Mbunge Joshua Nassari anusurika kupigwa na wananchi wa eneo hilo la Usariver

Dah nilikuwa sijaangalia tarehe na mwaka wa Post hii.! kumbe B7 ilikuwa haijasajiliwa vizuri!
 
View attachment 69499

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru, mashariki, Joshua Nasari amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi ambao walichukizwa na kitendo chake cha kuhamasisha wafuasi wa Chama chake, CHADEMA, kuwashambulia wanachama wa CCM na kumjeruhi Katibu kata wa CCM, kata ya Usariver, baada ya kuzuiliwa asifanye kampeni za uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji katika mji mdogo wa Usariver kabla ya wakati.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO, amesema katika vurugu hizo zilizotokea katika eneo hilo la Usariver, katibu wa kata ya Kisambare wa Chama cha mapinduzi, alijeruhiwa kichwani mdomo na mkono ambapo amefungua jalada kituo kikuu cha polidsi wilayani Arumeru, USRIVER/RB 4397 /2012.

Ammesema chanzo cha tukio hilo ni mbunge huyo kuanza kupita nyumba hadi nyumba na kwenye vilaub vya pombe za kiasili na kuwanunulia pombe akihamasisha wananchi kukichagua Chama chake kabla ya muda wa kampeni haujaanza.

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema mara baada ya kumuona ameanza kampeni kabla ya wakati, walimfuata na kumtaka asubiri muda ufike ndipo aanze kampeni, hatua iliyosababisha kuwaamrisha wafuasi wake ambao walikuwa zaidi ya kumi kuwashambulia wanachama wa CCM waliokuwa watano.

Katibu Akyoo amesema kufuatia vurugu hizo wananchi, walimzingira Mbunge hyo na wafuasi wake ambapo mbunge huyo baada ya kuona wananchi wamekusanyika kwa nia ya kumpiga, aliingia ndani ya gari lake na kutokomea akiwaacha wananchi waliokerwa.

Katibu wa kata wa Usariver, Edmund Milanzi, akizungumzia tukio hilo amesema alishambuliwa na wafuasi wa CHADEMA baada kumtaka Mbunge huyo kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati na ndipo ghafla alishitukia anapigwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walimjeruhi kichwani, mdomoni na mkononi.

Baada ya kushabuliwa amesema alikwenda Kituo Kikuu cha polidsi wilayani Arumeru kilichopo kwenye mji mdogo wa Usariver na kufungua jalada la kushabuliwa na kujeruhiwa na hivyo kuweza kwenda hospitalini kupata matibabu.

Hii taarifa ni ya kuchonga kwa mjibu wa Rb ya polisi tukio liliripotiwa mwaka2012 mwaka ambao tukio lilitendeka imekuwaje hizi taarifa zikaletwa sasa?.Au ndiyo kusema kuwa zilikuwa jikoni kuivishwa?.Halafu hili tukio limepelekwa polisi ambao wanawajibika kuthibitisha hilo tukio inakuwaje katibu wa CCM ndie awe muthibitishaji?.
 
Nassari ukirudia tena Mara ya tatu jambo baya litakutokea, chukua tahadhali.
 
Privatus Karugendo

Wapendwa sherehe za Mzee Pius Ngeze, kutimiza
miaka 70, zimefana. Tulianza kwa Ibada ya Misa,
Iliyoongozwa na Mhashamu Askofu Medhodius
Kilaini, Kanisa Kuu la Bukoba, baadaye jioni
sherehe ya kumpongeza na kuzindukia kitabu juu
ya maisha yake. Kwa taarifa zaidi tembelea
mtandao wa Bukobawadau, na JAMCO Bukoba
Blog.

Jumapili njema,

Padri Privatus Karugendo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom