Mbunge huyu anatumia posho yake vyema jimboni mwake

i411

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
906
290
Mtazamo wangu tuu, Kijana anafanya kazi ya maana jimboni kwake na umma yote inaona angalau anawagaia wananchi wa jimbolake posho yake. Wabunge wengi wanaleweyaa tuuu posho... tungekuwa na wabunge kama kumi kama Mo tungekuwa mbali.. Kabda mtu ajapinga anitajie mbunge mwengine aliyepewa kura kuwakilisha watu wake na kile akifanyacho toka alipoingia kula bata...
mo+1.JPG

mo+4.JPG

mo+6.JPG

picha kutoka kwa mjomba michuziblog
 
Watanzania bana unaridhika kupewa mbuzi bila kujiuliza anaiba ngapi huna tofauti na wanaoachiwa marahaba wa 3% kwenye dhahabu.
 
Dewji kweli anafanya Mazuri Jimboni kwake... Mimi siipendi CCM lakini huyu Jamaa kiboko anaisaidia kweli Singida Mjini
 
Mkuu, huyu si tajiri sana kiasi kwamba hayo anayofanya angeweza kuyafanya jata bila huo ubunge. Ametafuta ubunge kwa nia ya kujitafutia sifa tu.
 
Mnyika no.1. Maendeleo yataletwa kutokana na fikra mpya kuhusu nini kifanyike kujikwamua pa1 nakushirikisha Wananchi kujiletea maendelea yao binafsi kwa kiongozi kuwaonyesha njia na kiongozi kutetea haki na kubuni mifumo bora kupitia Bunge na kuhakikisha anaisamamia Serikali ili kuhakikisha Rasilimali za Nchi zinalindwa na zinawanufaisha Wananchi na sio Mafisadi wachache kitu ambacho Mnyika anakifanya kwa ufanisi Bungeni na kila mtu anaona,Nini mchango wa Dewji Bungeni?Anachokifanya Dewji nikuwapumbaza wananchi kuwa watumwa wakifikra kutokana na utajiri alio nao ambao hatujui aliupata kwa njia halali au hapana,kuwafanya Wasingida kuwa tegemezi kwamba bila Dewji hakifanyiki kitu na maendeleo hayapatikani hivyo rafiki yangu maendeleo yanaletwa na watu wenyewe,na ndio maana Singida ni miongoni mwa Mikoa mitatu ya mwisho kwa umaskini Nchini.TAFAKARI.
 
...hahitaji ubunge kupata sifa anageweza kuwa mfadhili wa taifa stars apate sifa nchi nzima. Anachotafuta ni advantage ya kibiashara kuwa bungeni kunamfanya awe na access ya taarifa muhimu za kisera na kimkakati za serikali mapema zaidi kaba ya washindani wake wa kibiashara nk....Anawasaidi watu wa singida ni kweli lakini mapenzi yakena Tanzania yanatia mashaka!..mashamba ya mkonge aliyonunua kule Tanga ameyatumia vipi zaidi ya kutumia lease kuchukulia mikopo. Huyu naye ni watu wanaoitafuna Tanzania kwa kutumia uchu wa viongozi/wanasiasa wazalendo.
 
Watanzania wepesi sana wa kuridhika. Yaani mtu unashangilia mbunge kutoa zawadi ya mbuzi? Kwani hitaji la muhimu la wananchi hapo singida ni mbuzi?

Hapo singida kulivyo na shida ya maji na umasikini wa kipato, ningemuona wa maana sana kama angekuwa ameyashughulikia hayo mambo muhimu sana na ambayo ndio hitaji la msingi na muhimu kwa wananchi.

Btw, hiyo pesa anayogawa huko singida kujitafutia sifa si amewadhulumu wakulima wa korosho mikoa ya kusini? Kama kweli huo ukarimu si wa ''kichina'' basi aanze kwa kuwalipa vizuri wakulima wa korosho, aache kuwapunja.
 
Hivi ni lini watanzania tutafika mahali pa kutambua majukumu ya mbunge na kuweza kuyatofautisha n majukumu ya serikali?

