Mbunge JUMA NKAMIA aonja joto ya jiwe

yani hata mm nimefurahi maana waandishi wengine wakijiona wanatangaza kwenye vituo vikubwa basi wanajiona wao ni wao na kuleta midomo ya utafikiri wametiwa morta mdomoni kumbe loo bora amefyatuliwa sasa naona atatulia na kutuliaza likichwa chake chini
Aliyekuwa mtangazaji wa TBC radio bwana Juma Nkamia amefyata mkia baada ya kurushiwa kombora la skadi huko jijini mwanza na aliyekuwa Mkuu wa BBC Swahili Tido Mhando.

Bwana Juma Nkamia alikuwa akivisakama vyombo vya habari na waandishi wenzake akiwaita makanjanja, baadhi ya media alizozisakama sana ni pamoja na Jamii Forum, kwa kujiona yeye ni mwandishi maarufu na aliwahi kiajiriwa BBC Swahili.

Sasa tangu bwana Tido amtupie dongo kali kuwa hajawahi kuajiriwa kazi BBC bali alikuwa ameenda kwa mafunzo na alikuwa akipewa kusoma taarifa ya habari tu kama sehemu ya masomo mheshimiwa huyu hajawahi kujibu tuhuma hizo wala kurudia kuvisakama vyombo vya habari tena.

Jamaa kashushuliwa hadi moyo wangu umesuuzika maanake alikuwa anajitutumua sijui alikuwa anatafuta uwaziri wa habari na utangazaji.

Mheshimiwa umebugi men.
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom