Mbunge Joseph Msukuma simuelewi, Ona anavyozungumzia faida ya bunge kutokurushwa "live"

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Tumekuwa tukilalamikia uwezo wa wabunge wengi wa CCM kifikra. Bungeni ndipo mahala ambapo wahusika wanatakiwa kutuliza akili na kutoa mawazo chanya ya kulijenga taifa na kusimamia serikali katika majukumu yake ya kila siku. Mimi binafsi nimekuwa siioni faida ya wabunge zaidi ya asilimia 98 ya wabunge wa CCM kwa taifa! Ni mzigo ambao watanzania tunaubeba huku ukiwa hauna faida yoyote ile kwetu.

Mbunge wa Geita vijijini ndugu Joseph Kasheku Msukuma (CCM) amesema kuwa amefurahi sana bunge kutokuonyeshwa "live" kwa madai kuwa jimbo lake halina umeme hivyo watu wa jimbo hilo walikuwa wakilazimika kununua mafuta ya petrol kwa ajili ya jenereta ili kuangalia bunge "live". Aidha amesema kuwa kwa sasa wananchi hao hawatalazimika tena kuingia gharama ya mafuta hayo ya petrol na badala yake watajikita kwenye kilimo.

"Jimbo langu halina umeme, wananchi wangu walikuwa wakilazimika kununua mafuta yapetrol kwa ajili ya kuendesha jenereta ili waone bunge "live" hivyo walikuwa wanaingia hasara. Kwa sasa nimefurahi sana bunge kutokuonyeshwa "live" kwa kuwa hawatalazimika tena kuingia gharama ya kununua mafuta ya petrol! Watajikita zaidi kulima mashamba yao" alisema mbunge Msukuma.

Hao ndiyo wabunge wetu watukufu wa CCM wanaotakiwa kumshauri rais Magufuli anayetokana na chama chao.
 
Na CCM siku hizi inajua, imedumaza elimu yetu ili kuzalisha vijana hewa, siku hizi Cv ya mchujo ugombea wa ubunge ndani ya CCM wanaangalia watu wenye elimu ndogo na udumavu wa akili ili wawe watu wa NDIO MZEE, wewe unategemea mtu mwenye elimu isiyo magumashi awe anasema kila kitu ndio mzee!!Kw amtaji huuu ccm bado ipo ipo sana.
 
Umefika wakati wa bunge wale wanaojitambua ndani ya CCM sasa wake juu kuzuia hii dharau wanayoipata kutoka kwa wa bunge wenzao kama hawa.
Ina yanayotokea kauli inakuwa ujinga wa wa bunge wa CCM! Ilipaswa sasa Mbunge kama Msukuma akizungumza pumba kama hizo anatokeawingine kama Bashe anampinga na kumwelimisha kuwa hapo ndio unapoonekana umuhimu wa bunge kuonwa na wananchi.
Nikikumbuka Marehemu Fulikunjombe alivyokuwa anawapasha wenzake na kuwaambia aache unafiki najiuliza hakuna tena kama yeye ndani ya CCM?
 
Wabunge wa CCM tupige mako kwa kwa kwa kwa kwaaaaaaa na wananchi waliomchagua makofi kwenu, kwa kwa kwa na uongozi wa CCM udumu milele yote, kwa kwa kwa hapa kweli ni kazi tuuuuuuuuu! Umeme wa nn? Tuwashe vibatali, hapa kazi tuuu!
 
Back
Top Bottom