Mbunge Esther Matiku Hajui Kiswahili AU Mikogo tu ya Kiswa-english?

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Esther Mattiku sikujua kama hajui Kiswahili mpaka nilipo mwona akichangia sasa hivi hotuba ya Wizara ya Kazi na Vijana
Huyu Mbunge wa viti maalum wa CHADEMA hajanifurahishi sana anavyojaribu kukinyonga kiswahili kiwe kiingereza.

Hivi kama unahisi umekaa nje sana na lugha ya kiingereza imekuathiri sana kwa nini usimwombe tu Spika uchangie kwa lugha ya KIINGEREZA kuliko kutumia Kiswahili ambacho hukijui sawasawa. Unapochanganya Kiswahili na kiingereza kwa kiasi kikubwa namna hii unatuudhi sisi wazalendo.

Namwomba wakati mwingine achangie kwa lugha anayoifahamu vyema la sivyo tutaanza kuona analichora bunge kwa mikogo ya kiswa english chake fake. Be NATURAL!!!!!!!!!!
 
Esther Matiku sikujua kama hajui Kiswahili mpaka nilipo mwona akichangia sasa hivi hotuba ya Wizara ya Kazi na Vijana.
Huyu Mbunge wa viti maalum wa CHADEMA hajanifurahisha sana anavyojaribu kukinyonga kiswahili kiwe kiingereza.
Hivi kama unahisi umekaa nje sana na lugha ya kiingereza imekuathiri sana kwa nini usimwombe tu Spika uchangie kwa lugha ya KIINGEREZA kuliko kutumia Kiswahili ambacho hukijui sawasawa.
Unapochanganya Kiswahili na kiingereza kwa kiasi kikubwa namna hii unatuudhi sisi wazalendo.
Namwomba wakati mwingine achangie kwa lugha anayoifahamu vyema la sivyo tutaanza kuona analichora bunge kwa mikogo ya kiswa english chake fake.
Be NATURAL!!!!!!!!!!
Hizo mbwembwe tu, kanifundisha 2009/2010 na alikuwa anaongea kiswahili kizuri tu inapombidi.
 
kwani akichanganya lugha tatizo ni nini? khaaaaaaaaaaaaaaa wewe mvumbuzi huna kazi za kufanya, sasa unataka wanaume wazima tuchangie huu upupu hapa, "kama umempenda kanywe nae chai"
 
Esther ni mwanasiasa mzuri sana....Kiswahili hakifahamiki sawasawa na watanzania walio wengi,Kiingereza ndiyo usiseme.Sasa sijui tutafikia hatua sasa tuataanza kuchangia kwa mother tongue

Kwa mfano mchango wa Esther wa Leo ni mzuri sana na watanzania wamemuelewa.Kinachohitajika ni mawazo huru,fikra pevu na uwezo wa kuhamasisha na kuongoza wale anaowawawakilisha au kuwaongoza

Guys,Are you insinuating that she's not wordsmiths? Or are you exasperated about her oratorical style?
 
Kaka sometimes wakati unachangia na kufanya comperatives katika ajira lazima usome kwenye nchi nyingine wanafanya nini hivyo kuchangia kwa kingereza sio issues maana kama watu wanaelewa ila ni mantiki nzima ya jambo lenyewe na pia amefanya vizuri sana kwa hilo
 
Esther ni mwanasiasa mzuri sana....Kiswahili hakifahamiki sawasawa na watanzania walio wengi,Kiingereza ndiyo usiseme.Sasa sijui tutafikia hatua sasa tuataanza kuchangia kwa mother tongue

Kwa mfano mchango wa Esther wa Leo ni mzuri sana na watanzania wamemuelewa.Kinachohitajika ni mawazo huru,fikra pevu na uwezo wa kuhamasisha na kuongoza wale anaowawawakilisha au kuwaongoza

Guys,Are you insinuating that she's not wordsmiths? Or are you exasperated about her oratorical style?

Mchango nimeukubali na ameeleweka ila jinsi mtu anavyobinya pua na mdomo inawafanya hata wasikilizaji wakwazike hata kama anatoa pointi wakati unajua kabisa ni mbongo. Bora hata kuchanganya lafudhi ya lugha ya mama inaeleweka.
 
kwani akichanganya lugha tatizo ni nini? khaaaaaaaaaaaaaaa wewe mvumbuzi huna kazi za kufanya, sasa unataka wanaume wazima tuchangie huu upupu hapa, "kama umempenda kanywe nae chai"
Wenye shida ya Chai Uganda , kwani sukari Kilo shs 5000, ila mimi sina haja nayo wala ntu wa kunywa naye nina Nke eti ndio huwa nakunywa naye chai tu na ananitosha.
 
Wenye shida ya Chai Uganda , kwani sukari Kilo shs 5000, ila mimi sina haja nayo wala ntu wa kunywa naye nina Nke eti ndio huwa nakunywa naye chai tu na ananitosha.

Hata mie nimemsikia na nimemuelewa ila wakati wa kusubiri ajibiwe umeme ukakatika
 
Kasumba hiyo si ya Mh. Matiku peke yake. Inawagusa wabunge wooote na mawaziri pia
 
Wachamene Mheshimiwa kabinti ketu kameongea bisuli,nyie munasema kameongea kingeresa kiswahili,musiasau anatoka tarime,lakini uchumbe si umefika chamani.Kwa maana yote aliyoongea bhinti huyu yote ni kweli tupu.Amesungumsia mambo ya kwetu kule tarime nyamongo wasungu wanapeana masiwa allowance safi lakini watansania hawaana hata kikombe kimocha cha mabele akhaaaa masiwa chamani kweli hiyo ni sawa.

Agacha akasungumsia kiwanda cha nguo cha urafki pale daisalama wafanyakasi wasamani wako kama mia na kitu awachalipwa teni yao ya kalibu shilingi bhilioni mocha sasa karibu miaka kumi na moya.

Kwa uhakika ni kameongea bisuli tena kwa uhakika hata Achelina anajua khabisa mrembo huyo mubhunge kaongea.

Ila kabinti khetu gachue tu kachitaiti ule usister dhuu wa kikoporate na graduate wa muchini daislama umo kwa bhunge auweke bembeni.Kwa kuwa anachiwesa kuzungumzia mambo ya muhmu kwenye chamii asihofu afute kamba akisema anaongea kingeresa basi aongeee sentensi yote dhadha.

Mubunge wetu wetu oyyyeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!! ila USILUTIE KUONGEA KILUGHA CHA WASUNGU NDANI YA BHUNGE.
 
Mchango nimeukubali na ameeleweka ila jinsi mtu anavyobinya pua na mdomo inawafanya hata wasikilizaji wakwazike hata kama anatoa pointi wakati unajua kabisa ni mbongo. Bora hata kuchanganya lafudhi ya lugha ya mama inaeleweka.

Watanzania tumeendekeza sana outside look na mtu anavyojiweka ndio maana tukaingia mkenge kuchagua mcheka hovyo eti "boys 2 men" with empty head. Shame. Sijamuona huyo Esther lakini sidhani kama hii argument inamshiko. Kwa mtizamo wangu huyo Esther angekuwa yuko kwenye interview ningeelewa (ingetegemea pia mwajiri anaangalia nini); lakini so far alichowakilisha 'substance" is what matters. Hiki kitu cha outside look, mtu anavyoongea etc ndio kimepelekea kuwa na lots of empty heads kwenye viti maalum pia. Kwani kuna std zimewekwa za jinsi wabunge wanatakiwa waweke midomo au pua?? Tusiwe wepesi kujaji watu kutokana na wanavyoongea/pose tukaacha vitu muhimu. ( Ha ha ha! Nimejishtukia na mimi nimechanganya lugha; well samahani kwa itakao wakera, you just have to get used to it or skip my comments when you see them lol!)
 
Esther ni mwanasiasa mzuri sana....Kiswahili hakifahamiki sawasawa na watanzania walio wengi,Kiingereza ndiyo usiseme.Sasa sijui tutafikia hatua sasa tuataanza kuchangia kwa mother tongue

Kwa mfano mchango wa Esther wa Leo ni mzuri sana na watanzania wamemuelewa.Kinachohitajika ni mawazo huru,fikra pevu na uwezo wa kuhamasisha na kuongoza wale anaowawawakilisha au kuwaongoza

Guys,Are you insinuating that she's not wordsmiths? Or are you exasperated about her oratorical style?

Kaka nawe kweli umekosa maneno mengine ya kidhungu ya kuchomeka hapo! Maana mi umeniacha kabisa hapo...Kha!
 
With a light touch; kuna dada alijiunga shuleni kwetu ilimchukua wiki 3 kusema biskuti na ugali, mwenyewe akizinadi 'nsia naomba kukuti' and 'ohmigosh! Its ugalai'!!

Anyways Ben & Co am not sure anyone is insuniating(sp) but merely pointing the obvious, there is absolutely no harm in speaking kiswahili if she knows it,
 
Nami ktk hili cjakubali linipite bila kuchangia! Huyu Honourable mi nshamckia lon' tym nikadhani anan'chefua mi peke yng atii! Sasa hilo la kumix language ni 9! 10 Mh. huyu ananichefua zaidi pale anapo'use R instead of L! kwenye L yeye ata'put R ! Mfano neno PROGRESS ana'pronounse PLOGLESS! au COLLECTIVE= CORRECTIVE, SUNGURA= SUNGULA, hii ni nini km si Rubish! Kuna umahiri gn wa ubingwa mjengoni Mbunge aongee lugha asiyoifahamu vyema? HAIPENDEZI & HAINA MASLAHI.
 
Mchango nimeukubali na ameeleweka ila jinsi mtu anavyobinya pua na mdomo inawafanya hata wasikilizaji wakwazike hata kama anatoa pointi wakati unajua kabisa ni mbongo. Bora hata kuchanganya lafudhi ya lugha ya mama inaeleweka.
Kweli wewe mvumbuzi alikuwa amevaa hereni za rangi gani.........
 
Back
Top Bottom