Mbunge Dar amtwanga msaidizi wake

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,098
Mbunge Dar amtwanga msaidizi wake

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MBUNGE mmoja wa Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, anadaiwa kumpiga hadi kumjeruhi msaidizi wake kwa madai ya ufujaji wa fedha.

Mbunge huyo (jina limehifadhiwa kwa sasa), anadaiwa kutoa kipigo hicho juzi katika ofisi yake iliyopo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na Tanzania Daima, msaidizi wa mbunge huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa, alidai kuwa amepata maumivu sehemu ya jicho na mkono.

Alidai kuwa siku ya tukio, mbunge huyo alimwita ofisini kwake na kuzungumza naye mambo mbalimbali ya utekelezaji wa jimbo.

Msaidizi huyo alidai kuwa katika hali isiyo ya kawaida, ghafla mbunge huyo alianza kumlalamikia kwamba amekuwa akitumia vibaya fedha alizozipanga kwa shughuli za maendeleo jimboni mwake.

“Nilijaribu kumfahamisha, lakini hakunielewa na katika mabishano hayo, ghafla alisimama kwa jazba na kuanza kunipiga. Nimepata maumivu sehemu ya jicho na mkono,” alidai.

Alidai kuwa, baada ya kupata maumivu hayo, mbunge huyo alikataa kumpa fedha za kumpeleka hospitalini na badala yake alipata msaada kutoka kwa mmoja wa madiwani wa wilaya hiyo.

Msaidizi huyo alidai kuwa kibaya zaidi, mbunge huyo alimtishia kwamba endapo angelifikisha suala hilo polisi, angempa adhabu kubwa zaidi.
 
Kwani huyo msaidizi ndio mshika pesa zake? Au kuna mambo mengine hatuelezwi?
 
Mbunge Dar amtwanga msaidizi wake

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

MBUNGE mmoja wa Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, anadaiwa kumpiga hadi kumjeruhi msaidizi wake kwa madai ya ufujaji wa fedha.

Mbunge huyo (jina limehifadhiwa kwa sasa), anadaiwa kutoa kipigo hicho juzi katika ofisi yake iliyopo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na Tanzania Daima, msaidizi wa mbunge huyo ambaye kwa sasa jina lake limehifadhiwa, alidai kuwa amepata maumivu sehemu ya jicho na mkono.

Alidai kuwa siku ya tukio, mbunge huyo alimwita ofisini kwake na kuzungumza naye mambo mbalimbali ya utekelezaji wa jimbo.

Msaidizi huyo alidai kuwa katika hali isiyo ya kawaida, ghafla mbunge huyo alianza kumlalamikia kwamba amekuwa akitumia vibaya fedha alizozipanga kwa shughuli za maendeleo jimboni mwake.

"Nilijaribu kumfahamisha, lakini hakunielewa na katika mabishano hayo, ghafla alisimama kwa jazba na kuanza kunipiga. Nimepata maumivu sehemu ya jicho na mkono," alidai.

Alidai kuwa, baada ya kupata maumivu hayo, mbunge huyo alikataa kumpa fedha za kumpeleka hospitalini na badala yake alipata msaada kutoka kwa mmoja wa madiwani wa wilaya hiyo.

Msaidizi huyo alidai kuwa kibaya zaidi, mbunge huyo alimtishia kwamba endapo angelifikisha suala hilo polisi, angempa adhabu kubwa zaidi.

Tetesi...Porojo...Udaku...Journalism ya vichochoroni...!
 
Kazi ipo hapo maana jamaa amekula kichapo na amepigwa mkwara asilipeleke polisi la sivyo..kibarua kitaota nyasi...ahhahaha du hali ni maya sana .......sidhani kama mimi nitaweza ...ningeenda polisi tu...hata kama nikimwagwa poa tuu...hawezi kunifanya kama "cha ndimu"
 
Mbunge aliyemtwanga msaidizi wake atajwa





Mhe. Idd Azzan




na Mwandishi Wetu



MBUNGE mmoja wa Wilaya ya Kinondoni, anayedaiwa kumpiga msaidizi wake wa zamani na kumjeruhi, sasa amejulikana.

Mbunge huyo ni Idd Azzan, wa Jimbo la Kinondoni, anadaiwa kumpiga msaidizi wake wa zamani, Shawej Mkumbuli, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kata ya Magomeni.

Sababu kubwa ya ugomvi huo, imeelezwa kuwa ni hofu ya uchaguzi, ambapo mbunge huyo anadai Shawej amekuwa akijenga mtandao na kuandaa mkakati maalumu wa kumng'oa katika jimbo lake, kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza katika ofisi za Tanzania Daima juzi, Shaweji alisema ugomvi kati yake na mbunge huyo, ulitokea Jumatano iliyopita, katika eneo la wazi linalotumika kuegeshea magari, katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni.

Akiwa ameongozana na Katibu Mwenezi wa kata hiyo, Juma Matandika na viongozi wengine waliodai kushuhudia ugomvi huo, Shawej alisema siku hiyo kulikuwa na uchaguzi wa naibu meya, ambapo mbunge huyo na naibu meya aliyemaliza muda wake, Tulian Bujugo, walikuwapo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni.

Alisema katika uchaguzi huo, yeye (Shewej) pamoja na viongozi wengine wa kata hiyo, walikuwa wakimpigia debe Diwani wa kata yao, Bujugo, ili atetee kiti chake lakini alishindwa na badala yake, Diwani wa Kata ya Goba, Ibrahim Kisoki, ndiye aliyeibuka mshindi.

"Sisi tulikuwa tumekaa kwenye sehemu ya wageni ukumbini. Wakati kura zinaendelea kuhesabiwa, ghafla nilimwona mgombea wetu ambaye muda wote alikuwa amekaa jirani na Idd Azzan, akitoka nje kwa haraka, nikaamua pia kutoka na kumfuata, lakini sikumwona.

"Badala yake nikakutana na viongozi wetu wengine wako nje, tukawa tunabadilishana mawazo, hasa baada ya kubaini kuwa mgombea wetu alikuwa anaelekea kushindwa.

"Tukiwa katikati ya mazungumzo, Idd Azzan, alikuja kuungana nasi na baada ya kusalimiana naye, akaanza kusema Shawej nimepata habari zako siku nyingi kuwa unanichimba, unanifitini eti una mgombea wako wa ubunge na unajenga mtandao wa kuniangusha," alisema Shewej.

"Nilitaka kujibu, lakini alinibeza kwa kunitaka nisijibu chochote, lakini nami nikawa mbishi kutaka nijibu, ndipo ghafla alinirukia na kunipiga ngumi ya kichwa, kofi na kurusha teke ambalo lilinikosa.

"Kanipiga vibaya ndugu yangu, lakini sikutaka kurudishia, ingawa ninaweza kupigana naye, bahati nzuri viongozi niliokuja nao hapa ofisini kwako, walikuwapo, wakaamua kuingilia kati kuamlia ugomvi huo," alisema Shaweji, huku akionyesha sehemu ya jicho na mkono, alivyodai kuumizwa.

Alisema malalamiko ya Azzan dhidi yake, amekuwa akiyasikia muda mrefu, lakini aliyapuuza kwa madai kuwa mbunge huyo ni mtu wake wa karibu, hivyo kama ana malalamiko angeweza kumwita na kuzungumza naye kindugu.

Shawej alimtaja mtu anayedaiwa kuanza kumpigia debe kuwa ni Tarimba Abbas, jambo ambalo alisema si la ukweli, bali inatokana na hofu ya mbunge huyo.

Akizungumzia uhusiano wake na Azzan, tangu mbunge huyo alipoingia madarakani, alisema amekuwa msaidizi wake, lakini ilipofika Mei mwaka jana, aliacha kazi hiyo kutokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo kichama.

"Yeye mwenyewe Azzan, ndiye aliyeniambia kuwa sasa niache kuwa msaidizi wake kutokana na kazi nyingi nilizokuwa nazo kichama na tulikubaliana nimchagulie msaidizi mwingine na tangu wakati huo, nimekuwa na maelewano na mbunge wangu vizuri," anasema.

Shawej alisema yeye ndiye aliyechangia Azzan kuwa diwani wa kata yao na hata baadaye kuwa mbunge, hivyo alielezea kushangazwa kwake na hatua ya mbunge huyo kutoa kipigo kwake kwa tuhuma zisizo za ukweli.

Hata hivyo, alisema kama mwenyekiti wa kata, ameamua kulipeleka suala hilo kwenye kamati ya siasa ya kata, inayotarajia kukutana wiki hii na kupeleka taarifa ya tukio hilo la aibu kwenye ngazi za juu za chama.

Mbali na kulipeleka kwenye chama, suala hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, ambapo Idd Azzan, ndiye aliyefungua jalada la kudai kuwa ametukanwa na Shawej.

Habari kutoka ndani ya kituo hicho cha polisi, zilikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini mlalamikaji akiwa Idd Azzan, ambaye amedai kutukanwa na Shawej.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Tarimba juu ya kuwapo kwa malalamiko dhidi yake ya kutaka kuwania jimbo hilo, alikataa katakata huku akizitaka pande hizo mbili zinazotofautiana, zisimhusishe kwenye ugomvi wao.

"Mimi ndugu yangu haya mambo sijui yanatokea wapi. Ila wasinihusishe kwenye ugomvi wao," alisema kwa kifupi Tarimba.

Juhudi za kumtafuta Azzan kwa simu yake ya mkononi, hazikufanikiwa, kwani muda wote ilikuwa imezimwa.

Azzan amekuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2005, baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Peter Kabisa




hii kasheshe tena! nae ataenda jela mwaka ama?
 
Back
Top Bottom