Mbunge gani ajitokeze kujibu maswali haya.

SPACED

Senior Member
Jun 7, 2016
137
132
Wanabodi salamu ziwatangulieni nyote

Nidhahiri kabisa kila mmoja wetu ameshapata muda kutosha kutafakari kauli za viongozi wetu walizozitoa pale Chimwaga jana.
Binafsi nimeitafakari kauli iliyotolewa na waziri wa nchi UTUMISHI NA UTAWALA BORA akirejelea masharti yaliyomo katika ibara ya 67(1) ya katiba ya nchi ya 1977, kuwa zoezi la uhakiki halikuwagusa viongozi wa kisiasa na WABUNGE ikiwa ni miongoni mwao

Katika ufafanuzi wake alisema moja ya sifa kuu ya kuwa mbunge ni "kujua kusoma na kuandika" yaani KK. Nikiwa nimezama katika tafakuri yangu, nimejikuta najiuliza maswali mengi yanayohitaji maamuzi ya haraka iwezekanavyo yatakayoliweka taifa letu salama zaidi.

1. Je, tukiwaita wabunge wetu kuwa ni vilaza tutakuwa tunawakosea heshima?
2. Je, tukiwaambia wabunge wetu ukweli kuwa ni watu waliopata fa fa fa fa kwa masomo yasiyo ya KK watatuchukia?
3. Kwa mazingira ya dunia tulionayo leo ni halali kuongozwa na wabunge wenye vyeti vinavyowaonyesha kuwa wamefaulu katika madaraja mawili tu ya KK? ( ni dhahiri K ya tatu inawapa shida sana mjengoni)
4. Je, Wasomi wakiandamana kupinga kuongozwa na wabunge vihiyo wataonekana watukutu?
5. Je, Watumishi wa umma wenye sifa za kitaaluma wakikataa kusimamiwa na mawaziri ambao sharti awe mbunge wataonekana wakorofi?

6. Je, kwa mujibu wa ibara ya 67 wabunge wanayo mamlaka ya kumuita Makonda au RC yeyote na kuhoji? au kumtaka awaonyeshe vyeti?

Nimetafakari na kujiaminisha kuwa wakati mwingine wabunge wanaingia mgogoro na wakuu wa mikoa na wilaya pamoja na wakurugenzi sababu kuu ikitokana na sifa za teuzi zao ikiwa ni pamoja na uwezo wao (darasani)kitaaluma.

Ili kuliweka taifa letu salama, kuanzia sasa wabungwe wote wapigwe stop:
1. kwenda kuhoji taasisi za kiserikali katika maswala ya kitaaluma kwa mwamvuli wa kamati za ya bunge.
2. Kuridhia mikataba inayohusisha hesabu
3. Kujadili hoja iliyojuu ya uwezo wao 'isiyohisu KK' waruhusu hoja hiyo ikajadiliwe kwenye taasisi kielimu.
4. Kupitisha sheria yeyote iliyoletwa na mtumishi asiye mbunge.
5. kupitisha bajeti ya nchi iliyokataliwa na wasomi ikilenga kuwaumiza wananchi
6. Ongezea jambo lolote lililojuu uwezo wa mbunge mwenye KK

Pendekezo langu, wabunge wote kuanzia sasa wasimame kidete kupinga ibara ya 67 ifutwe au ifanyiwe marekebisho LA hasha wakae kimya kabisa uwezo wa kiutendaji wa watumishi katika idara mbalimbali.
Njooni tutafakari pamoja kuliokoa taifa
 
Back
Top Bottom