Mbunge huyu anatumia posho yake vyema jimboni mwake

Ubunge ni dili kubwa sana kwa huyu jamaa. Nakumbuka 1995 alishinda kwenye kura ya maoni, lakini ccm ilimpiga chini kwa madai kuwa hajakomaa kisiasa. Tokea hapo ilibidi aanze kugawa chakula kwa wananchi, na pia akajitolea kujenga jengo la ofisi ya ccm mkoa wa Singida kwa gharama yake. Hapo utagundua aliutafuta ubunge kama kinga ya baadhi ya biashara zake zisizofuata utaratibu. Pia utagundua kuwa siyo kwamba anatumia posho za kibunge kuwasaidia wapiga kura wake, kwasababu alikuwa akifanya hivyo hata kabla hajawa mbunge. Msaada anaoutoa ni mdogo sana kulinganisha na anavyowaibia wananchi.
 
Naona ndugu mmesahau,aliahidi kujenga uwanja wa namfua jee kashatumia posho yake vizuri kuujenga?watu wa singida nisaidieni.
 
Hivi ni lini watanzania tutafika mahali pa kutambua majukumu ya mbunge na kuweza kuyatofautisha n majukumu ya serikali?

Tutaacha kutumiwa kwa manufaa ya kisiasa ya wanasiasa mpaka pale tutakapotambua tofauti hii

Majukumu ya viongozi yalihama kutoka kuwa kiongozi na kuwa mfadhili baada ya Azimio la Arusha kuvunjwa kwa lile la Zenji.

Na hapo ndipo wajinga tunapoliwa
 
Ubunge ni dili kubwa sana kwa huyu jamaa. Nakumbuka 1995 alishinda kwenye kura ya maoni, lakini ccm ilimpiga chini kwa madai kuwa hajakomaa kisiasa. Tokea hapo ilibidi aanze kugawa chakula kwa wananchi, na pia akajitolea kujenga jengo la ofisi ya ccm mkoa wa Singida kwa gharama yake. Hapo utagundua aliutafuta ubunge kama kinga ya baadhi ya biashara zake zisizofuata utaratibu. Pia utagundua kuwa siyo kwamba anatumia posho za kibunge kuwasaidia wapiga kura wake, kwasababu alikuwa akifanya hivyo hata kabla hajawa mbunge. Msaada anaoutoa ni mdogo sana kulinganisha na anavyowaibia wananchi.

kheee! mabwaku kumbe ndivyo ilivyo mwarabu wa singida anawafanya raia wake..
 
Dewji kweli anafanya Mazuri Jimboni kwake... Mimi siipendi CCM lakini huyu Jamaa kiboko anaisaidia kweli Singida Mjini

mohamedi dewji ni mtu mbaya sana kwa singida, anabadili mindset ya wanyaturu kuwa ya kupokea rushwa kwa sana. analeta ulemavu wa akili, ni wa kuogopwa kama ukoma. huo sio msaada hata kidogo
 
Watanzania bana unaridhika kupewa mbuzi bila kujiuliza anaiba ngapi huna tofauti na wanaoachiwa marahaba wa 3% kwenye dhahabu.

Kuna wengine wanapiga kelele kuhusu hao wanaoiba wakibanwa wazikatae posho wanasema "sijataka niwe mbunge ili niwe masikini!" naona bora ya huyo anaetoa mbuzi kuliku anaetoa povu la mdomo akabaki na pesa zake!
 
Mo ana financial muscle na utakuta ni social responsibility ya Metl. Only few can be reach that niche
 
Mtazamo wangu tuu, Kijana anafanya kazi ya maana jimboni kwake na umma yote inaona angalau anawagaia wananchi wa jimbolake posho yake. Wabunge wengi wanaleweyaa tuuu posho... tungekuwa na wabunge kama kumi kama Mo tungekuwa mbali.. Kabda mtu ajapinga anitajie mbunge mwengine aliyepewa kura kuwakilisha watu wake na kile akifanyacho toka alipoingia kula bata...
mo+1.JPG

mo+4.JPG

mo+6.JPG

picha kutoka kwa mjomba michuziblog

anarudisha kidogo ktk nyingi alizotuibia lkn si haba
 
Sijawahi kumsikia bungeni huyu mbunge, yupo bungeni kwa kupiga na kuwa muhuri wa wabunge wa CCM tu au kuwawakilisha wananchi. Wanaojua hansadi za bunge watuambie lini huyu alishawahi kutoa mchango wa maoni bungeni.
 
Huyu jamaa kamaliza nchi.Tanga kanunua mashamba yamkonge kwa bei chee.morgro viwanda kamaliza. Sababu ya ubunge wake.
 
ubunge ni assets kubwa sana kwa kwani ndio anapofanikishia mambo yake mengi
 
Dewji kweli anafanya Mazuri Jimboni kwake... Mimi siipendi CCM lakini huyu Jamaa kiboko anaisaidia kweli Singida Mjini

halipi kodi anajificha nyuma ya pazia la wananchi sijui lini atarudi kwao huyu ponjoro!!
 
Anaongoza kwa kuingiza sukari,cement bila kulipa kodi!pia govt inampa korosho apeleke india fisadi huyu
 
Myopic! Shortsitedness! My dear tanzanians hivi value ya kiwanja chake ni actual au fictitious! Angalieni tusijeitwa ny
 
Ndugu zangu kwani MO, alitoa mbuzi wangapi????? Si mbuzi mmoja akizidi saana ni laki moja tu?? Kwani ni nani anayeshindwa kutoa laki moja??? au kuweka jiwe la msingi la darasa sijui ni nini si kazi zake tu za kawaida?? Mbona watanzania tunadanganywa na vitu vidogo saaana??? Huyu mtu afanye mambo makubwa kuitoa singida na mikoa mingine ya Central katika umasikini uliokithiri na wakati ni matajiri. Ajenge shule na aweke madawati na maofisi na maabara hayo ndo mambo kuwaondoa watu kwenye Ujinga na si kutoa mbuzi, unga, mchele hivyo awaachie watu wadogo wadogo.
 
anachovuna ni kingi kuliko anachotoa; haya makapi tu! Ni kweli dewj kazi yake n ufugaji? anawalaghai tu wananchi na rushwa ya mbuzi
 
nafikiri wewe ni mfuasi wake na lazima umsifie,mimi niko singida,tuna uhaba wa madawa hospitalini,tuna uhaba wa madaktari wa kutisha,kuna uhaba wa walimu mashuleni,kuna shida ya maji hasa wakati wa kiangazi,sokoni ni pachafu sana,uhalifu(vibaka) ni wengi sana,umasikini ni mkali sana hapa na jimbo lake halina hospitali wantegemea hospitali ya mkoa.nafikiri useme vizuri una maslahi gani na huyu bwana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom