Mbunge Komba analala Bungeni wakati Mbamba Bay inazidi kudumaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Komba analala Bungeni wakati Mbamba Bay inazidi kudumaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 8, 2011.

1. Candid Scope

Candid Scope JF-Expert Member

#1
Jul 8, 2011
Joined: Nov 8, 2010
Messages: 11,896
Likes Received: 119
Trophy Points: 160
[​IMG]
Bandari ya Mbambabay- Mkoani Ruvuma kando ya ziwa Nyasa​

NI nchi chache duniani zinazoweza kuwa na jiografia nzuri kama Tanzania, halafu ziwe dhaifu katika matumizi ya jiografia hiyo katika kujiendeleza.
Tanzania ina ufukwe wa bahari upatao kilometa 1,424 na ndani yake kuna bandari za Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na Zanzibar kwa upande wa Mashariki. Upande wa kaskazini, kaskazini magharibi, magharibi na kusini magharibi, inapakana na nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia na Malawi. Haya yote ni mataifa ambayo hayakujaliwa milango ya bahari, hivyo ni tegemezi kwa mataifa ya Tanzania, Kenya, na Msumbiji, kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa zao. Tanzania ina fursa kubwa zaidi kuliko nchi nyingine nilizozitaja. Miongoni mwa nchi hizi tatu – yaani Tanzania, Kenya na Msumbiji, Tanzania ina nafasi ya kipekee kabisa. Ni tofauti na Kenya, ambayo inapakana na nchi moja tu isiyokuwa na bandari ambayo ni Uganda.

Pia, ni tofauti na Msumbiji, ambayo inapakana na nchi zisizokuwa na bandari za Swaziland, Zimbabwe na Malawi. Tanzania inayopakana na mataifa sita yasiyo na bandari. Hii ina maana kwamba bandari za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara ni maeneo ambayo yalitakiwa kuwa na pilikapilika nyingi katika harakati za usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka katika nchi hizi za jirani. Bandari hizi zilitakiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ajira na cha mapato ya nchi, lakini kwa bahati mbaya haiko hivyo, kwani zimekuwa zikisuasua miaka nenda miaka rudi. Tukiachana na bandari zilizo katika mwambao mwa bahari ya Hindi, pia nchi yetu ina bandari katika maziwa kama vile bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo katika Ziwa Victoria, bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika na Bandari ya Mbamba Bay katika mwambao wa Ziwa Nyasa.

Kabla ya kuendelea ni vyema nikakujuza mpendwa msomaji, kuwa lengo la makala haya si kuzungumzia bandari pekee, bali nimeanza kwa utangulizi huo kwa kuwa baada ya kufika Mbamba Bay, nilijiuliza maswali mengi kwamba kwa nini fursa hiyo haitumiki kuendeleza eneo hilo kupitia shughuli za kiuchumi, badala yake eneo hilo limeendelea kubaki katika umasikini wa kupindukia. Tofauti na bandari zilizopo katika mwambao mwa Ziwa Victoria na bandari ya Kigoma, bandari ya Mbamba Bay imeachwa mbali katika suala zima la utoaji huduma, kwani haina mchango mkubwa wa kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine ya jirani. Bandari imekuwa ikisaidia kusafirisha abiria waishio katika maeneo yaliyopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. Maeneo haya ni pamoja na Lupingu, Manda, Mbamba Bay na sehemu kadhaa zilizopo mwambao mwa ziwa hilo.

Wasafiri wa eneo hilo wamekuwa wakitumia meli ya mv Songea, ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Kyela mkoani Mbeya hadi Mbamba Bay na kisha kuelekea Nkhata Bay katika nchi jirani ya Malawi. Tofauti na wengi wanavyodhani, kuwapo kwa meli hii katika eneo hilo, hakusaidii sana kuinua shughuli za kiuchumi zinazoweza kuchangamsha eneo hilo, badala yake maisha ya wananchi yameendelea kuwa duni. Mbamba Bay haionekani kuwa eneo lenye maendeleo ya kasi, badala yake limeendelea kuonekana kama mji wa kihistoria. Mji uliojaa majengo ya zamani ya wenyeji, yaani mchanganyiko wa makabila ya Wamanda, Wanyasa na Wamatengo kutoka maeneo ya milimani.

Kwa ambao hawajawahi kufika Mbamba Bay, niwafahamishe kuwa wakazi wa eneo hili hawakupaswa kuwa masikini, kwa kuwa ni eneo lenye neema kubwa, ya kuwa moja ya maeneo maarufu kwa shughuli za utalii na pilika pilika nyingine za kiuchumi. Ukiwa umbali wa kilometa kumi hivi, eneo la milimani karibu ya kufika eneo hili, unaweza kujionea mandhari tulivu na kufaidi upepo mwanana, unaovuma kutoka katika ziwa Nyasa, lililojizamisha katika ya bonde la ufa. Sio siri, mandhari ya eneo hilo hasa maeneo ya mwambao ni ya aina yake, kwani eneo hili limejaliwa fukwe safi na maji ya ziwa ambayo hayajachafuliwa, tofauti na maeneo mengine kama hayo ambayo niliwahi kuyatembelea. Ukweli ni kwamba iwapo serikali ikijipanga vyema kuhamasisha utalii katika eneo hilo, watalii lukuki watamiminika katika eneo hilo.

Tofauti na maeneo mengine nchini, yenye mchanganyiko mkubwa wa watu, wakazi wa Mbamba Bay wanaonekana labda kutokana na mazoea, fukwe nzuri walizonazo hawazioni kama fursa muhimu. Baadhi ya wenyeji niliozungumza nao, wanasema kuwa hawana utamaduni wa kutembelea ufukoni kwa ajili ya kupunga upepo na kufurahia mandhari ya eneo hilo, kwa kuwa mazingira hayo wameyazoea. Wanasema kuwa wamekuwa wakienda katika eneo hilo kwa shughuli mbalimbali, kama vile kufua nguo, kuoga au kununua samaki kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki kienyeji, yaani kwa kutumia mitumbwi midogo na ndoano.

Alex Komba ni mkazi wa eneo hilo, ambaye anasema kuwa kwa wenyeji wa eneo hilo suala la mandhari nzuri ya eneo hilo, si lolote si chochote, kwa kuwa wameizoea, ndio maana maeneo ya ufukweni yanauzwa bei rahisi, sawa na maeneo mengine. "Hapa ukija na laki tatu au nne, unapata kiwanja mara moja, tena ukiwa na milioni moja na nusu au mbili, unaweza kumhamisha mtu katika kibanda chake. Unadhani watu wa hapa wanababaishwa na haya maji?

Kama vipi toa fedha nikutafutie eneo," anaeleza Komba. Wakieleza sababu ya eneo hilo kudumaa kimaendeleo, wanasema kuwa ubovu wa barabara na mawasiliano hafifu ya redio na simu ni miongoni mwa sababu ambazo zinazokwamisha maendeleo ya eneo hilo. Margareth Nchimbi ni mama ntilie anayefanya biashara hiyo Mbamba Bay, ambaye anaeleza kuwa hadi sasa katika eneo hilo, hakuna mawasiliano ya redio za hapa nchini, badala yake wamekuwa wakisikiliza Redio Malawi. Kwa upande wa simu, anasema kuwa kwa miaka mingi eneo hilo hakikuwa na mawasiliano ya simu, jambo ambalo lilikuwa likikwamisha shughuli za kibiashara na maendeleo yao.

Lakini, hali ni tofauti kwa sasa, ambapo huduma za mawasiliano zimeanza kuboreka baada ya baadhi ya kampuni za simu, kusimika minara ya mawasiliano katika eneo hilo. Hali ya eneo hilo kuwa duni, imeendelea kutowavutia wawekezaji kutoka maeneo mengine nchini, hivyo wakazi wake wanaendelea na shughuli yao kuu ya uvuvi wa kutumia zana duni.

2. Candid Scope

Candid Scope JF-Expert Member

#2
Jul 8, 2011
Joined: Nov 8, 2010
Messages: 11,896
Likes Received: 119
Trophy Points: 160

NI nchi chache duniani zinazoweza kuwa na jiografia nzuri kama Tanzania, halafu ziwe dhaifu katika matumizi ya jiografia hiyo katika kujiendeleza.

Tanzania ina ufukwe wa bahari upatao kilometa 1,424 na ndani yake kuna bandari za Tanga, Dar es Salaam, Mtwara na Zanzibar kwa upande wa Mashariki. Upande wa kaskazini, kaskazini magharibi, magharibi na kusini magharibi, inapakana na nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia na Malawi. Haya yote ni mataifa ambayo hayakujaliwa milango ya bahari, hivyo ni tegemezi kwa mataifa ya Tanzania, Kenya, na Msumbiji, kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa zao. Tanzania ina fursa kubwa zaidi kuliko nchi nyingine nilizozitaja. Miongoni mwa nchi hizi tatu – yaani Tanzania, Kenya na Msumbiji, Tanzania ina nafasi ya kipekee kabisa. Ni tofauti na Kenya, ambayo inapakana na nchi moja tu isiyokuwa na bandari ambayo ni Uganda.

Pia, ni tofauti na Msumbiji, ambayo inapakana na nchi zisizokuwa na bandari za Swaziland, Zimbabwe na Malawi. Tanzania inayopakana na mataifa sita yasiyo na bandari. Hii ina maana kwamba bandari za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara ni maeneo ambayo yalitakiwa kuwa na pilikapilika nyingi katika harakati za usafirishaji wa bidhaa zinazoingia na kutoka katika nchi hizi za jirani. Bandari hizi zilitakiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ajira na cha mapato ya nchi, lakini kwa bahati mbaya haiko hivyo, kwani zimekuwa zikisuasua miaka nenda miaka rudi. Tukiachana na bandari zilizo katika mwambao mwa bahari ya Hindi, pia nchi yetu ina bandari katika maziwa kama vile bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo katika Ziwa Victoria, bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika na Bandari ya Mbamba Bay katika mwambao wa Ziwa Nyasa.

Kabla ya kuendelea ni vyema nikakujuza mpendwa msomaji, kuwa lengo la makala haya si kuzungumzia bandari pekee, bali nimeanza kwa utangulizi huo kwa kuwa baada ya kufika Mbamba Bay, nilijiuliza maswali mengi kwamba kwa nini fursa hiyo haitumiki kuendeleza eneo hilo kupitia shughuli za kiuchumi, badala yake eneo hilo limeendelea kubaki katika umasikini wa kupindukia. Tofauti na bandari zilizopo katika mwambao mwa Ziwa Victoria na bandari ya Kigoma, bandari ya Mbamba Bay imeachwa mbali katika suala zima la utoaji huduma, kwani haina mchango mkubwa wa kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine ya jirani. Bandari imekuwa ikisaidia kusafirisha abiria waishio katika maeneo yaliyopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. Maeneo haya ni pamoja na Lupingu, Manda, Mbamba Bay na sehemu kadhaa zilizopo mwambao mwa ziwa hilo.

Wasafiri wa eneo hilo wamekuwa wakitumia meli ya mv Songea, ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Kyela mkoani Mbeya hadi Mbamba Bay na kisha kuelekea Nkhata Bay katika nchi jirani ya Malawi. Tofauti na wengi wanavyodhani, kuwapo kwa meli hii katika eneo hilo, hakusaidii sana kuinua shughuli za kiuchumi zinazoweza kuchangamsha eneo hilo, badala yake maisha ya wananchi yameendelea kuwa duni. Mbamba Bay haionekani kuwa eneo lenye maendeleo ya kasi, badala yake limeendelea kuonekana kama mji wa kihistoria. Mji uliojaa majengo ya zamani ya wenyeji, yaani mchanganyiko wa makabila ya Wamanda, Wanyasa na Wamatengo kutoka maeneo ya milimani.

Kwa ambao hawajawahi kufika Mbamba Bay, niwafahamishe kuwa wakazi wa eneo hili hawakupaswa kuwa masikini, kwa kuwa ni eneo lenye neema kubwa, ya kuwa moja ya maeneo maarufu kwa shughuli za utalii na pilika pilika nyingine za kiuchumi. Ukiwa umbali wa kilometa kumi hivi, eneo la milimani karibu ya kufika eneo hili, unaweza kujionea mandhari tulivu na kufaidi upepo mwanana, unaovuma kutoka katika ziwa Nyasa, lililojizamisha katika ya bonde la ufa. Sio siri, mandhari ya eneo hilo hasa maeneo ya mwambao ni ya aina yake, kwani eneo hili limejaliwa fukwe safi na maji ya ziwa ambayo hayajachafuliwa, tofauti na maeneo mengine kama hayo ambayo niliwahi kuyatembelea. Ukweli ni kwamba iwapo serikali ikijipanga vyema kuhamasisha utalii katika eneo hilo, watalii lukuki watamiminika katika eneo hilo.

Tofauti na maeneo mengine nchini, yenye mchanganyiko mkubwa wa watu, wakazi wa Mbamba Bay wanaonekana labda kutokana na mazoea, fukwe nzuri walizonazo hawazioni kama fursa muhimu. Baadhi ya wenyeji niliozungumza nao, wanasema kuwa hawana utamaduni wa kutembelea ufukoni kwa ajili ya kupunga upepo na kufurahia mandhari ya eneo hilo, kwa kuwa mazingira hayo wameyazoea. Wanasema kuwa wamekuwa wakienda katika eneo hilo kwa shughuli mbalimbali, kama vile kufua nguo, kuoga au kununua samaki kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki kienyeji, yaani kwa kutumia mitumbwi midogo na ndoano.

Alex Komba ni mkazi wa eneo hilo, ambaye anasema kuwa kwa wenyeji wa eneo hilo suala la mandhari nzuri ya eneo hilo, si lolote si chochote, kwa kuwa wameizoea, ndio maana maeneo ya ufukweni yanauzwa bei rahisi, sawa na maeneo mengine. “Hapa ukija na laki tatu au nne, unapata kiwanja mara moja, tena ukiwa na milioni moja na nusu au mbili, unaweza kumhamisha mtu katika kibanda chake. Unadhani watu wa hapa wanababaishwa na haya maji?

Kama vipi toa fedha nikutafutie eneo,” anaeleza Komba. Wakieleza sababu ya eneo hilo kudumaa kimaendeleo, wanasema kuwa ubovu wa barabara na mawasiliano hafifu ya redio na simu ni miongoni mwa sababu ambazo zinazokwamisha maendeleo ya eneo hilo. Margareth Nchimbi ni mama ntilie anayefanya biashara hiyo Mbamba Bay, ambaye anaeleza kuwa hadi sasa katika eneo hilo, hakuna mawasiliano ya redio za hapa nchini, badala yake wamekuwa wakisikiliza Redio Malawi. Kwa upande wa simu, anasema kuwa kwa miaka mingi eneo hilo hakikuwa na mawasiliano ya simu, jambo ambalo lilikuwa likikwamisha shughuli za kibiashara na maendeleo yao.

Lakini, hali ni tofauti kwa sasa, ambapo huduma za mawasiliano zimeanza kuboreka baada ya baadhi ya kampuni za simu, kusimika minara ya mawasiliano katika eneo hilo. Hali ya eneo hilo kuwa duni, imeendelea kutowavutia wawekezaji kutoka maeneo mengine nchini, hivyo wakazi wake wanaendelea na shughuli yao kuu ya uvuvi wa kutumia zana duni.

3. Kichuguu

Kichuguu Platinum Member

#3
Jul 8, 2011
Joined: Oct 11, 2006
Messages: 7,202
Likes Received: 863
Trophy Points: 280
Tmelaaniwa au tumejilaani. Godfrey Mwakikagile katika vitabu vyake huwa anaainisha waziwazi kuwa Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania tuna bahati mbaya ya kuwa na viongozi wabovu miaka yote tagu tumepata uhuru.

4. Nyambala

Nyambala JF-Expert Member

#4
Jul 8, 2011
Joined: Oct 10, 2007
Messages: 4,470
Likes Received: 21
Trophy Points: 135
[​IMG]

Just imagine hii picha tu ni hela!!!! What's wrong with us?

5. M

Mbopo JF-Expert Member

#5
Jul 8, 2011
Joined: Jan 29, 2008
Messages: 2,532
Likes Received: 8
Trophy Points: 0
Nachukia wabunge kusinzia bungeni na kushindwa kuchangia mijadala yenye umuhimu mkubwa katika maendeleo ya nchi. Ni usaliti pia kwa sababu wametumwa na wapiga kura wao kuja kutekeleza legislative ajenda kwa niaba yao.

Lakini kudhani kwamba kutosinzia peke yake ndiyo muarobaini wa matatizo yetu, au kudhani kwamba abunge ambao macho yao makavu pale bungeni wana mchango mkubwa katika kuondoa kero za wapiga kura wao ni kujidanganya na pengine kutofahamu ni kwa kiasi gani tatizo la wabunge wetu ni kubwa. Hata wale wanaoongea sana na wenyewe wamebaki kuwa mashujaa katika ngazi ya kitaifa wakati huko kwenye majimbo yao hali inazidi kuwa mbaya. Overhaul ya mfumo wa kupata wawakilishi ni miongoni mwa mambo ambayo yanaweza kuleta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo yetu.

6. C

CLEMENCY JF-Expert Member

#6
Jul 8, 2011
Joined: Feb 4, 2008
Messages: 211
Likes Received: 10
Trophy Points: 35
Mkuu,amekunywa dawa za mafua toka ile zahanati ya Bunge.............

7. Mamndenyi

Mamndenyi JF-Expert Member

#7
Jul 8, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 29,060
Likes Received: 6,507
Trophy Points: 280
nimepita hapa.

8. F

FJM JF-Expert Member

#8
Jul 8, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
With all due respect, OBESE inamfanya mtu kulala mara kwa mara. Badala ya Mh Wasira kung'aka angechukulia mjadala wa picha yake ya kulala kama changamoto. Najua sio kazi rais kupunguza uzito lakini for his own good na hata Captain Komba wajitahidi kupunguza kilo.

9. Mwanamageuko

Mwanamageuko JF-Expert Member

#9
Jul 8, 2011
Joined: Oct 31, 2010
Messages: 3,796
Likes Received: 1,294
Trophy Points: 280
TATIZO LA USINGIZI WA WABUNGE WETU HUSUSAN WALE 'MATUNYENYE" Hawazingatii afya zao hasa ratiba za kula na wale nini!
Pale nyuma ya jengo la bunge kuna kila aina ya "choma na chemsha" achlia mbali mibaniko...sasa waheshimiwa sana na wapambe wao wakifika pale wanakula kana kwamba wanakwenda jangwa la ethiopia hawatokula tena!! Huo ni ULAFI WA CHAKULA sasa jiulize ikiwa ndivo je UCHU WA MALI NA MADARAKA UKOJE HAPO?

Lazima wachape usingizi WABUNGE WETU! Kwani baada ya kampeni za uchaguzi hawana mawazo tena wala changamoto!
Labda wanalala kufidia usingizi ambao walipoteza nyakati za kampeni na uchaguzi!!?
Mbunge kulala bungeni!!!!!!????????????????????????????????????????????
Mmeshawauliza huwa wanakesha wapi?????????????????? au wanafanya kazi zipi usiku????????????????????????????????
Ikiwa mbunge analala bungeni mnatarajia atoe mchango upi?????

Hivi mmesahau kwamba Watanzania anapenda sana starehe? waliona viti vile vya kizamani vinawakosesha raha wakataka vya kunesa na kuzunguuka!! Ili wachape usingizi wao vema (WAWE NA NDOTO ZA MAFANIKIO NA MAISHA BORA KWA WATU WAO!) Tazameni hata lile bunge la mabwanyenye wa kiingereza hawana viti kama vile!!! Lakini sisi.... Maskini wa fikra matajiri wa kujifaharisha!!!

Nadhani vema sasa bungeni nako kuanzishwe ule utaratibu kama wa mashuleni zamani... RUKA RUKA RUKA SIMAMA KAAA!!!

10. nngu007

nngu007 JF-Expert Member

#10
Jul 8, 2011
Joined: Aug 2, 2010
Messages: 15,871
Likes Received: 56
Trophy Points: 145
kenya inapakana na south sudan, ethiopia na uganda ambazo zote hazina bahari na sio uganda pekee; kwa upande wetu wa tanzania ni uganda, rwanda, burundi malawi na zambia ni nchi tano na sio sita usemazo kwahiyo tafadhali verify inforamtion zako kabla ya kutoa habari --- jamii forum yetu lazima iwe ya ukweli

11. Candid Scope

Candid Scope JF-Expert Member

#11
Jul 8, 2011
Joined: Nov 8, 2010
Messages: 11,896
Likes Received: 119
Trophy Points: 160
Hoja hapa utajiri asilia wa nchi yetu ikiwemo madhari nzuri kama hi ya Mbambabay ambayo hata siku moja sijamsikia Captain Kombo akiongelea bungeni namna gani angependekeza sehemu hii iendelezwe ikiwa kama kiungo kizuri na Malawi.

12. Juaangavu

Juaangavu JF-Expert Member

#12
Jul 8, 2011
Joined: Nov 3, 2009
Messages: 915
Likes Received: 14
Trophy Points: 35
Nafikiri wanakuwa wanatafakari jinsi watakavyogawa zile posho zao kwa wapiga kura wao, tehe tehe teheee; wengine wanakuwa wanatakafari hoja watakazochangia siku inayofuata; nk. nk.

13. Candid Scope

Candid Scope JF-Expert Member

#13
Jul 8, 2011
Joined: Nov 8, 2010
Messages: 11,896
Likes Received: 119
Trophy Points: 160
Mbambabay ni ukingoni kabisa kwenye kona ya Tanzania, Msumbiji na Malawi. Kwa upande wa Tanzania, Mbam abay ina nafasi ya kukua na kuwa mji mkubwa wa biashara kutokana na historia yake na pia kiungo cha biashara kati ya nchi tatu hizi.
Labda itachangamka sasa Wachina wanapokusudia kujenga reli ya Mtwara -Mchuchuma - Mbambabay kuwa kiunganishi na Malawi, kutokana na mradi wa Mawe na chuma katika eneo la Mkoa mpya wa Njombe na mkoa wa Ruvuma.

Loading...