Mbunge Joshua Nassari anusurika kupigwa na wananchi wa eneo hilo la Usariver

huyu dogo nae vipi kama ni kweli amewahamasisha kufanya ivo amefanya kosa, yabid awekwe chini akaangwe.
anahitaji awe na busara tumechoka na vurugu za hapa na pale tunategemea watu wa chadema kuwa na busara na kuact kwa busara
acha uhuni dogo
Jifunze kutumia ubongo wako sawasawa na sio kupayukapayuka na kutoa mapovu.

Jifunze kutofautisha kati ya propaganda na ukweli kabla ya kutoa maoni yako.

Hii ni full propaganda, ni sawa na mtu aje humu JF na kudai JK kakamatwa akiiba kuku
huko Bagamoyo na wewe uanze kuropoka na kushauri kuwa achomwe moto.
 
Uchaguzi wa 2010 JK alifanya kampeni hadi usiku! Sharobaro mmoja akasema, 'Jiografia ya huko inaruhusu'. Nami nasema Physics ya Arumeru inaruhusu
 
huyu dogo nae vipi kama ni kweli amewahamasisha kufanya ivo amefanya kosa, yabid awekwe chini akaangwe.
anahitaji awe na busara tumechoka na vurugu za hapa na pale tunategemea watu wa chadema kuwa na busara na kuact kwa busara
acha uhuni dogo

mkuu umeisoma hii post vizuri..?au uongo wa huyu gamba umekunasa....kwa jinsi post ilivyo hakuna great thinker yeyote anaeweza kuamini habari hii.
 
Tulioko huku mbona hakuna hicho kitu wala tetesi acheni uwongo kwanza ccm hawawezi kuwafuata chadema kwani ccm huku imekufa.
 
infact sikumaanisha achomwe moto, nimetumia tu lugha picha pili ushaui wangu kwa viongozi wote kuact kwa busara ikiwamo Nasari mheshimiwa sidhani kama nilisema neno baya
 
Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

fikiri kwanza kabla ya kuandika, kampeni za wapi zinaanza 28 Octoba ...@#%$#!!!???
 
Nipo usa river nilifika jana kufuatilia cheti cha kuzaliwa. Nimefikia hotel moja inaitwa ivory na jana nimezunguka sana hapa usa river kuwacheki marafiki zangu wa kitambo. Hizo habari umetengeneza ndugu! Tiiya Uresi mbee!
 
View attachment 69499

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru, mashariki, Joshua Nasari amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi ambao walichukizwa na kitendo chake cha kuhamasisha wafuasi wa Chama chake, CHADEMA, kuwashambulia wanachama wa CCM na kumjeruhi Katibu kata wa CCM, kata ya Usariver, baada ya kuzuiliwa asifanye kampeni za uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji katika mji mdogo wa Usariver kabla ya wakati.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO, amesema katika vurugu hizo zilizotokea katika eneo hilo la Usariver, katibu wa kata ya Kisambare wa Chama cha mapinduzi, alijeruhiwa kichwani mdomo na mkono ambapo amefungua jalada kituo kikuu cha polidsi wilayani Arumeru, USRIVER/RB 4397 /2012.

Ammesema chanzo cha tukio hilo ni mbunge huyo kuanza kupita nyumba hadi nyumba na kwenye vilaub vya pombe za kiasili na kuwanunulia pombe akihamasisha wananchi kukichagua Chama chake kabla ya muda wa kampeni haujaanza.

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema mara baada ya kumuona ameanza kampeni kabla ya wakati, walimfuata na kumtaka asubiri muda ufike ndipo aanze kampeni, hatua iliyosababisha kuwaamrisha wafuasi wake ambao walikuwa zaidi ya kumi kuwashambulia wanachama wa CCM waliokuwa watano.

Katibu Akyoo amesema kufuatia vurugu hizo wananchi, walimzingira Mbunge hyo na wafuasi wake ambapo mbunge huyo baada ya kuona wananchi wamekusanyika kwa nia ya kumpiga, aliingia ndani ya gari lake na kutokomea akiwaacha wananchi waliokerwa.

Katibu wa kata wa Usariver, Edmund Milanzi, akizungumzia tukio hilo amesema alishambuliwa na wafuasi wa CHADEMA baada kumtaka Mbunge huyo kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati na ndipo ghafla alishitukia anapigwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walimjeruhi kichwani, mdomoni na mkononi.

Baada ya kushabuliwa amesema alikwenda Kituo Kikuu cha polidsi wilayani Arumeru kilichopo kwenye mji mdogo wa Usariver na kufungua jalada la kushabuliwa na kujeruhiwa na hivyo kuweza kwenda hospitalini kupata matibabu.

tangu lini watu kama hao kwenye red wakaaminiwa kuthibitisha madai au malalamiko dhidi ya mtu mwingine?
 
View attachment 69499

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO,

Katibu wa kata wa Usariver, Edmund Milanzi, akizungumzia tukio hilo amesema alishambuliwa na wafuasi wa CHADEMA baada kumtaka Mbunge huyo kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati na ndipo ghafla alishitukia anapigwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walimjeruhi kichwani, mdomoni na mkononi.
Yaani yeye anaongea na Nassari kisha ghafla anashitukia akipigwa. Huyu Nassari aliwezaje kuongea na gamba wakati huohuo akiamrisha apigwe. Hizi huwa zinaitwa propaganda chafu
 
Back
Top Bottom