Mbunge Kigwangalla Afunga Mgodi wa Isungangwanda kwa Nguvu ya Umma! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Kigwangalla Afunga Mgodi wa Isungangwanda kwa Nguvu ya Umma!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zulqarnayn, Oct 20, 2011.

 1. Z

  Zulqarnayn Senior Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WanaJF nimeikuta hii kule Wanabidii,
  Naona Mbunge Kigwangalla sasa ameanza kufanya kweli, Resolute nao wakae sawa sasa!


  Wananchi wa Kijiji cha Mwabangu ambao wamedhulumiwa haki ya kumiliki mgodi wao maarufu kama 'Isunga Ngwanda' waliokuwa wakiumiliki toka Mwaka 1987 na kila mara wakikata na kulipia leseni mpya. Mkataba wa kwanza ulikuwa baina ya Mmbando and Partners na Kijiji cha Kilabili/Mwabangu, ambao walikiuka masharti na kuacha kulipia ushuru wa kijiji na kijiji kikaamua kuuvunja mkataba huo. Watu hao walijipanga upya na kuamua kwa njia za hila kwenda kubadilisha jina la kampuni na kuchukua leseni yao (PML) kwenye kitalu kile kile kwa njia ya ulaghai na kujiita jina jipya la Rebman Damson Tarimo and partners na kuja kuanzisha mgodi wao na kuwafukuza wachimbaji wadogo wadogo na baadaye kuanza kuwachaji wanakijiji ushuru wa kuingia kuchimba

  Mkuu wa Wilaya mwezi wa kwanza aliamua kusitisha uchimbaji katika eneo hili mpaka ufumbuzi utakapopatikana, wananchi walitii agizo hili lakini Rebman na wenzake waliendeleza uchimbaji, hali iliyofanya wanakijiji kukasirika na sasa kuamua kuweka ulinzi wao na kuwaondoa wawekezaji hao

  Mbunge wa Nzega Dkt. Kigwangalla, akiambatana na diwani wa kata ya Nata Mhe. Joseph Malongo wameungana na wananchi kwenye eneo hili la mgodi ili kuzuia dhulma hii kwa nguvu za umma!

  Wananchi zaidi ya 1500 wamekusanyika hapa na mpaka sasa hivi wameshafanikisha kuzuia uchimbaji kwenye maduara yote matatu!
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  all the best hon.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hivi huu ndio ule mgodi alikuwa anasema Kingwangallah kwamba ataandamana? I thought ni Resolute?
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  safi sana wananchi wenzetu kwa mshikamano wenu huo. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  kakosa kazi, kwa ilani hipi anatumia nguvu za umma? watamwaga utumbo asubuhi tu kwa kukwapua kadi yao ya chama
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,275
  Trophy Points: 280
  People power!!
   
 7. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  aende akafunge resolute kama kweli ana gats. Aache danganya toto.yeye alisema resolute sasa leo kaanzia wapi tena.
   
 8. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  He has set an example and proved to walk the talk unlike his irresolute counterparts like Zitto and the like whose aggressiveness can easily be extinguished by money. Zitto, once notable anti-graft crusader has turned out to be Barrick's policies espouser only after being baksheeshed a handsome sum.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,204
  Trophy Points: 280
  Kama habari hii ya kweli basi anahitaji pongezi za dhati kabisa. Hongera Mkuu na usimamie pia kuhakikisha migodi yote nchini inafungwa hadi hapo kutakapokuwa na mikataba ambayo inainufaisha nchi, vinginevyo uchimbaji wa rasimali zetu usimamishwe mara moja.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Madai mazito haya una ushahidi kaka ?
   
 11. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  huyo anajipendekeza kwa wananchi.juz juz alikuwa Bukene akimpiga tafu mbunge wa bukene kwenye zile fainal za kumbe la mbunge.hawana jipya wizi mtupu.
   
 12. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huko hakuna mgodi, nisehemu ya wa chimbaji wadogo wadogo, kama ana ubavu kweli aje resolute tuone. Hana lolote huyo, hayo maduara ndo anaita migodi anatafuta umaaru.
   
 13. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Gamba limeota tena? Au wamekulipa mshiko wako? I knew u were a phony!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wamefunga huo mgodi kwasbabu ni rahisi kumbana mmatumbi kuliko mzungu

  kama wana uwezo wakafunge migodi inayonyonya wabongo
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hajafunga mgodi.......... wananchi wamefunga mgodi, yeye alifika kuondoa jazba, na aliyeneemeka kwa ujio wake na wa wanausalama ni huyo mwekezaji. unadhani angekua mgeni si huyo mbunge na wananchi wote wanguwekwa ndani?

  wabongo aisee...............
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,204
  Trophy Points: 280
  Kumbee...ndio maana imekuwa rahisi kuufunga.

   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mgodi au kamgodi?? waende migodini waone basi kama hujasikia hata Muzee ya madigirii ya kupachika hajaenda mwenyewe hata kwa miguu
   
 18. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hili ndiyo tatizo la siasa za Waafrika, kufikiri kuwa kama upo upinzani basi uchekelee kila kitu.
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Si afadhali ajipendekeze kwa wananchi kuliko kwa hao wawekezaji uchwara. Kumpiga tafu yeyote hiyo ni biashara tafauti

   
 20. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hii safi. Aungwe mkono Sio kubezwa. Tabia za kubeza ndizo hukatisha tamaa viongozi jasiri na kusababisha warudi nyuma.
   
Loading...