Mbunge huyu anamwakilisha nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge huyu anamwakilisha nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kabipi, Dec 14, 2011.

 1. k

  kabipi New Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Pindi Chana,Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kule Bungeni anamwakilisha nani? Nimeshangazwa na mchango wake alioutoa kwenye kuchangia Hotuba ya Bajeti ya Maliasili ambapo kwenye hansard alinukuliwa akisema:


  MHE. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Lini vibali vya kupasua miti
  katika Shamba la Sao Hill vitatoka? Mimi ni miongoni mwa walioomba vibali na sifa na vitendea
  kazi ninavyo; je, nitapata kibali cha kupasua mbao Sao Hill?
  Mheshimiwa Spika, Mbuga ya Kitulo Makete ipewe kipaumbele na uwezeshaji na Ruaha
  National Park Iringa ili watalii waweze kufika katika mbuga hizo za wanyama kwa wingi sana"


  nukuu hii inapatikana katika ukurasa wa 101 katika hansard iliyomo kwenye tovuti ya Bunge
  http://parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-4-50-2011.pdf

  kweli kwa mwendo wa wawakilishi wanaoweka maslahi yao mbele kwa namna hii tutafika? Kama ni kulipwa posho 200,000 ni kwa ajili ya kujiombea tender basi tumekwisha!
   
 2. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  wawakilishi bora wa wananchi wako bize kuendesha teksi, kusukuma mikokoteni na kunyoa kwenye masaluni..... hao wakina chana they are just golddiggers..
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Wakuu,
  Yatupasa kutambua jambo moja,nchi hii imeoza.shit!!!!
   
 4. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  unadhani NI TOFAUTI IPI KATI YA HUYU NA MBOWE AU JOSEPH SELASINI?THEY ARE THE SAME MPENDWA!!!!WAKATI WA UKOMBOZI NI SASA!!!
   
 5. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Amekwenda bungeni kuwakilisha kampuni yake ya kupasua mbao. You can see how ****** they are! How on earth can a representative of the people ask such a question. Mungu ihurumie Tanzania.
   
 6. s

  salaama JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Kasema hayo kweli au mchango wake umechakachuliwa tu ili kufurahisha genge humu ndani?
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hapana. Kifupi mwambie Chana amekwenda bungeni kuwakilisha kampuni yake ya mbao,familia yake/zake,na mafisadi wenzake wa kiwango chake!
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwani hamjui kwamba Pindi Chana na mbuge wa viti maalumu? Tangu lini wabunge wa viti maalumu
  wakawa wawakilishi wa wananchi? Wananchi gani waliomuchangua Pindi Chana kwa mbunge. Hawa akini
  Pindi Chana hawatakiwi kuwepo Bungeni in the first place. Get rid these nonsense MPs. Where is katiba
  mpya I'm tired and sick
   
 9. m

  marembo JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wanasema ulevi wa kitu chochote nooma! hawa ni zao la ufisadi kwa sasa hawaoni haya wanaiba na kuhujumu mchana kweupe. Hawamwakilishi mtu yeyote ni matumbo yao yasiyokuwa na mpaka. Kwa sasa wamekula bila kunawa na kuvimbiwa.
   
 10. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Du kwa mwendo huu wa magamba sijui kama tutafika,mtu anahoji wazi wazi kuhusu kupewa msitu apasue mbao?hapana wamevuka mipaka sasa.
   
 11. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Pathetic fool!


  Kuna siku niliwahi kusema kuwa nafsi dhaifu haimfai mwanaume. Huu ni mfano wa nafsi dhaifu na akili za kitoto. Mtu dhaifu mwanawe akifeli darasani, hasemi mwanangu kafeli badala yake atasema mwaka huu watoto wamefeli sana. Kule kuwajumuisha watoto wa wenzie kwenye ujinga wa mtoto wake humpa nafuu ambayo ukiizingatia ni UJINGA ULIOTUKUKA.

  Hii ishu ya Pindi Chana kuuliza mambo yake binafsi badala ya kuwawakilisha wananchi wake inahusianaje na Mbowe na Selasini? Unajifanya mwanachama wa CHADEMA kumbe una ugomvi wako binafsi na Mh.Mbowe. Ktk maaisha kubali kuwa kuna watu wana uwezo zaidi yako kwa hiyo suluhisho ni kuwa karibu nao ili uweze kujifunza kwao na sio kuwachukia na kuwazulia mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.

  Huyu aliyeanzisha hii thread ameweka na nukuu ya hansard ya kikao cha bunge na shutuma zake zimeegemea kwenye ushahidi huo, wewe wa kwako dhidi ya Mbowe na Selasini uko wapi?


  Kama huna kaa kimya, usilazimishe watu wengine kushiriki umbea na majungu yako ya saluni za kike za uswahilini. Shame on you! Chuki imekujaa mpk unshindwa kuwa reasonable, au Mh. Mbowe kakuzidi kete sehemu kwenye vi-chanchede?
   
 12. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hapana muheshimiwa, imechakachuliwa ili ikufurahishe. Hata hiyo link ni ya uongo.
   
 13. d

  dada jane JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh Shizukan huwa nayakubali majibu yako. Live long life. We will meet somewhere.
   
 14. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Narudia kusema kua WEWE ni Mamluki,shen.z.i type.Tueleze waliyoyasema Mbowe na Selasini.
   
 15. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu hili ni BONGE la jibu kwa huyo MPUMB.AV.U,ana boa sana huyo jamaa..
  c
   
 16. p

  politiki JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Pindi Chana atakuwa amevunja sheria ya maadili ya uongozi ambayo inasema kwamba kiongozi yeyote aruhusiwi kutumia nafasi yake ya uongozi kwa ajili ya manufaa yake binafsi. cha kufanya hivi sasa ni kwa mtu yoyote kupata copy ya hansard
  hii na kwenda kufungua complain dhidi ya Pindi Chana kwenye tume ya maadili ya viongozi.
   
 17. p

  politiki JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hizi ndizo sheria alizovunja pindi chana akiwa kama mtumishi wa umma.

  [h=2]B. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995[/h]Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:
  • Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;
  • …
  • Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;
  • Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.
  Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:
  • kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;
  • kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;
  • kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;
  • kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;
  • kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;
  • kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;
  • kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;
  • …
  • Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;
  • Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma.
  [HR][/HR][1] - Ibara ya 8(1)
  [2] - Ibara ya 9
  [3] - Ibara ya 26(1)
  [4] - Ibara ya 27(1)
  [5] - Ibara ya 27(2)
   
 18. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Usiwe mvivu wa kufikiri na kutenda; double click hiyo link ya website ya bunge na utaona inafunguka uisome live bila chenga. Kama huna adobe pdf reader, download au nitumie PM nikurushie adobe pdf professional upate vya bure!!!
   
 19. N

  Ndole JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mama mdogo sijakuelewa, unasema hiyo link imechakachuliwa au .........sijakuelewa ma mdogo tafadhali..
   
 20. D

  DT125 JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ntongwisangu kijapani ni mtoto mwenye jinsia mbili, ya kike ina nguvu zaidi lakini anakuwa na maumbile ya kiume na huvaa nguo za kiume. Utafiti uliofanyika Prof K. P Saimoto huko Japan mwaka 1976 umeonesha kuwa mara nyingi watu wa namna hii hupenda kufunga ndoa na akina mama wajawazito wasio usababisha wao. Kwa wanaojua kijapani nitawapa tovuti siku nyingine.
   
Loading...