Mbunge kortini kwa kumkashifu Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge kortini kwa kumkashifu Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 29, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  • Adaiwa kusema kazi ya rais ni kuchekacheka, ameshindwa kuongoza na anakumbatia mafisadi
  Na Benedict Kaguo,Tanga

  MBUNGE wa Viti Maalumu-CUF, Bi. Nuru Awadh Bafadhili na viongozi wengine waandimizi wa Chama hicho wilaya ya Tanga wamekamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.

  Mbunge huyo na wenzake walifikishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga mbele ya Hakimu Mkazi, Bw.Laurent Mbuya na kusomewa mashtaka matatu ya kula njama za kutenda kosa, kukusanyika bila kibali na kutumia lugha ya kashfa kinyume cha sheria.

  Wakili wa Serikali, Bi.Doroth Massawe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Septemba 27 mwaka huu majira ya saa 10 hadi 12 jioni eneo la Chuda jijini
  Tanga, mbunge huyo ambaye ni mshitakiwa wa kwanza na wenzake walifanya mkutano bila kibali na kumkashifu Rais Kikwete kuwa na kazi yake ni kuchekacheka na ameshindwa kuongoza na kukumbatia
  mafisadi hali iliyosababisha uvunjifu wa amani.

  Wakili huyo wa serikali aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walisababisha usumbufu kwa majirani waliokuwapo katika eneo hilo.

  Mbunge huyo na wenzake, Rashid Jumbe, Diwani wa Kata ya Mwanzange (CUF), Mussa Mbarouk, Diwani wa Kata ya Ngamiani Kusini (CUF), Abdarhman Hassan Mkurugenzi wa haki za Binadamu wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Amina Yusuph na Mohamed Asilia kwa pamoja wamekana mashtaka hayo na wako nje kwa dhamana hadi Oktoba 12 mwaka huu kesi yao itakapojatwa tena.

  Mamia ya wafuasi wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo wengi wao kutoka maeneo ya vijijini wakitaka kujua hatma ya viongozi wao kushikiliwa.

  Wakizungumza na gazeti hili nje ya mahakama ya hiyo, wafuasi hao walieleza kuwa kukamatwa kwa viongozi hao hakumaanishi kuwa ndio mwisho wa kufanya mikutano na walilifananisha tukio hilo kama ni vita ya kisiasa hasa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa CUF ambao hawakutaka kutajwa majina yao walieleza kuwa pamoja na tukio hilo bado wataendelea kufanya mikutano ya hadhara ili kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kushiriki uchaguzi huo.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  He he he he well said.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahah nilidhani wa CCM ....ningeshangaa sana!
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  jamani si rais mwenyewe alisema kuchekacheka kwake sio kuwa yeye ni mpole..sasa hapo kakashifiwa nini..teh teh kazi ipo mwaka huu
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,876
  Likes Received: 23,503
  Trophy Points: 280
  Message sent and DELIVERED!
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Yaani ndugu zangu tutaona mengi sana katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwakani
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu angalia sana maneno yako na jamaa wa CUF, au umesahau ule usemi wa wahenga wetu zamani kuwa UKWELI UNAUMA??
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  eeeeh
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Vipi tena...habari ndo hiyo,, sasa hapo watawakamata wangapi? na je ingekuwa Lipumba wangemkamata? manake nadhani yeye na maalim huwa wana maneno makali zaidi ya hayo.

  kisha kashfa ni nini hasa? wale waliomuliza maswali ya moja kwa moja kwen Tv majuzi mbona hawajakamatwa?
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ndio maana kila kesi wakipeleka mahakamani wanashindwa. KUKURUPUKA
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Naona Jeshi la polisi hapa wameamua kumpelekea JK message direct kuwa "kazi yake ni kuchekacheka na kukumbatia mafisadi". Wasingewapeleka mahakamani asingepata huu ujumbe!
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Hawana kazi hao poilisi na kufanya kazi kwa woga na kujipendekeza tuu,hawana sheria yeyote hapo ya kuwashitaki na kupata conviction kwa hao jamaa ni kupoteza muda tuu na pesa walipa kodi,lakini hii ndio legacy ya CCM!
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ni sheria ipi? na kama rais anafanya madudu, tunapaswa kukaa kimya? Na uhuru wa kutoa maoni je? hii haijatulia kabisa!!
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  unajua ccm ni chama chenye vituko na akili za kitoto duniani kushinda chama chochote kile.sasa mtu kasema ukweli unampeleka mahakamani? sasa demokrsia hiko wapi hapa? hivi hakuna hata mmoja wao mwenye common sense ya kuwaambia "jamani hapa tunachemsha"?.manake hapa polisi wao wametumwa tu hamna kitu kama cha kuchafua amani kwa kusema ukweli kuhusu ufanyaji kazi wa raisi hata kama si kweli lakini hayo ni maoni yake na ndio jinsi anaona ufanyaji wa kazi wa raisi huko hivyo.raisi wote duniani kazi zao uchambuliwa wao kama hawataki wasigombee uongozi.inamana watanzania hatuna haki ya kutoa maoni jinsi raisi wetu anavyofanya kazi?
   
  Last edited: Sep 29, 2009
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  .....kwa kumppeleka mahakamani wamempa umaarufu..na hata wale wananchi waliokuwa hawajuwi kuwa jk ...ana jina lingine la "mchekajichekaji"...kama de.... basi wamejuwa...., bora wangekaaga kimya ....maana kila anapofikishwa mahakamani tutakumbushwa kuwa anafikishwa kwa kosa la kusema ukweli kuwa rais wetu amezidi kuchekacheka !!![[hata kwa issues serious]...ndio tatizo la kuchagua watu ambao muda wote wanafikiri wanatongoza!!
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  lakini mbona hawakumshika maalim ..ambaye mara nyingi tu akiojiwa kwenye tv humponda jk kwa kusema anacheka cheka....hata kwa ishu muhimu kama muhafaka....?
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  hivi watamtia hatiani kwa sheria gani???...wanasheria jk tusaidieni...

  ukimuambia mtu anacheka cheka ni tusi au umemsifia .......,nadhani ingekuwa amesema anacheka cheka kama ,mwanamke ...kidogo ingeleta mantiki ya tusi..but kuchekacheka si tusi....hapa polisi ndio wamemtukana rais......na wataambiwa wafute kesi maana inaendelea mchafua rais.....

  je wamejaribu kupima madhara atakayopata rais kulinganisha na adhabu ya juu ya kutoa lugha "chafu"...ambayo ni kifungo cha miezi mitatu au faini ya pesa ndogo tu au onyo!!!
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Upuuzi hawishi nchi hii mijizi na mijambazi inaachwa inatembea wasema kweli ndo wanabanwa.
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hiyo mbona ni tisa, kumi soon utasikia katokea mtu kampiga na yai viza!!! watu wamedata mazee!!
   
 20. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anachekacheka kama Kanumba alipokua big bro house au???
   
Loading...