Mbunge Kingu: Askofu Gwajima alidhamiria kuchonganisha Serikali na Wananchi

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
53,713
2,000
Mbunge Elibariki Kingu amesema kwa mujibu wa Uchambuzi wake, Askofu Josephat Gwajima alidhamiria kuichonganisha Serikali na Wananchi ili watu wakose imani nayo

"Kitendo cha Gwajima kujitokea hadharani na kuwaambia Watanzania Chanjo mnayokwenda kuchanjwa haijafanyiwa Utafiti, adhabu zisiishie hapo. Hata Halima Mdee hajawahi kutufanyia vitimbi vya namna hii"

Amesema anashangaa kwanini Chama cha Mapinduzi (CCM) haijachukua hatua dhidi ya Askofu Gwajima
Acha wauane hawa wapuuzi
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,588
2,000
Pamoja na gwajima kuwa layman kwenye maswala hayo ya chanjo, bado kuna mambo yenye kizungumkuti kwenye kutumia vinasaba kwenye maswala ya tiba na chanjo hasa wakitokea watu waka misuse technology na kuanza ku-edit vinasaba vya asili vya binadamu na kupelekea kuzaliwa watu wenye tabia, mienendo na maumbile ambayo ni tofauti na binadamu wa kawaida. Haya tumeshayashuhudia kwenye viumbe vingine kama mazao ya GMO kama mahindi......juzi hapa nimesikia India wanataka kutengeneza chanjo ya covid kwa kutumia DNA, yaani wanaiita DNA vaccine, ni katika mwendelezo ule ule wa kuingilia mfumo wa vinasaba vya binadamu.......ambavyo kimsingi ndo vinaamua tabia, mienendo, maumbile na mifumo yote inayomfanya binadamu aweze kuishi.
 

ielewemitaa

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
5,482
2,000
Je nini wapenda chanjo mna ushahidi wa utafiti wa madhara ya hiyo chanjo??? Wewe na wenzako kwa sababu mlikuwa na chuki binafsi na Magufuli ndiyo maana kila linaloenda kinyume na Magufuli mnalibeba bila kutumia akili.
Wataalamu waliounda tume ya Rais kutafiti chanjo wameruhusu pasi na shaka kuwa chanjo inafaa , na Rais akapigwa chanjo, halafu anatokea mtu amekula maharage anasema watu wamepewa pesa, akiambiwa athibitishe hawezi sasa unataka achekewe tuuu haipo
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,337
2,000
Mbona wanahangaika Gwajima alishawaambia yupo tayari kwa lolote si mfukuzeni.
Kama mnaunga mkono hoja mchanjwe wabunge wote na msifupishe hivyo vipindi si mtakuwa salama.

Wabunge njaa Kama huyu hovyo kabisa,anataka kujulikana kupitia mgongo wa Gwajima.
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,337
2,000
H
Hoja zenyewe haziko kitaalam ,atjibiwaje kitaalam
Anauliza hi chanjo inaweza kumkinga mtu kwa muda gani?
Tujibu wewe mtaalamu.

Anauliza kwanini mtu lazima ajaze consent form kabla ya chanjo wakati chanjo zote hatukuwahi kujaza consent form Kama za yellow fever,tetanus, typhoid nk.

Tujibu wewe mtaalamu Ili tuachane na huyu jamaa.
 

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
45,195
2,000
kopo langu la popcorn limejaa na mirinda nyeusi bariiidi pembeni nashuhudia mpambano tu...
 

real life skills

Senior Member
Jul 16, 2021
189
250

Mbunge Elibariki Kingu amesema kwa mujibu wa Uchambuzi wake, Askofu Josephat Gwajima alidhamiria kuichonganisha Serikali na Wananchi ili watu wakose imani nayo.

"Kitendo cha Gwajima kujitokea hadharani na kuwaambia Watanzania Chanjo mnayokwenda kuchanjwa haijafanyiwa Utafiti, adhabu zisiishie hapo. Hata Halima Mdee hajawahi kutufanyia vitimbi vya namna hii".

Amesema anashangaa kwanini Chama cha Mapinduzi (CCM) haijachukua hatua dhidi ya Askofu Gwajima.
 

real life skills

Senior Member
Jul 16, 2021
189
250
Pumba kabisa. Mama Samia atakuwa anawazoom tu. Gwajima kasema chanjo ni ya majaribio na hata Magufuli alishaonya, then huyu mbunge msaka tonge anadhani atateuliwa anaongea pumba
Utakuwa unasumbuliwa chuki binafsi kwa serikali ya raisi Samia.

Kingu ameongea vizuri mno!
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
8,364
2,000
Utakuwa unasumbuliwa chuki binafsi kwa serikali ya raisi Samia.

Kingu ameongea vizuri mno!
Mimi mama Samia nampenda sana tena sana, na kwa taarifa yako namuunga mkono kwa 100%. Hata yeye anawawashangaa wabunge walivyo mbumbu kwa kumhukumu Gwajima.
 

kamdudu

JF-Expert Member
Jan 20, 2015
1,176
2,000
hawa wachumia tumbo ndio wameifikisha Nchi hapa ...

kamchukulie hatua wewe sasa maana sisi Raia tunamuelewa sana tu
 

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
5,087
2,000
Pumba kabisa. Mama Samia atakuwa anawazoom tu. Gwajima kasema chanjo ni ya majaribio na hata Magufuli alishaonya, then huyu mbunge msaka tonge anadhani atateuliwa anaongea pumba
Hajawahi kuteuliwa, sijui ana mkosi gani. Kazi yake kuuza sura kahawa pale na sendoz zake za plastic. 😀

Labda this time atakumbukwa.
 

E oxygen

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
326
250

Mbunge Elibariki Kingu amesema kwa mujibu wa Uchambuzi wake, Askofu Josephat Gwajima alidhamiria kuichonganisha Serikali na Wananchi ili watu wakose imani nayo.

"Kitendo cha Gwajima kujitokea hadharani na kuwaambia Watanzania Chanjo mnayokwenda kuchanjwa haijafanyiwa Utafiti, adhabu zisiishie hapo. Hata Halima Mdee hajawahi kutufanyia vitimbi vya namna hii".

Amesema anashangaa kwanini Chama cha Mapinduzi (CCM) haijachukua hatua dhidi ya Askofu Gwajima.
Tangu hisa za shirika la ndege tz kupikwa kwa namna ile mwaka juzi na mkaguzi kuja kulibumbulua kwenye tarifa yake je wanatofautiana vipi na kajima.
 

papaayenga

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
765
500
Wajibu kitaalamu hoja za Gwajima na siyo kuleta mipasho

Gwajima hana hoja yeyote zaidi ya uchale chaplin na hata hao walio mweka kikao nao wanachekesha na kupoteza muda pia mfumo kristo na mfumo ccm ndio ulio muokoa gwajima kufikishwa mahakani kujibu tuhuma kutokana na ule upuuzi aliokua anawalisha kondoo wake waliopotea pale kigangoni mwake.
 

Gift mzalendo

Senior Member
Dec 13, 2019
146
250
Anauliza hi chanjo inaweza kumkinga mtu kwa muda gani?
Tujibu wewe mtaalamu.

Anauliza kwanini mtu lazima ajaze consent form kabla ya chanjo wakati chanjo zote hatukuwahi kujaza consent form Kama za yellow fever,tetanus, typhoid nk.

Tujibu wewe mtaalamu Ili tuachane na huyu jamaa.
Inategemea na aina ya chanjo kuna chanjo kama za hepatitis unachoma zaidi ya mara moja baada ya hapo huhitaji tena kuchanjwa
Na hizi za Corona zipo ambazo unachomwa mara huhitaji kuchanjwa tena
So inategemea na aina ya chanjo husika ilivyotengenezwa
Consert fomu haijaanza leo kwenye ishu za afya ipo na ni kawaida mtu kuridhia kilahuduma unayompa kwanza. Ingawa kuna procedure ambazo ni lazima, Na hakuna consert form inayosaniwa na serikali kama muhusika yuko kwenye hali mbaya anaweza kusai iwa na ndugu wa karibu
Sayansi inazidi kukua na tecklogia inazidi kukua kila siku tusikariri
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom