Mbunge Ghasia alia na wanaotaka kuvuruga agizo la Rais. Awatupia lawama madiwani

Mar 22, 2019
46
55
Na Bakari Chijumba,Mtwara.

Zikiwa zimepita Siku kadhaa tangu Rais Magufuli aagize Hospitali ya Wilaya ya Mtwara ijengwe katika kijiji cha Nanguruwe badala ya Mkunwa kama ilivyoamuliwa na madiwani, Mbunge wa jimbo la Mtwara Vijijini(CCM), Bi.Hawa Ghasia ametembelea kijiji cha Nanguruwe na kusema atashirikiana na wananchi kutekeleza agizo la Rais,licha ya uwepo wa baadhi ya watu wanaojaribu kukwamisha agizo hilo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Jumamosi 20 April 2019, Bi.Hawa Ghasia amesema wapo baadhi ya watu wanaotaka kukwamisha ujenzi wa Hospitali kijijini hapo kwa kisingizio cha udogo wa eneo na madai ya sehemu hiyo kukosa sifa ya kujengwa Hospitali ya wilaya.

"Mchakato wa Kujenga Hospitali ya wilaya Nanguruwe,tumeuanza tangu 2010 Rais Kikwete alipokuja kuomba kura hapa..Kilichonishangaza serikali imetoa Billion 1.5 badala ya kujenga Hosptali hapa,Watu wengine wanaamua kuhamisha kwenda kuanzisha sehemu nyingine kwasababu zao" amesema Bi.Hawa Ghasia na kuongeza kwamba;

"Tulikubaliana Bilion moja imalizie Hosptali ya wilaya Nanguruwe,Million 500 ibaki Mkunwa ijenge kituo cha Afya..Juzi nikiwa Dodoma napigiwa simu naambiwa kuna watu wanasema eneo la Nanguruwe ni Dogo halifai,nimeshangaa nafika hapa tumezunguka eneo zaidi ya Dk 30,eneo linatosha na ni eneo kubwa zaidi ya Hospitali za wilaya nyingi nchini"

Aidha Mbunge huyo amewaelezea wananchi wa Nanguruwe kiini cha tatizo na kile kilichopelekea ujenzi wa Hospitali kuhamishiwa Mkunwa badala ya Nanguruwe na kusisitiza kuwa Madiwani Walidanganywa.

"Kabla ya Rais kufika hapa..Nilipata taarifa kuwa Baraza la Madiwani wamehamisha Hosptali ya wilaya Mtwara,isijengwe Nanguruwe na wameipeleka mkunwa wakidai kuna maelekezo toka Tamisemi..Nikaenda Tamisemi wakakataa..Siwalaumu Madiwani,wamedanganywa" amesema Mbunge Ghasia na kuongeza;

"Siwalaumu Madiwani,walidanganywa kwamba kuna maamuzi ya TAMISEMI, walienda kwenye kikao wakasomewa kwamba kuna barua inasema hospitali ijengwe mkunwa au Msijute,badala ya Nanguruwe,Madiwani wakachagua mkunwa..Nikamfata Waziri Jafo akakataa na kuahidi atakuja"

Bi.Hawa Ghasia akatumia Fursa hiyo kuwasihi wananchi wa Nanguruwe kuungana nae na kushirikiana nae katika kuhakikisha wanasukuma maendeleo ya eneo hilo badala ya kuendeleza misuguano itakayowafanya washindwe alichoita vita dhidi ya wasiowatakia mema.

'Tangu nimekuwa Mbunge sijawahi kuwa na mkutano mkubwa kama huu..Ndugu zangu wa Nanguruwe tukitaka tushinde hii vita mimi na nyinyi tuwe kitu kimoja,tukianza kugombana wenyewe tutashindwa na ndo wanachotaka..Hakuna anayeweza kubadili agizo la Rais,Hospitali itajengwa Hapa"~amesema Mbunge Ghasia na kuongeza kuwa;

"Mimi ni mjumbe kamati ya huduma za jamii,baada ya kutoka kamati ya Bajeti..Tulienda Mwananyamala,kilikuwa kituo cha huduma za mama na mtoto,ikawa zahanati kisha kituo cha Afya,hadi Hosptali ya wilaya,sasa ni Hosptali ya Rufaa..kwanini Nanguruwe tusibadili kuwa Hosptali ya Wilaya?" amehoji Mbunge huyo.

Katika hatua nyingine Ghasia akaonesha kusikitishwa na uzushi unaoenezwa ili kuwajengea wananchi dhana ya kwamba yeye ndo anakwamisha ujenzi wa Hospitali hiyo.

"kuna wengine wanaozusha kwamba eneo la Mkunwa ni la Hawa Ghasia, Jamani! Ghasia ana maeneo mangapi?uko munakosikia wanasemaje kwamba mimi ndo nalazimisha wajenge Mkunwa nilipwe fidia?,Musidanganyike..Niko na nyinyi kuhakikisha maagizo ya Rais Maguful yanatekelezwa.

Ziara hii ya Mh.Ghasia inakuja wakati ambapo siku chache zilizopita Rais Magufuli akiwa kwenye ziara Mkoani Mtwara alisimamishwa na wakazi wa eneo hilo ili kutoa changamoto zao kadhaa ikiwemo ya kuhamishwa kwa Hopsitali, jambo lililopelekea Rais Magufuli kuagiza Hospitali ya wilaya ya Mtwara ijengwe hapo hapo.View attachment 1077111
IMG_2616.JPG
View attachment 1077112
 
Sijaelewa hapa, serikali imetoa hela bilion 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospital nanguruwe, hela ilipofika nyinyi mkazigawa zingine nanguruwe zingine mkunwa?? Hayo maamuzi ya kugawa hela elekezi yalisababishwa na nini?? Nani walizigawa?? Na kwanini wazigawe???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom