Mbunge Jerry Silaa na ufafanuzi wa Askofu Bagonza

Badala ya kupangua hoja za Jerry kwa kutumia hoja Ndugai anatumia nguvu ya kiti cha uspika.
Hii kweli kabisa. Baada ya uamuzi kutoka, spika kama msimamizi mkuu wa mhimili hakutakiwa tena kutoa mfululizo wa kejeli kwa wahusika.
Ingekuwa mahakimu wanafanya hivyo ingeonekana mahakimu wanapendelea upande wa mashtaka.
Hii inaonyesha wazi kuwa mtu akiitwa kwenye kamati ya maadili hachomoki.
 
Kuna cheo cha kikanisa ukifika hustahili kuwa mwanaharakati. Tatizo ndio hilo walitoka katoliki wakajianzishia taratibu zao tofauti na katoliko lakini majina ya viongozi , mavazi wakayabeba hivyo hivyo kwa hiyo ni vigumu kwa mtu asiye mkristu kuwatofautisha watu hawa ndio maana akina shehe mazinge wanawaita mapadri , maaskofu wakidhani ndio sawa na wale wakatoliki. Askofu ni mtu ambaye ni miongoni mwa mapadre mwenye sifa za utulivu uliotukuka na busara ipitayo upeo wa kawaida.
 
Jambo hili linatukumbusha suala la Mh. Stephen Masele, aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge la Afrika hata kuwajibika kuomba radhi baada ya kuitwa mbele kamati hii ya maadili. Hii inaonyesha chuki ya wazi kwa wabunge vijana waliopo ndani ya Bunge la Afrika.

Wabunge vijana na wenye akili kubwa na fikra pevu wanapigwa sana vita ya chini chini ndani ya bunge linaloendeshwa na watu wasiopenda mafanikio yao ya hapo baadaye ya kisiasa. Pale wanapojipambanua na kuthubutu kuonyesha umahiri wao, na kudhihirisha wazi kuwa wao ni hazina na wana fursa ya kuweza kuaminiwa zaidi katika siku zijazo, jambo hili huwa linawaudhi mno watu kama Ndugai.
 
Back
Top Bottom