Mbunge Joshua Nassari anusurika kupigwa na wananchi wa eneo hilo la Usariver

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
nassari.jpg

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru, mashariki, Joshua Nasari amenusurika kipigo kutoka kwa wananchi ambao walichukizwa na kitendo chake cha kuhamasisha wafuasi wa Chama chake, CHADEMA, kuwashambulia wanachama wa CCM na kumjeruhi Katibu kata wa CCM, kata ya Usariver, baada ya kuzuiliwa asifanye kampeni za uchaguzi wa wenyeviti wa vitongoji katika mji mdogo wa Usariver kabla ya wakati.

Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO, amesema katika vurugu hizo zilizotokea katika eneo hilo la Usariver, katibu wa kata ya Kisambare wa Chama cha mapinduzi, alijeruhiwa kichwani mdomo na mkono ambapo amefungua jalada kituo kikuu cha polidsi wilayani Arumeru, USRIVER/RB 4397 /2012.

Ammesema chanzo cha tukio hilo ni mbunge huyo kuanza kupita nyumba hadi nyumba na kwenye vilaub vya pombe za kiasili na kuwanunulia pombe akihamasisha wananchi kukichagua Chama chake kabla ya muda wa kampeni haujaanza.

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema mara baada ya kumuona ameanza kampeni kabla ya wakati, walimfuata na kumtaka asubiri muda ufike ndipo aanze kampeni, hatua iliyosababisha kuwaamrisha wafuasi wake ambao walikuwa zaidi ya kumi kuwashambulia wanachama wa CCM waliokuwa watano.

Katibu Akyoo amesema kufuatia vurugu hizo wananchi, walimzingira Mbunge hyo na wafuasi wake ambapo mbunge huyo baada ya kuona wananchi wamekusanyika kwa nia ya kumpiga, aliingia ndani ya gari lake na kutokomea akiwaacha wananchi waliokerwa.

Katibu wa kata wa Usariver, Edmund Milanzi, akizungumzia tukio hilo amesema alishambuliwa na wafuasi wa CHADEMA baada kumtaka Mbunge huyo kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati na ndipo ghafla alishitukia anapigwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walimjeruhi kichwani, mdomoni na mkononi.

Baada ya kushabuliwa amesema alikwenda Kituo Kikuu cha polidsi wilayani Arumeru kilichopo kwenye mji mdogo wa Usariver na kufungua jalada la kushabuliwa na kujeruhiwa na hivyo kuweza kwenda hospitalini kupata matibabu.
 
Hata uongo magamba hawajui kutengeneza siku hizi.
Kwa mfano
1/Uthibitisho wa tukio ni katibu wa CCM!!!!

2/Nasari akimbie na gari halafu wafuasi wake kumi wabaki na hakuna aliyekamatwa!!!

3/Chadema walikuwa wanatoa rushwa ya kununulia pombe watu!!!
 
baada ya ile habari kuwa lema kapigwa kupuuzwa naona mmekuja na hii!!ccm is 6 feet from the edge!lets wait and see!!
 
Ulitegemea CCM wampende? Rekebisha heading ya uzi wako kuwa Mbunge Nasari anusurika kupigwa na WANACHAMA WA CCM
 
Habari hii haina ukweli mwandishi hajafafanua ni wanachama wa chama gani walikuwa wana taka kumpiga ,ameelezea tu ni wananchi ,hawa watakuwa ni wafuasi wa chama fulani ni vyema aweke wazi
 
inamaana waliotaka kumpiga Nassari ndio waliompiga katibu kata wa ccm.?....uongo mwingine hata kuutengeneza tabu.!
 
kichwa kingekuwa hivi" MAKADA WA CCM WAMGWAYA JOSHUA NASARI'' na sio wananchi wa user river
 
Dogo asilete mchezo huyu! Hakumbuki mateso aliyopata kwa kauli yake ya Kanda ya Kaskazini na ya Ziwa kujitenga?
 
Hata uongo magamba hawajui kutengeneza siku hizi.
Kwa mfano
1/Uthibitisho wa tukio ni katibu wa CCM!!!!

2/Nasari akimbie na gari halafu wafuasi wake kumi wabaki na hakuna aliyekamatwa!!!

3/Chadema walikuwa wanatoa rushwa ya kununulia pombe watu!!!

well said mkuu, kula 5
 
kama ameanza kampeni kabla kwa nini msiitarifu policcm ili wamkamate na mkataka kukabiliana nae wenyeewe?huyo aliyepasuliwa mdomo haikutosha angepasuliwa kichwa kabisa damu ya mbwambo inalia toka ardhini!
 
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO............,

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema alishambuliwa na wafuasi wa CHADEMA baada kumtaka Mbunge huyo kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati na ndipo ghafla alishitukia anapigwa na wafuasi wa CHADEMA ambao walimjeruhi kichwani, mdomoni na mkononi.

Mkuu, hongera kwa kutujuza. Lakini nadhani umekurupuka sana kuandika na kutuletea habari hii humu JF.
Mkuu, kama kampeni zitaanza kesho tarehe 28/10/2012, uchaguzi utafanyika lini? Au huo ni uchaguzi tofauti na zitakazofanyika tarehe 28/10/2012?
Mkuu, hata kama uliamrishwa uende uka-post haraka hiyo story katika JF, ulitakiwa uipitie kwanza kujiridhisha kwamba iko sawa. Matokeo ya kutokufanya hivyo ni hayo kwamba story inaonekana kabisa kwamba ni udaku.
 
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Katibu wa CCM wilaya ya Meru, LANGAEL AKYOO, amesema katika vurugu hizo zilizotokea katika eneo hilo la Usariver, katibu wa kata ya Kisambare wa Chama cha mapinduzi, alijeruhiwa kichwani mdomo na mkono ambapo amefungua jalada kituo kikuu cha polidsi wilayani Arumeru, USRIVER/RB 4397 /2012.

Ammesema chanzo cha tukio hilo ni mbunge huyo kuanza kupita nyumba hadi nyumba na kwenye vilaub vya pombe za kiasili na kuwanunulia pombe akihamasisha wananchi kukichagua Chama chake kabla ya muda wa kampeni haujaanza.

Kampeni zimepangwa kuanza Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema mara baada ya kumuona ameanza kampeni kabla ya wakati, walimfuata na kumtaka asubiri muda ufike ndipo aanze kampeni,
Kumbe anastahili kupigwa! yeye amekuwa tume ya uchaguzi?

Back
Top Bottom