Mbunge Jerry Silaa agoma kusindikizwa na Polisi akielekea kuhojiwa na Kamati ya Maadili, adai kanuni

Kuna mkubwa flani hapo bungeni kaitwa baada ya Jerry kuwapiga mkwara askari wanao msindikiza. Alipo jibishana na Jerry maneno mawili matatu akatoa kadi nyeusi nadhani ya mualiko mfukoni mwake akamwambia mbunge Karibu na kwa mshangao mbunge akatii. Haya mambo kumbe si kwenye bar tu.
 
Kuna mkubwa flani hapo bungeni kaitwa baada ya Jerry kuwapiga mkwara askari wanao msindikiza. Alipo jibishana na Jerry maneno mawili matatu akatoa kadi nyeusi nadhani ya mualiko mfukoni mwake akamwambia mbunge Karibu na kwa mshangao mbunge akatii. Haya mambo kumbe si kwenye bar tu.
Duh hiyo "kadi nyeusi" naona umetumia codes...

Utakuwa mguu wa kuku lazima
 
Wabunge wa CCM hawawaamini wanakamati wa Bunge la CCM, ambao ni wana CCM,kazi kweli
 
Baada ya jana askofu Gwajima kugomea baadhi ya mambo kwenye kamati ya kumhoji ,leo tena mbunge wa Ukonga Jerry Slaa akielekea kuhojiwa kwenye kamati ya bunge alipofika kwenye geti aligoma kusindikizwa na askari na kuwataka wamuonyeshe ni kanuni ipi ya bunge inayomtaka akifika hapo getini asindikizwe na polisi mpaka kwenye ukumbi wa kamati.


---
Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa amewasili jijini hapa tayari kuhojiwa na Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge huku akikataa kusindikizwa na askari polisi kama ilivyokuwa kwa mwenzake, Askofu Josephat Gwajima aliyehojiwa jana.

Baada ya mabishano yaliyodumu kwa dakika kadhaa Silaa alikubali kuongozana na askari hao kuelekea ukumbini ambako mahojiano yalitarajiwa kufanyika.

Silaa amewasili bungeni hapa baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kumwamuru yeye na Askofu Gwajima kuhojiwa na kamati hiyo kwa kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge. Ndugai alitoa amri hiyo Jumamosi iliyopita.

Silaa amewasili bungeni saa 6:49 mchana akiwa kwenye gari jeusi sawa na suti aliyoivaa huku mkononi akisukuma sanduku jeusi pia.

Akiwa katika geti kubwa la kuingilia, Silaa alikataa kuongozana na askari wawili kama ilivyo utaratibu akitaka aonyeshwe kanuni inayotaka mbunge kusindikizwa anapoenda kuhojiwa na kamati.

“Hawa najua (waandishi wa habari) wapo kwa mujibu wa kanuni, hawa pia (maofisa usalama wanaolinda getini) wapo kwa mujibu wa kanuni, niambie kanuni gani inayonitaka niongozane nao (askari),” alihoji mbunge huyo ambaye kati ya mwaka 2010 na mwaka 2015 alikuwa meya wa Manispaa ya Ilal ajijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, Ofisa Mwandamizi wa Usalama bungeni, Peter Magati alimweleza Silaa kuwa Bunge huendeshwa kwa utaratibu, kanuni, sheria na miongozo ambavyo kila anayeingia ndani ya viunga hivyo anapaswa kuvizingatia.

Baada ya maelezo hayo Silaa alikubali kuongozana na askari hao mmoja akiwa amevaa kiraia na mwingine sare za polisi hadi katika viti vilivyokuwa karibu na mashine ya kukagulia watu wanaoingia jengo la utawala la Bunge.

Mgomo kama huo ulifanywa jana na Mbunge wa Kawe, Askofu Gwajima mara tu alipoingia kwenye ukumbi ambako mahojiano yalifanyika.

Gwajima alikikataa kiti kilichoandaliwa kwa ajili yake na akataka kipaza sauti kibadilishwe ndipo aongee. Kamati ilitekeleza masharti hayo na mbunge kiongozi huyo wa Kanisa la uzima na Ufufuo akahojiwa.

Chanzo: Mwananchi
Kinachofanyika na hawa akina Askofu Josephat Gwajima na Jerry Slaa ni Uthibitisho tosha kuwa kuanzia ndani ya CCM, Serikalini na hata System kwenye hakuko salama na Mama ( Rais ) ajiangalie na awe makini kuliko anavyodhani.
 
Huyu ndo alizima na ule mjadala ndege hazina faida.
Ni kidume wa mbegu.

Lakini wakati mwengine Katiba yetu inafikirisha. Tunaambiwa mbunge akiwa kwenye bunge au viwanja vya bunge askari hawatakiwi kumkamata. Tumeona askari wakiwasindikiza wabunge kama wanasindikiza wahalifu wastraabu.
 
Kuna mkubwa flani hapo bungeni kaitwa baada ya Jerry kuwapiga mkwara askari wanao msindikiza. Alipo jibishana na Jerry maneno mawili matatu akatoa kadi nyeusi nadhani ya mualiko mfukoni mwake akamwambia mbunge Karibu na kwa mshangao mbunge akatii. Haya mambo kumbe si kwenye bar tu.
Hahahaaaa....... Nimekuelewa bwashee!

Kadi nyingine ina kichuma katikati!
 
Back
Top Bottom