Mbunge: JK hana wasaidizi wazuri; Asema ndiyo maana bajeti haikidhi mahitaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge: JK hana wasaidizi wazuri; Asema ndiyo maana bajeti haikidhi mahitaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, JUNI 21, 2012 06:03 NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA

  *Asema ndiyo maana bajeti haikidhi mahitaji
  *Asema Serikali imevunja sheria kuwasilisha bajeti
  *Adai inastahili kuburuzwa mahakamani

  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), amesema kuwa kuandaliwa vibaya kwa bajeti ya Serikali ya mwaka huu ni kielelezo kwamba, Rais Jakaya Kikwete, hana wasaidizi wazuri.

  Alisema kutokana na hali hiyo, kuna hatari Serikali ikaburuzwa mahakamani kutokana na kuwasilisha bajeti hiyo kinyume cha sheria.

  Mbunge huyo, alisema sheria hiyo namba 40 kifungu cha (1), (2) na (3), cha Sheria ya Ukaguzi ambacho kinaitaka Serikali kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), juu ya matumizi ya fedha zilizotumika katika miradi mbalimbali ya Serikali.

  Mpina, alisema kutokana na sheria hiyo aliishangaa Serikali kutozingatia sheria hiyo na kwamba kuiandaa bajeti na kuiwasilisha bungeni ni sawa na kukiuka sheria hiyo.

  “Kimsingi sikubaliani na bajeti hii kwani haikuzingatia sheria na haijajibu hoja za CAG za mwaka wa fedha wa 2009/10, ambapo Bunge hili lilitakiwa kujibu hoja hizi kisha ndiyo Serikali iwasilishe bajeti.

  “Kwa hali hii, bajeti hii si halali na sasa umefika wakati wabunge wote tuikatae bajeti hii, ambayo imeletwa hapa kabla hata ya majibu kutolewa kuhusu matumizi ya fedha za Watanzania.

  “Hivyo kwa mujibu wa sheria, Serikali inastahili kuburuzwa kortini kwa ukiukwaji huu, na ni vema wabunge wenzangu wakatambua kuwa, wasaidizi wa Rais Kikwete hawafanyi kazi ipasavyo, sasa tuikatae bajeti hii ili kuweza kumsaidia rais kufanya marekebisho muhimu ya bajeti hii.

  “Umbile la bajeti hii limekuwa tofauti na bajeti iliyowasilishwa katika Kamati ya Fedha ya Bunge, ambapo ilitengwa Sh trilioni 2.1 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeeleo,” alisema Mpina.

  Alisema kuwa, bajeti hiyo haikuzingatia mahitaji ya sekta ya kilimo ambayo huajiri takribani asilimia 75 ya nguvu kazi nchini, kwa sababu imepungua kutoka asilimia 4.2 mwaka 2010 hadi 3.6 mwaka 2011, wakati kasi ya ongezeko la watu limeendelea kuwa juu.

  “Kutokana na hali hii, siyo halali Bunge hili kuanza kuijadili bajeti mpya, kabla ya kujiridhisha fedha za Watanzania walizozigawa zifanye kazi, zimetumika vipi,” alisema na kusisitiza Mpina.

  Pia alisema bajeti hiyo si halali kwa sababu, Bunge liliazimia asilimia 35 ya bajeti itengwe kwa ajili ya shughuli za maendeleo na asilimia 65 kwa shughuli za kila siku, lakini imekuwa asilimia 70 kwa 30.

  “Asilimia 30 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na 70 kwa shughuli za kila siku ni wazi kwamba, inakinzana na azimio la Bunge na mpango wa maendeleo, kwamba Sh trilioni 2.7 zilitakiwa zitengwe kwa maendeleo lakini imetenga Sh trilioni 2.2 kinyume na makubaliano.

  “Bajeti ya miradi ya maendeleo leo imepunguzwa kwa kiasi cha Sh bilioni 400 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka jana,” alisema na kuongeza Mpina.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wasaidizi wa Rais ni Mawaziri au Makati Wakuu? Wanaopanga bajeti ni Makatibu Wakuu

  Sasa nani sio Mshauri Mzuri wa Rais wetu?
   
 3. p

  politiki JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kukubali kuhudumiwa na wasaidizi wabovu ni udhaifu mkubwa sana kwani kazi ya Rais siyo ku hire tu bali na ku fire pia.
  kitendo cha kusindwa kutimua wasaidizi wabovu kinaonesha tatizo ni jk mwenyewe na siyo wasaidizi wake.
   
Loading...