mwaka huu kesi yao itakapojatwa tena.

Mamia ya wafuasi wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo wengi wao kutoka maeneo ya vijijini wakitaka kujua hatma ya viongozi wao kushikiliwa.

Wakizungumza na gazeti hili nje ya mahakama ya hiyo, wafuasi hao walieleza kuwa kukamatwa kwa viongozi hao hakumaanishi kuwa ndio mwisho wa kufanya mikutano na walilifananisha tukio hilo kama ni vita ya kisiasa hasa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa CUF ambao hawakutaka kutajwa majina yao walieleza kuwa pamoja na tukio hilo bado wataendelea kufanya mikutano ya hadhara ili kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.

Majeshi yetu including hawa wanaitwa usalama wa chama cha majambazi ndio kazi waliobaki nayo.
Inashangaza sana kiasi kwamba sasa hata viongozi weetu wametumia ujinga wa hawa malugaluga kuiibia nchi kiulaini?
Vitisho as if wao hawatakufa ndio vimejaa.
Anyway. Mwisho wetu wote ni kifo na tukitokea tu mbele za muumba hapo ndipo watajua wanayofanya sasa yana malipo.
Ila tu Mungu ninayemfahamu mara nyingine uanza kulipa hapa hapa na hivyo utawasikia wakifa na mipresha na kuacha kila kitu hapa wakifaidi wengine. Na kwa kuwa wamekuwa wajinga kiasi cha kutotafakari hili, nawaonea huruma. Ni bora wageuke nyuma wamkimbirie Mungu na kuacha dhuluma.
Mungu hajui kama wewe ni Polisi au usalama wa chama cha wezi Tanzania. Yeye anakuangalia na unyofu wako wa moyo.
Tumechoka kutishwa.
 
Back
Top Bottom