Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mhe.Kishimba amejenga hoja bungeni kuhusu umuhimu wa kutumia bangi Kama zao la biashara tofauti na Sasa linavyopigwa marufuku.

Amedai gunia la bangi kwa Sasa hapa Tanzania linanunuliwa kwa milioni nne wakati Zimbabwe linanunuliwa kwa dola elfu saba ambazo ni karibia milioni ishiria za Tanzania.

Amewataka wabunge na wananchi wafahamu kuwa dawa za usingizi zinatokana kwa kiasi kikubwa na bangi.

Amehoji Kama japani wanatumia bangi kwa kuvuta na bishara kwanini sisi tusikubali kuruhusu usafirishaji na ulimaji wa bangi.

Bangi soon inakuwa bidhaa halali

UPDATE:

Kishimba tena - Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba ataka waliolima Bangi waruhusiwe kuiuza
 
Iruhusiwe ni jambo zuri, lakini iwe katika ushirika yan watu binafsi (mmoja mmoja) asiruhusiwe kulima Bali vikundi na kazi hii wapewe vijana wasio na ajira fresh from college hasa wale wa kilimo waifanye hii kazi...

Pia iundwe board ya bangi Kama ilivyo kwa pamba, tobacco etc
 
Sasa kama mpaka sasa inavutwa,si bora iruhusiwe ili iwe rahisi kumdhibiti mvutaji.
inavutwa na wachache na impact inakuwa ndogo.
Ikiruhusiwa itavutwa kuanzia mtoto mdogo anayevuta majani ya mpapai hadi baba yake,
mwanafunzi hadi mwalimu.
kwa sasa mwalimu mmoja kati ya 30 anaweza kuwa anapuliza. Wanafunzi 10 kati ya 100 wanaweza kuwa wanapuliza pia. Ila ukifanya virzeversa kwa kuhalalisha badala ya kuongeza juhudi za kuharamisha kazi itakuwa ngumu kupindukia.
 
ikikamilika bangi, na akili zetu zikawa arosto ushoga utafuata bila kupingwa.
Sio Lazima kuiga kila kitu. Kama tumeona madhara ya Bangi Live kwa jamii na vijana kwa nini tujihatalishe kwa kutaka kuiga maamuzi ya wazungu na Maabara zao feki.
Binafsi natumia bangi, heroin, cocaine and co. Nipo Straight, Nina afya na utimamu wa akili na mwili.

Tatizo kwa hao ni nini?
 
ikikamilika bangi, na akili zetu zikawa arosto ushoga utafuata bila kupingwa.
Sio Lazima kuiga kila kitu. Kama tumeona madhara ya Bangi Live kwa jamii na vijana kwa nini tujihatalishe kwa kutaka kuiga maamuzi ya wazungu na Maabara zao feki.
Wenye maabara feki ndo hao wanakuletea Kila aina ya pills na wewe ukiumwa unakimbilia kumeza hizo dawa.
 
Back
Top Bottom