Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,682
- 1,234
MBUNGE JACQUELINE KAINJA AGAWA MASHUKA NA NETI ZAHANATI YA KATUNDA, WILAYA YA UYUI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja Tarehe 09/07/2024 nimefanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Mabama Kijiji cha Katunda ndani ya Wilaya ya Uyui Jimbo la Uyui Kaskazini.
Mhe. Jacqueline Kainja ametembelea Zahanati ya Kijiji cha Katunda ambayo imekamilika na imeanza kufanya kazi na kuwakumbusha wananchi wa Kijiji cha Katunda kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Jacqueline Kainja amewakumbusha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi huku akiwakumbusha wananchi muda ukifika wa kupiga kura wenyeviti wote wa vitongoji watoke CCM lakini vilevile kuheshimisha Mkoa wa Tabora kuendelea kuwa ngome ya CCM daima
Jacqueline Kainja amewaeleza kazi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wabunge wa majimbo, Wabunge wa Viti maalumu, Madiwani wa Kata na madiwani wa Viti maalumu na alipata muda wa kusikiliza ushauri kutoka kwa wananchi.