Mbunge Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave afanya kikao na Viongozi wa CRDB tawi la Temeke

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
867
947
MBUNGE JIMBO LA TEMEKE MHE.DOROTHY KILAVE GEORGE AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA CRDB TAWI LA TEMEKE.

Kikao hiki kimefanyika muda wa Saa 4:30 Asubuhi Maeneo ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke.

Lengo lakikao hiki ni kufanya Mazungumzo na Benki ya CRDB juu ya kutoa Mikopo ya Riba Nafuu Pamoja na Elimu ya Usimamizi wa Fedha kwa Wananchi wa Jimbo la Temeke.

Mbunge Jimbo la Temeke Mhe Dorothy Kilave George amewaeleza Maafisa hao juu ya namna serikali inavyotoa Mikopo kupitia Manispaa zetu lakini amedhamiria kupanua wigo wa Mikopo katika makundi matatu (*Walemavu,*Kinamama na *Vijana)

MR.ENDREW AUGUSTINE ambaye ni Manager wa Tawi la CRDB Temeke Amekubaliana na Maombi ya Mhe.Mbunge wa Jimbo la Temeke na ameahidi kuandaa utaratibu maalumu kwaajili ya kuwanufaisha wananchi wa Temeke kwa Mikopo ya Riba nafuu Pia watashiriki kwa ukaribu sana kuhakikisha wanatoa mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa Vikundi na wajasiriamali Kama ilivyokubaliwa.

Kutoka
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Temeke.
06/04/2021.
 
Siasa za uongo hizi. CRDB wana principles za utendeji kazi ikiwepo vigezo vya kutoa mikopo na riba wanayopata. Siyo rahisi wabadilishe eti kwa sababu mbunge amefanya nao kikao. Benki haziendeshwi kwa siasa za ghilba.
 
Back
Top Bottom