Mbunge filikunjombe atumia michezo kuhamasisha maendeleo ludewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge filikunjombe atumia michezo kuhamasisha maendeleo ludewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Francis Godwin, Jun 22, 2011.

 1. Francis Godwin

  Francis Godwin Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG][FONT=&quot]Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Filukunjombe akakabidhi zawadi ya Ng’ombe na kombe kwa mabingwa wa mashindano ya Filikunjombe Cup kata ya Lupanga timu ya kijiji cha Lupanga timu hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa timu ya Rusala kwa jumla ya goli 2-0 katika mchezo wa fainali[/FONT]
  [​IMG][FONT=&quot]Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Filukunjombe akakabidhi kombe kwa mabingwa wa mashindano ya Filikunjombe Cup kata ya Lupanga timu ya kijiji cha Lupanga timu hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa timu ya Rusala kwa jumla ya goli 2-0 katika mchezo wa fainali[/FONT]

  MASHINDANO ya kuwania kombe la mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa Deo Filikunjombe yameendelea kushika kasi katika kata mbali mbali za wilaya ya Ludewa huku timu zaidi zikiundwa .  Mashindano hayo yameanza kutoa hamasa kubwa za kimichezo katika wilaya hiyo kutokana na timu hiyo kushuhudia zoezi la timu za kata ya Lupanga kukabidhiwa kombe ,Ng’ombe na vifaa vya michezo kutoka kwa mbunge huyo kama alivyopata kuahidi .

  Tayari kata ya Lupanga imeweza kukamilisha mashindano hayo kwa timu ya kijiji cha Lupanga kufamnikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya kombe la mbunge Filikunjombe baada ya kuiadhibu vikali timu ya timu ya Rusala kwa jumla ya magoli 2-0

  Fainali hiyo imefanyika juzi katika uwanja wa michezo wa kijiji cha Lupanga na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata hiyo wakiongozwa na diwani pamoja na mbunge wa jimbo hilo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo.

  Mashindano hayo yalishirikisha jumla ya timu 3 kutoka vijiji vya kata hiyo ikiwemo timu ya Utiriri , Rusala na Lupanga ambayo ndio iliibuka mabingwa wa jumla wa mashindano hayo mwaka 2011.

  Lupanga ilijinyakulia kombe hilo baada ya kufanikiwa kufiisha magoli 13 ya kufunga na magoli 5 ya kufungwa na kuwa na pointi 9 ambazo hazikufikiwa na timu nyingine zilizopata kushiriki mashindano hayo.

  Wakati mshindi wa pili katika mashindano hayo ni Rusala iliyokuwa na magoli ya kufunga 8 kufungwa 8 na pointi 5 huku Utiriri ikishika nafasi ya mwisho kwa kuwa na goli 1 la kufunga na magoli 3 ya kufungwa na pointi 1 pekee.

  Katika mchezo huo wa fainali Lupanga iliweza kuiadhibu Rusala kwa jumla ya magoli 2 -0 na kujiongezea pointi zaidi zilizopelekea kutwaa ushindi huo.

  Wakizungumza katika ufungaji wa mashindano hayo mbunge Filikunjombe alisema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo kwa kata zote za jimbo hilo la Ludewa ni kutaka kuhamasisha michezo na kuepusha makundi ya kisiasa wakati huu wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kama mbunge.

  Filikunjombe alisema kuwa pamoja na kuwa timu ya Lupanga ndio imeibuka bingwa katika mashindano hayo ila bado amelazimika kukabidhi zawadi kwa timu zote zilizopata kushiriki ligi hiyo ili kuziwezesha kuendelea na michezo katika maeneo yao.
  BOFYA HAPA

   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni hatua nzuri sana kwa kuanzia. Lakini sisi wakazi wa Ludewa tunajua kabisa kwamba changamoto za Ludewa ni kubwa kuliko hiyo hamasa ya michezo. Kumbuka kilichomuangusha mtangulizi wako Profesa Mwalyosi. Mara nyingi viongozi wajanja wajanja husahaulisha watu ahadi na shida zao kwa kuanzisha na kudhamini mashindano!
   
 3. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Bado unaendelea au umemaliza? Natafuta maendeleo siyaoni. Au kwako wewe maendeleo ni kurukaruka na kukimbiza mpira tu?
   
 4. johnluoga

  johnluoga Member

  #4
  Feb 21, 2013
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi kama mwanaludewa nimulaishwa sana namaendeleo ya mbunge wa jimbo kwa kasi anayo ifanya jimboni LUDEWA.
  Pamoja na kutekeleza ilani ya ccm humojimboni ludewa bado nayeye anakuja kasi sana ukilinganisha na wabunge waliopita.mimi kama mwana nchi wa ludewa naseme tumemupa mbunge ambae yopo makini sana ktk utendajiwake wakazi .DEO FILIKUNJOMBE nijembe ambalo haishindwi popote deo songa mbele na ludewa ssi tupo nyumayako.
   
 5. bysange

  bysange JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2013
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 4,378
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jamaa jembe sana sehemu kubwa ya ahadi zake kagusa na kitaifa bado ana tikisa kutetea wanyonge
   
Loading...