Tutaacha kutumiwa kwa manufaa ya kisiasa ya wanasiasa mpaka pale tutakapotambua tofauti hii
 
Mnyika no.1. Maendeleo yataletwa kutokana na fikra mpya kuhusu nini kifanyike kujikwamua pa1 nakushirikisha Wananchi kujiletea maendelea yao binafsi kwa kiongozi kuwaonyesha njia na kiongozi kutetea haki na kubuni mifumo bora kupitia Bunge na kuhakikisha anaisamamia Serikali ili kuhakikisha Rasilimali za Nchi zinalindwa na zinawanufaisha Wananchi na sio Mafisadi wachache kitu ambacho Mnyika anakifanya kwa ufanisi Bungeni na kila mtu anaona,Nini mchango wa Dewji Bungeni?Anachokifanya Dewji nikuwapumbaza wananchi kuwa watumwa wakifikra kutokana na utajiri alio nao ambao hatujui aliupata kwa njia halali au hapana,kuwafanya Wasingida kuwa tegemezi kwamba bila Dewji hakifanyiki kitu na maendeleo hayapatikani hivyo rafiki yangu maendeleo yanaletwa na watu wenyewe,na ndio maana Singida ni miongoni mwa Mikoa mitatu ya mwisho kwa umaskini Nchini.TAFAKARI.

Ni kweli kabisa ndugu yangu, wala sihitaji kuongeza kitu hapo!
 
Ela alizokwapua serikalini haviendani na izo mbuzi na cement ambavyo vyote havifiki 10mil
 
Mtazamo wangu tuu, Kijana anafanya kazi ya maana jimboni kwake na umma yote inaona angalau anawagaia wananchi wa jimbolake posho yake. Wabunge wengi wanaleweyaa tuuu posho... tungekuwa na wabunge kama kumi kama Mo tungekuwa mbali.. Kabda mtu ajapinga anitajie mbunge mwengine aliyepewa kura kuwakilisha watu wake na kile akifanyacho toka alipoingia kula bata...
mo+1.JPG

mo+4.JPG

mo+6.JPG

picha kutoka kwa mjomba michuziblog
Elimu ya shule ya kata inakusumbua .
 
Wewe unajua vizuri huyu ni mfanyabiashara anaeyekwepa kodi na kuingia mikataba feki na serikali huku akilindwa na ccm. Leo hii unataka kumlinganisha na mbuge wa kawaida kama Ole Sendeka mfugaji tu wa ngombe? Hataa haiwezekani bwana! Hata hivyo tumshukuru kwa kurudisha kodi zetu kwa njia hiyo hapa singida.
 
Dewji kweli anafanya Mazuri Jimboni kwake... Mimi siipendi CCM lakini huyu Jamaa kiboko anaisaidia kweli Singida Mjini
Kumpa pipi mtoto mwenye njaa haisaidii kumuondolea njaa inayomsumbua ingawa anaweza kuacha kulia kutokana na utamu wa pipi
 
Hii falsafa ya kugawa vijizawadi ndiyo inayofanya wabunge washindwe kutekeleza majukumu yake kuwajibisha serikali ilimradi wananchi wanawapenda kutokana na vijizawadi. Wananchi nao wanabweteka na vijizawadi wanashindwa kufikiria kwa upana ubora wa huduma kama elimu, barababa, hospitali, maji, n.k ambavyo havipatikana kwa sababu ya ufisadi. Wananchi wanashindwa kuwajibisha watendaji wa halmashauri wanaofuja mabilioni ya pesa za miradi, badala yake wanashangilia na kuridhika na vijizawadi vya wanasiasa
 
Watanzania bana unaridhika kupewa mbuzi bila kujiuliza anaiba ngapi huna tofauti na wanaoachiwa marahaba wa 3% kwenye dhahabu.

Watanzania bana kwa maneno ya vijiweni hivi ukiitwa mahakamani ukatoe ushahidi wa maneno yako upo tayari?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom