Mbunge huyu wa CHADEMA azidi kuimaliza CCM huko Iringa vijijini

Kama wabunge wa chadema wangezama vijijini kama chiku abwao mbunge wa Iringa akiwa na
gari yake ndogo aina ya suzuki kwenye roof ikiwa imezungukwa na maspika na bendera za chadema.
mama huyu kazi yake ni moja tu nayo ni kuibomoa CCM Iringa vijijini na hasa eneo la Kalenga.
ningependa wabunge wa chadema wafuate nyayo za huyu mama waache siasa za maofisini na kuzama vijijini.

JEMBE LA CHADEMA HUKO KALENGA.
mbunge Chiku Abwao baada ya kazi nzito ya kujenga chadema vijijini leo

Wafuasi wa Chadema kata ya Luhota wakisukuma gari alilopanda mbunge wao Chiku Abwao leo

Matembezi ya kwenda kufungua ofisi ya kata ya Chadema kata ya Luhota jimbo la Kalenga leo

Mbunge Chiku Abwao akimwaga noti na bendera za Chadema kwa ajili ya kuchangia ufunguzi wa ofisi kata ya Luhota leo

Wananchi wakiandamana kwenda kufungua ofisi ya Chadema vijijini kwenye kata ya Luhota jimbo la kalenga wilaya ya Iringa vijijini leo

Gari la mbunge Chiku likisukumwa leo

Katibu wa chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo akimkaribisha mbunge Chiku Abwao leo
CHADEMA cha demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa vijijini kimeanza kukibomoa chama cha mapinduzi (CCM ) baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kata ya Luhota na mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM wilaya ya Iringa vijijini Sihuna Kapalampya kuhamia Chadema na kuwa mwenyekiti mpya wa Chadema kata ya Luhota .

picha hizi kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com mwandishi nguli huko Nyanda za juu kusini.

tunaomba ofisa za CDM hapa ngara mjini mkoa wa kagera,kuna mashabiki wengi sana wanaosubiria kua wanachama kamili..ama nipeni mie mwongozo nifanye ntakacho kiweza.
 
sawa ni kweli uyu mbunge wetu ni makini na mpambanaji wa kweli kwa jinsi anavyopigana uko vijijini lakni kama kada mkongwe nampa ushauri uyu mama kama naingilia maisha yake binafsi anisamehe lakini aache kutumia calorite yani kujichubua kwake kwa kweli kunakera na sisi chadema atuna wabunge mashangingi wanaojichubua km ccm,yaani ata kama chiku sio shangingi lakin kwa jinsi alivyojichubua ameonekana kama shangambwali flani vile !
 
CHADEMA itoe maelekezo na kuwapangia malengo makatibu, viongozi wa ngazi za wilaya kufungua matawi vijijini, watu wanakosa hata sehemu ya kuchukulia kadi.

Umesema vyema mno .Chadema ime enea kote hta vijijini ila bado wananchi wale hawana mtu wa kuwashika mkono kwa kweli .Chadema tamkeni mambo yawe mambo jamani .
 
Chiku anabomoa vijijini kama anavyobomoa mjini. Waulize Mrema na Cheyo alivyowapiga kavukavu za uso kuwa wao ni mapandikizi ya CCM kidogo wale wazee wamwage chozi Bungeni. Tunataka wanawake wa shoka kama huyu sio wale chakula maalumu wa makofi kwa sana na mipasho waliojazwa na Twawala
 
Nikiona kazi ya huyu mama yetu natamani sana hata nihamie Iringa vijijini nikatoe support yangu niungane na wapambanaji, anyway acha tu nawasubiri wenje na highness wakija kufungua matawi mwanza
 
picha hazimpambi huyu mama, kwanza zinaonyeshwa anasukumwa kwenye gari (mrema, jairo), anagawa pesa (JK na wenzake), very minimal audience (nape), mkorogu umedunda (Anne Kilango malecela)

Lets share her success na sio picha ambazo ziko kama amepiga John Guninita
Tuache siasa za ki CCM. mwandishi francise hajakidhi baadhi ya mambo ambayo yameniacha na maswali mengi.:
1: Kwa nini mh mbunge anagawa fedha hadharani? ananunua haki? Sio sera ya CDM
2:Ofisi iliyofunguliwa mbona haionekani? Kanya boya hilo. Janja ya nyani anataka kuwaaminisha watu ili apate msaada wa fedha. Tumeliwa.
3:bona kama kanyumba kako isolated? hao wanachama wako wapi? naona kama ni vijana aliotoka nao Iringa mjini sio wananchi wa eneo husika.
4: NAOGOPA KUTUKANWA LAKINI TUWE MAKINI SANA NA HAYA. ISIJE KUWA MTAJI WA KISIASA 2015. MSIGWA KAA MKAO WA KULA.
 
JEMBE LA CHADEMA HUKO KALENGA.
mbunge Chiku Abwao baada ya kazi nzito ya kujenga chadema vijijini leo

Ameji-cream kweli kweli. Ngozi imeshaanza kuonyesha mabaka. Inabidi ashauriwe aache cream, vinginevyo atasema CCM wamemuwekea sumu.
 
Kama wabunge wa chadema wangezama vijijini kama chiku abwao mbunge wa Iringa akiwa na
gari yake ndogo aina ya suzuki kwenye roof ikiwa imezungukwa na maspika na bendera za chadema.
mama huyu kazi yake ni moja tu nayo ni kuibomoa CCM Iringa vijijini na hasa eneo la Kalenga.
ningependa wabunge wa chadema wafuate nyayo za huyu mama waache siasa za maofisini na kuzama vijijini.

JEMBE LA CHADEMA HUKO KALENGA.
mbunge Chiku Abwao baada ya kazi nzito ya kujenga chadema vijijini leo

Wafuasi wa Chadema kata ya Luhota wakisukuma gari alilopanda mbunge wao Chiku Abwao leo

Matembezi ya kwenda kufungua ofisi ya kata ya Chadema kata ya Luhota jimbo la Kalenga leo

Mbunge Chiku Abwao akimwaga noti na bendera za Chadema kwa ajili ya kuchangia ufunguzi wa ofisi kata ya Luhota leo

Wananchi wakiandamana kwenda kufungua ofisi ya Chadema vijijini kwenye kata ya Luhota jimbo la kalenga wilaya ya Iringa vijijini leo

Gari la mbunge Chiku likisukumwa leo

Katibu wa chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo akimkaribisha mbunge Chiku Abwao leo
CHADEMA cha demokrasia na maendeleo (chadema) wilaya ya Iringa vijijini kimeanza kukibomoa chama cha mapinduzi (CCM ) baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi kata ya Luhota na mjumbe wa kamati ya utekelezaji CCM wilaya ya Iringa vijijini Sihuna Kapalampya kuhamia Chadema na kuwa mwenyekiti mpya wa Chadema kata ya Luhota .

picha hizi kwa hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com mwandishi nguli huko Nyanda za juu kusini.

Tuache siasa za ki CCM. mwandishi francise hajakidhi baadhi ya mambo ambayo yameniacha na maswali mengi.:
1: Kwa nini mh mbunge anagawa fedha hadharani? ananunua haki? Sio sera ya CDM
2:Ofisi iliyofunguliwa mbona haionekani? Kanya boya hilo. Janja ya nyani anataka kuwaaminisha watu ili apate msaada wa fedha. Tumeliwa.
3:bona kama kanyumba kako isolated? hao wanachama wako wapi? naona kama ni vijana aliotoka nao Iringa mjini sio wananchi wa eneo husika.
4: NAOGOPA KUTUKANWA LAKINI TUWE MAKINI SANA NA HAYA. ISIJE KUWA MTAJI WA KISIASA 2015. MSIGWA KAA MKAO WA KULA.

hata mimi nakuunga mkono, ugawaji wa pesa hadharani ni mfumo wa waliolewa madaraka na kuiibia nchi hii wa kuwarubuni wananchi na huyu mama anarudia makosa yaleyale. nimeshangaa kata mbili za katikati ya mji katika uchaguzi wa madiwani CCM wamechukua kirahisi sana.
hiyo idadi hapo inatia shaka tofauti na mwandishi anavyopamba
ni vizuri kubuni njia mbalimbali za kujitangaza otherwise wananchi huko hawaoni tofauti kati ya hivi vyama
 
Bi. chiku abwao anafanya kazi nzuri na yenye manufaa kwa chama,kuhamasisha watu vijijini ni jambo la msingi na vilevile kuwapa mwamko wa kujua haki zao za kiraia.
 
Well done !!!! Kila kwenye mwanya kunatakiwa kuzibwa, ili Ccm wasipate njia ya kupita. Mwanzo mzuri kabisa huo na mwisho
uwe mzuri sana wenye matunda mema kwa Watanzania wote, na cha zaidi ni kuchangia Idea zetu na kuzifanyia kazi mara
moja kwa kila sehemu inayoonekana ni kikwazo kwa kusonga mbele. Na kule kwenye Tume ya uchaguzi kufanyiwe kazi ya
kuondoa na kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni, haswa Shaada ya kupiga kura iondolewe na kitabu cha kudumu cha
wapiga kura kiondolewe, Serikali za mitaa, Kata na za vijiji wao ni wahusika wa orodha ya wananchi wanaoishi sehemu husika.
Na mfumo mzima wa kuliwezesha swala hilo lipo na inawezekana, na hapo tutatokomeza swala la wizi wa kura, na hapo Ccm
ndipo utakuwa mwisho wake. Kwa ilo mswada Bungeni upelekwe kwani ni kikwazo cha maksudi cha kuleta rushwa na kuwan-
yima haki wapiga kura. Na mfumo mzima wa Bunge unatakiwa urekebishwe, Bunge lisiwe kama mvua ya masika ikiisha basi
mpaka mwakani, yaani ikishapitishwa Bajeti na Bunge limeisha mpaka mwakani, hivyo sivyo kabisa Bunge linatakiwa wakati
wote linafanya kazi chochote kinachoonekana katika sheria akiendani mara moja mswada upelekwe bungeni na kufanyiwa
kazi. Kwa hiyo hapo tuelewe kwamba vikao vya bunge viwe vinakuwepo kwa mwaka mzima mara kwa mara na sio kwa msim-
u. CDM hatua mliofikia mpaka sasa ni nzuri, makini na ya kutia moyo kwa Watanzania wote. Michango zaidi ya mawazo na
kuitekeleza ili kufungua njia ya Taifa jipya 2015.
 
tumieni akili kufikiri na sio masaburi.....huyo mbunge ametoa bendera za chedema na pia hicho kiasi cha pesa cha kuitegemeza ofisi mpy kwa ajili ya kununulia vifaa vya oficn walau kwa kuanzia kulingana na mazingira...sasa hapo ninyi mnafikiri kuwa huyu mama anagawa pesa kwa hao wananchi?? ..halafu MTM nashukuru umeelewa mdu alivyofafanua maana wakati nasoma post zako nilikuwa nimefumba jicho moja.
 
Kazi nzuri mama Abwao.
Inapendeza sana kuona jinsi unavyojitoa katika kwafikishia ujumbe wa CDM wananchi wa vijijini maana huko ndiko uelewa wao bado ni mdogo na tunakuomba usiishie tu hapo maana wananchi wa vijijini wanahitaji ukombozi wa kifikra na ufahamu.Wao ni wanaumia na kuishi maisha magumu lakini wanalaghaiwa kwa kupewa kanga, vitenge(wanawake) na kofia na T-Shirts( wanaume).Tunaomba ujumbe huu uende hata kwa wabunge wengine wa CDM
 
Tunaomba mbunge wetu Mch.Msigwa usaidiane na mama Chiku katika kuwafikia wanakijiji maana huko ndiko wanakohitaji elimu ya kuwakomboa kutoka umaskin.
 
A long safari starts with a single step! Good job cdm, magambazi tumbo linahara!
 
tumieni akili kufikiri na sio masaburi.....huyo mbunge ametoa bendera za chedema na pia hicho kiasi cha pesa cha kuitegemeza ofisi mpy kwa ajili ya kununulia vifaa vya oficn walau kwa kuanzia kulingana na mazingira...sasa hapo ninyi mnafikiri kuwa huyu mama anagawa pesa kwa hao wananchi?? ..halafu MTM nashukuru umeelewa mdu alivyofafanua maana wakati nasoma post zako nilikuwa nimefumba jicho moja.
mkuu kama ulikuwa unajibu hoja za IPOGOLO umetumia maneno mazuri nahisi kama ningesema kabla yako ningetumia maneno makali, labda mama alitakiwa awaandikie cheque akiwa kajificha sijui, kama huoni ofisi iliyofunguliwa mlaumu mpiga picha, kwa mawazo yako mama alienda pale kupiga picha(yapo maeneo mengi tu mazuri ya kupiga picha), usiliwe kaa na vijisenti vyako watakula wengine labda massage ya sinza, hao wanachama sijui wameruka kwa ungo sababu wasingetoshea kwenye gari la pekee tunajua mmezoea kuwapakia wapiga kelele wenu kwenye ma-fuso na scania kutoka mikoa ya jirani, mwisho sina haja ya kutukana jina lako linatosha...
 
mtamaholo

wewe ni muungwana na nimekusoma... iwapo sisi wanaJF tungekua kama wewe, basi tungekua mbali sana

Nimeheshimu sana ushauri wako na kuukubali kabisa, pamoja na hayo nadhani sisi tusioishi iringa ni vyema tukaona madawati, matrekta, vocha za mbolea hazijaibiwa, mipango ya maendeleo iko wilayani na pia mihutasari ya vijiji inafanyiwa kazi vyema

You have earned my reputation and i pray that you live long to realise our dream

Mkuu MTM i salute you for this. A very useful contribution.
 
tumieni akili kufikiri na sio masaburi.....huyo mbunge ametoa bendera za chedema na pia hicho kiasi cha pesa cha kuitegemeza ofisi mpy kwa ajili ya kununulia vifaa vya oficn walau kwa kuanzia kulingana na mazingira...sasa hapo ninyi mnafikiri kuwa huyu mama anagawa pesa kwa hao wananchi?? ..halafu MTM nashukuru umeelewa mdu alivyofafanua maana wakati nasoma post zako nilikuwa nimefumba jicho moja.
kuna bifu la chini kwa chini kati ya Msigwa na Chiku na bango hili lina kazi "maalum" na nimemuona Msigwa katupia dongo lake kwa mbaaali. Hebu nijishindilie kande zangu miye!! kwa wale msiojua Chiku keshaanza kutengeneza mtandao wake wa mwaka 2015 ubunge Iringa Mjini ua Isimani hali ambayo imeleta tafrani kati yake na Msigwa. Ndiyo maana humu ndani kuna maneno kama "Isimani" au "Iringa Mjini' yamejitokeza tokeza.
 
Back
Top Bottom