Mbunge hutunza kumbukumbu za ofisi au la?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
1,250
:behindsofa:
Ofisi ya bunge ni sehemu ya ofisi za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mbunge ni mmoja kati ya wachaguliwa na wananchi wanaofanya shughuli za Baraza kuu la kutunga sheria Tanzania na pamoja na kuwa karibu na wananchi katika shughuli za maendeleo na maisha ya kila siku. Ndio maana mbunge ni msemaji wa wananchi kwenye vikao vya bunge na serikali.

Kwa vile mbunge ana ofisi ni dhahiri ofisi hutunza kumbukumbu za majukumu na shughuli mbalimbali zambazo hufanywa na mbunge, na kumbukumbu hizo hutoa tadhmini ya majukumu yake kwa wananchi na pia hutoa mwanya wa kujua mbunge anayefuata katika ofisi nini mwenzake amefanya na wapi pa kuanzia katika utendaji wake wa kazi jimboni.

Mbunge mpya anapoingia na kukuta ofisi tupu inayoonyesha kwamba imesahaulika kwa miaka bila kutunza, hali kadhalika hakuna kumbukumbu ya nyaraka zo zote wakati jimbo hilo lipo tangu tupate uhuru, ni uthibitisho kwamba wabunge waliotangulia wamekuwa wakifanya shughuli zao za wajibu wa bunge kama mradi binafsi na wala si kwa ajili ya maslahi ya umma. Kwa maneno mengine kwa miaka yote mitano na zaidi hakuna kilichofanyika katika jimbo hilo kwa sababu ya kutokuwepo kumbukumbu yo yote ya kiofisi.

Wabunge wanaolalamikiwa ni wale wa Chama cha mapinzuzi kuhamisha vitendea kazi vya ofisi pamoja na kumbukumbu zote za utandaji wao katika ofisi ya jimboni mwao kwa baadhi ya majimbo. Kwa maana ya mfumo wa siasa safi na uongozi bora tungetazamia viongozi wa ngazi ya juu wa CCM kutoa tamko kuhusiana na jambo hilo lakini wamekuwa bubu, wakati huo wabunge wamekuwa wakipewa pesa za kukendeshea ofisi pamoja na fungu la serikali la kuhudumia ofisi hizo. Kama vifaa hivyo walinunua wenyewe pesa walizopewa kuendeshea ofisi za bunge wamezipeleka wapi?

Ama kwa hakika jungu kuu halikosi ukoko. Unapokosekana ushindani wa kweli kidemokrasia kila aliyepata nafasi hufanya kama ofisi yake binafsi na wala ya si ya shughuli za serikali. Baada ya upinzani kuanza kuwa na nguvu sasa tunashuhudia uvundo kwenye ofisi za wabunge ambazo wapinzani wameshinda. Sasa je ushindani ukipata nafasi ya kushika nchi niambieni uozo mwingi utakavyofumuka amini usiamini, kwani huu ni mwanzo tu.

Kwa mtu mwenye ustaarabu wa kushika wadhifa mkubwa kama uwaziri, ukuu wa mkoa nk. tungetazamia anakuwa mwadilifu na mtulivu na kufanya makabidhiano mazuri ya ofisi, na hapo ingekuwa maelewano yao kwamba hiki kilikuwa changu, badala ya kung'oa kitasa kabisa na kuleta hisia mbaya kwa jamii na viongozi wajuu wa CCM kubaki wameshona midomo kama hawajui nini kilichotokea. Ni aibu na wapinzani yote wanayachora na miaka mitano si mbali. Je watakapoyafumua yaho katika kampeni zijazo watasema ni uzushi, wapuuzeni tu?
Hata mjasirimali binafsi hutunza kumbukumbu za umachinga wake, iweje ofisi kubwa ya Bunge inayotambuliwa kikatiba ikose kumbukumbu za kiofisi? Aibu tupu!!!!!!!!
:behindsofa:
 

Gad ONEYA

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
2,633
1,195
Unazungumza ukiwa afrika au ulaya na marekani? Jibu ni obvious!
:couch2: ndo maana unaongea behind sofa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom