Mbunge Deo Sanga: Kikwete, Nape na Ndugai wasisemwe vibaya mitandaoni

sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,890
2,000
Mbunge wa Makambako (CCM), Deo Sanga ametaka tabia ya baadhi ya wabunge na viongozi wastaafu kusemwa vibaya katika mitandao ya kijamii akiwemo rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kukomeshwa kwa maelezo kuwa ikiachwa itaibua sintofahamu nchini.

Sanga maarufu Jah People ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 21, 2021 katika mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2021/22.

Mbali na Kikwete, amesema wengine wanaosimangwa mitandaoni ni mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, katibu mkuu wa zamani wa CCM, Abdulrahman Kinana na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

“Nani atafuata mheshimiwa Spika hii ni hatari, ni lazima tukemee kwa jambo ambalo linaweza kutugombanisha Watanzania. Hayo ni hatari kwa vitu ambavyo wameandika kule. Tukiliacha likaendelea kesho kutwa hatujui atawekwa nani.”

“Mheshimiwa Kikwete akapumzike amefanya kazi yake vizuri, Kinana akapumzike. Nape wewe ni shahidi 2013 hadi 2015 wakati wa uchaguzi..., Nape na Kinana walizunguka miaka mitatu kutafuta kura za CCM,” amesema.

Amebainisha kuwa katika kutafuta kura hizo Nape alikatwa hadi kiganja na Kinana kupata maumivu ya bega.

“Na wewe (Ndugai) wameanza kukuweka katika mtandao, wakuache ufanye kazi yako vizuri. Suala la Bagamoyo (bandari) Spika alichokisema ni nini? Amesema lijadiliwe. Nyinyi mna uwezo wa kusema hiki kinafaa hakifai,” amesema.

Baada ya kumaliza mchango huo, Ndugai amesema, “Nilimvumilia maana seneta ndio wazee wa mji huu.”
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,513
2,000
Wanademka tu!

Ingawa hilo la JK kutuhumiwa na kutajwa kwenye "kuondoka" kwa mwendazake pia ni tatizo. Needs to be addressed ASAP.
 

nizakale

JF-Expert Member
Oct 23, 2019
2,281
2,000
Wakati Rais aliyefariki anasemwa vibaya mitandaoni mbona hakukemea ? Kiongozi yeyote kusemwa haikwepeki. Pamoja na hayo sisi watanzania bado ni wamoja na undugu wetu uko pale pale kuanzia visiwani mpaka bara. Mbona waasisi wetu akina Nyerere na Kawawa na wengineo waliohatarisha maisha yao kudai uhuru walisemwa sana ? Kwa nini Nape na Kinana tu wasisemwe ?
 

Trimmer

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,666
2,000
Sawa ngoja tuheshimu wazee tusije laanika,, hatutawasema tena vibaya viongozi wetu wastaafu lakini tunaamini katika "KARMA" lazima italipa,, hapa hapa duniani..
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,762
2,000
Wakinga lini wataacha tabia ya kupeleka darasa la 7 mle bungeni.
Darasa la 7 wote huwa wanajadili watu badala ya hoja mezani.
Mnatukosea sana, mbunge ni kwa faida ya nchi sio jimbo tu.Wakinga msirudie tena 2025 kuchagua la7 hata kama ana wahonga mapesa, msimchague tena.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
46,819
2,000
Sasa jah people anajua kazi ya mitandao?

Mbona hata mjomba wake ambaye ni mganga mkuu wa kuwapa utajiri wakinga huwa anaandikwa mitandaoni?!
 

chibuga mugeta

JF-Expert Member
Jun 29, 2012
1,096
2,000
JK kayataka mwenyewe angetulia km mheshimiwa,
Wanademka tu!

Ingawa hilo la JK kutuhumiwa na kutajwa kwenye "kuondoka" kwa mwendazake pia ni tatizo. Needs to be addressed ASAP.
akumbuke kabaki peke yake,atunze legacy yake aache ujana,pia aieleze familia yake itulie iachane na ufisadi na tuhuma za ajabu,la sivyo atakuja kuzeeka vibaya,angalau siku hizi Ridhiwani na mama wametulia na saga za ajabu naye atulie,kuonekana kwake kuwe ktk matukio maalum
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom