Mbunge, Deo Sanga ataka Magufuli kuongezewa kipindi

Hii mambo ya kuengeza muda,kuna kitu gani kisichoeleweka,Dr Bashiru alimpiga yule Mh wa chemba STOP na akatoa sababu.Sasa huyu mwingine karudia yale yale ya mwakilishi wa Chemba,au tuseme hawa wabunge wetu wa CCM hawamu heshimu katibu mkuu wa chama au kuna kitu hatukijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1065240

MBUNGE wa Makambako, Deo Sanga maarufu Jah People (CCM), ameshauri Rais John Magufuli kuongezewa kipindi kimoja cha uongozi ambacho badala ya kumaliza urais mwaka 2025, akae hadi mwaka 2030. “Rais wetu (Magufuli) ana maono makubwa ya kuikisha mbali nchi yetu, hivyo aombewe awe rais wa kudumu, aongezewe kipindi kimoja hadi mwaka 2030, “Mimi na wenzangu tutatembea nchi nzima kumuombea…ikika mwaka 2021 wabunge tuanze kutembea nchi nzima kumuombea Rais Magufuli aongezewe muda,” alisema Sanga.

Mbunge huyo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, alitoa maoni yake hayo wakati akichangia Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwenye Osi ya Waziri Mkuu na Osi ya Bunge kwa mwaka 2019/2020 yaliyowasilishwa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Naye Mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha (CCM) alisema Rais Magufuli ana maono ya kulipeleka Taifa mbali zaidi na kuachana na kupitisha bakuli kwa wafadhili kuombaomba, hivyo kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili Taifa lijitosheleze. Kwa upande wake, Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali (Chadema)alisema “Inasikitisha wabunge wana mawazo ya kutaka Katiba ifanyiwe marekebisho makubwa ili rais aongezewe muda…inafedhehesha sana.

” Hata hivyo, Rais Magufuli mara kadhaa ameshasema hana mpango wa kuongeza muda wa uongozi na ikika muda wake wa kuachia madaraka, atafanya hivo tarehe hiyohiyo anayotakiwa kufanya hivyo. Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael (Chadema) alitaka wafanyabiashara wa masoko kutopewa vitambulisho vya ujasiriamali kwani kumesababisha halmashauri kukosa mapato na kushindwa hata kulipia gharama za kusasha masoko hayo.

Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo (CCM), alitaka Wizara ya Madini na Tume ya Madini kuwasimamia watendaji wao wanaowanyima leseni wachimbaji madini walio sa, wasio na matatizo na wanaotaka kulipa kodi. Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Jaku Hashim Ayoub (CCM) aliitaka serikali kuwapeleka Zanzibar viongozi mashuhuri wanaotoka nje ya nchi wanaotembelea Tanzania.
Huyu Mbunge kwanini anamjalibu Katibu Mkuu Bashiru? Hakumsikia Nkamia alivyoambiwa?

Hana akili huyu.. ndio aliye cheza nusura suruali imdondoke wapipo pitisga sifa ya kuwa mbunge ni kusoma na kuandika.

Deo sanga hakumaliza darasa la.saba

Hivi kuna sababu ya huyu Mh. kuchaguliwa tena,Dr Bashiru aliongea kiswahili tukamuelewa, Mh.nadhani hakumuelewa au ni utovu wa nidhamu kwa Katibu Mkuu..........anyway...!!!Time will tell.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni Mkinga ila siamini kama huyo ni Mkinga mwenzangu maana hana akili timamu
Hapana huyu si ndiye aliyecheza kiduku ndani ya ukumbi wa Bunge la katiba baada ya kupitisha mapendekezo ya mbunge lazima ajuwe kusoma na kuandika bila kujali hata kama hakumaliza darasa la Saba, DAB kwenye serikali ya Magufuri wapo wengi! maneno mengi maarifa zero usanii na matumizi ya nguvu ndiyo unatawala kwa sasa
 
Nchi hii kuna watu walistahili kuwa hospitalini Milembe lakini wapo majukwaani!!
 
Nakereka sana watu wanapoacha kujadili mambo ya maendeleo ya nchi kwa maana ya maisha ya siku kwa siku kwa wafanyakazi,wakulima na wafanyabiashara na baadala yake wanajadili
1) kuongeza ukomo wa kipindi cha urais maana yake nyingine ni kuwa na ubunge pia uongezewe ukomo;
2) kujadili raisi ajaye baada ya huyu wa sasa.
Hivi wabunge wamekosa kabisa ya kujadili ila urais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nini hawajadili namna ya kujenga middle class kubwa katika taifa letu bila porojo. Kwa nini hatujifunzi toka China,Malaysia,Vietnam n.k. Walikuwa wenzetu tu miaka ya 60,70 na hata 80 imekuwaje wanetuacha!.Taifa likiwa na middle class kubwa hakuna haja ya kulialia kuhusu korosho, viwanda kwa sababu demand inakuwa kubwa. Sina hakika kama hoja za baadhi ya wabunge kama mh. M. Bashe na mh Zitto huwa zinachambuliwa na kunyumbulishwa ili kutoa kitu kizuri kwa maendeleo yetu au wanazungumza inaishia hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom