Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa amekanusha vikali kuwa anataka kuhamia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa amekanusha vikali kuwa anataka kuhamia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Duble Chris, May 7, 2012.

 1. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  MBUNGE wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya Dr.Mary Mwanjelwa amekanusha uvumi ulioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa anatarajia kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


  Alisema taarifa hizo ni uzushi na uongo kwa sababu yeye ni kada wa CCM wa siku nyingi ambaye amepewa dhamana na chama hicho kugombea ubunge kupitia jumuiya ya wanawake hivyo hatarajii kuwageuka kwa sababu bado anayo dhamana ya kuendelea kuwa Mbunge.


  Alisema, taarifa hizo zimenishtua sana, na hata wapiga kura wangu nao wamepata mshtuko mkubwa na wakanipigia simu ili kutaka kupata ukweli kutoka kwangu hivyo nimeona ni vizuri nitoe ufafanuzi.  Alisema yeye ni mbunge wa wananchi wote mkoani hapa, hana matatizo yeyote na chama hivyo haielewi sababu za kumfanya ahame chama chake na kujiunga na CHADEMA, kwa sababu ya uteuzi wa baraza jipya la mawaziri.  "Mimi ni mbunge kwa tiketi ya CCM na pia ni kada wa chama ambacho ndicho kilichonipitisha kugombea nafasi ya ubunge viti maalumu, na hatimaye nikafanikiwa kuchaguliwa sasa iwaje leo nikihame chama,"alihoji Mbunge huyo.  Aliongeza habari zilizoripotiwa ni za uongo, na kuwa kamwe hawezi kuingilia uteuzi wa Rais Kikwete katika kuwateua mawaziri, kwani hayo ni mambo ambayo hayamhusu kabisa.

  Dk.Mary alisema yeye amekwenda Bungeni kuwawakilisha wananchi wa mkoa wa Mbeya, sikwenda Bungeni kwa sababu ya kutaka kuwa Waziri, hizo ni nafasi za uteuzi na mwenye mamlaka hiyo ni Rais Kikwete.  Mbunge huyo wa viti maalum Mbeya, aliongeza hivyo ni vyema waandishi wa habari waache kuandika habari za kuchafuana, kuharibiana bali wafuate misingi na maadiri yanayolinda tasnia ya habari.  Alisema iwapo mwandishi anakuwa amepata taarifa ni vyema amfuate muhusika ili kupata ukweli juu ya habari anayotaka kuiandika iwapo ina ukweli wowote ndani yake.

  Aliongeza kama hayo yalikuwa ni maoni ya wananchi, anashindwa kuelewa yeye anaingizwaje katika habari hiyo, kwani ana mkataba wa kuwatumikia wananchi kwa miaka mitano na amebakiza miaka mitatu.  "Siwezi kuhamia CHADEMA, kwani CCM haijanifanyia kosa lolote, sikwenda Bungeni ili niteuliwe kuwa Waziri, kikubwa kwangu ni kuingia Bungeni kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi wangu wa mkoa wa Mbeya" alisema Dk.Mary.  Kwa mujibu wa Mwanjelwa alisema kuwa ni kweli alizungumza na Mwandishi aliyeandika habari hizo na kwamba mwandishi huyo alikuwa akitaka kupata ufafanuzi wa uvumi ulioenea ya kwamba kuna baadhi ya wananchi wanataka kwenda kumuona ili wamshawishi akihame chama kwa sababu ya Rais hakumteua kwenye Baraza jipya la Mawaziri.  "Mimi nilimjibu mwandishi huyo ya kwamba huo ni mtazamo wa wananchi lakini si wa kwangu "alisema Mwanjelwa huku akisisitiza kuwa hicho ni kipindi chake cha kwanza kuingia Bungeni sasa iwaje ashikwe na tamaa ya kutaka kushika madaraka ya juu .  Hata hivyo, alisema atagombea tena nafasi hiyo kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ili wanawake wampe tena kura zao kwani anajijua bado anafaa zaidi ya kufaa, hivyo atajitokeza katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kutetea nafasi yake hiyo kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi..


  SOURCE: - HAPA

  MY TAKE waandishi muwe makini sana
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mlitaraji akubali?
   
 3. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  huyo kimoyo moyo anataka kuhama ila anaogopa......yaani magamba wanawaogopa mabosi wao balaa
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kapigwa mkwara kaamua kuufyata!
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  wewe ndo uwe makini na wanasiasa. ulitaka akubali ili kesho atimuliwe ccm?
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Gamba mkubwa huyo tena mchumia tumbo na kamwe kwa hali ya uroho wa madaraka na kupenda bata za kijinga jinga hawezi kujiunga na makamanda wa millenia kama CDM ktk harakati hizi kwani CDM tunataka watu waliojizabihu nafsi zao kwa ajili ya maslahi ya wengi ikiwemo pa1 na kutokuogopa, kuwa tayar kupinga kila aina ya unyonyaji ikibidi hata kufa, sasa huyo ataweza kweli?
  YUPO TAYARI KUPIGANIA WANYONGE ATAWEZA KUHATARISHA MAISHA YAKE KWA KUCHINJWA KAMA iIP MWENYEKITI USER RIVER? Jibu ni kwamba hawezi so tumache amalize bata za mwisho huko ccm kwani almost wana miaka 3 tu ya kula bata koz baada 2015 wote wataingia gerezani kwa wizi wa rasilimali zetu.
   
 7. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ukisoma katikati ya mistari utaona kuwa majibu yake yamejikita zaidi kwenye kuongelea uteuzi wa mawaziri, lakini hajaisema vibaya wala kuikandia CDM hata kidogo, jambo linaloashiria ana hisia chanya na chama hiki. Zaidi sana maneno yake yanamuonyesha kama mtu ambaye ana wasiwasi na ikiwa kwa mfano atafuatwa na mtu kama Halima Mdee naamini anaweza kutetereka. Lakini kwa namna yoyote ile hawa ni suala la muda tu kabla mmoja mmoja hawajaanza kubisha hodi CDM.
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Hapo kwenye RED, huyu ni mbunge wa viti maalum, sasa hao wapiga kura wa ni kina nani?

  Inampasa atambue kuwa yeye amechaguliwa na magamba na sio wananchi wa Mbeya mjini, wananchi wa Mbeya mjini walimchagua Sugu..
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  sijamwelewa amesema wapiga kura wake yeye si mbunge wa viti maalumu hao wapiga kura wake toka mbeya wametokea wapi?na sugu amechaguliwa kuongoza wapi aache unafiki kwani ameshaona ni vigumu kumng'oa sugu kwa jinsi anavyokubalika
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hakusema anahamia cdm bali anapima upepo kwanza. Ila nadhani akiungana na sugu watafika mbali
   
 11. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wapiga kura wake ni wale wa ndani nadhani UWT huwapigia kura wote wanao hitaji ubunge kupitia viti maalum
   
 12. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Who needs her anyway!
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Mafuta na maji havichangamani hata siku moja. Na hapo ndipo CDM inatakiwa kuwa makini sana na wote wanaohamia huko sasa hivi.
   
 14. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,671
  Likes Received: 2,205
  Trophy Points: 280
  mwanbie akanushe kuwa ni mzazi mwenza na Jk!!!tunalojua ni kuwa ndoa yake na ccm IPO kulinda ndoa yake na jk!!
   
 15. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  I wonder! especially a thief like her!
   
 16. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hizi viti maalaam tolea mbali kabisa ni moja kati ya vitu vinavyotudididimiza bure ,kaazi yao kubwa malumbano majimboni huko wanajipanga na 2015
   
 17. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  swali langu ni kwamba,mwandishi wa habari ile hakumungunya maneno,alimtaj hadi kwa jina na akafanya hadi nukuu ya baadhi ya maneno ya mheshimiwa mary mwanjelwa ,sasa je ujasiri huu mwandishi wa habari aliupata wapi?iwapo habari ni ya uongo?
   
 18. w

  winner forever JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 1,097
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Taarifa yake inadokeza uwaziri siyo issue ila kama ushawishi wa kujiunga na movement for change utamfikia kikamilafu atasepa,
   
 19. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  maajabu haya tena inamaana taarifa zilizoletwa hapa juzi zilikuwa zauongo? au ameongopa ma boss wake? tuweni makini na hawa mamruki
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,611
  Likes Received: 4,717
  Trophy Points: 280
  Anaipenda sana Chadema sema tu anaogopa kulambishwa sumu na haya magamba.
   
Loading...