Mbunge CUF adai kuna Meli ya Mizigo imebadilishwa jina inasafirisha abiria katika Ziwa Victoria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge CUF adai kuna Meli ya Mizigo imebadilishwa jina inasafirisha abiria katika Ziwa Victoria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 3, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]IJUMAA, AGOSTI 03, 2012 05:13 NA MAREGESI PAUL, DODOMA

  MBUNGE wa Ole, Rajab Mbarouk (CUF), amesema kuna meli ya mizigo imebadilishwa na kuanza kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria.

  Kutokana na hali hiyo, amesema Serikali isipochukua tahadhari, meli hiyo inaweza kuzama na kusababisha vifo kama ilivyotokea katika Meli ya Mv Skagit, iliyozama hivi karibuni kisiwani Zanzibar.

  Mbarouk alitoa taarifa hiyo bungeni jana, alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.

  “Meli ya MV Skagit, ilizama kwa sababu baada ya kununuliwa na wafanyabiashara wa Zanzibar kutoka Marekani, ilibadilishwa muundo wake na ikaanza kubeba abiria.

  “Kutokana na mabadiliko hayo, mwishowe meli hiyo imezama na kuua makumi ya wananchi kwa sababu hata ukifuatilia historia yake, inasemekana ilikuwa ikitakiwa kusafiri umbali usiozidi kilomita saba.

  “Kwa hiyo, kama tahadhari isipochukuliwa, yaliyotokea Zanzibar yanaweza kutokea katika Ziwa Victoria, kwa sababu kule kuna meli inaitwa Sumar II inasafirisha abiria kutoka Mwanza kuelekea Nansio Ukerewe na wakati mwingine inakwenda Uganda.

  “Meli hii, inayobeba abiria zaidi ya 200 ilikuwa ni ya mizigo, lakini sasa imebadilishwa matumizi yake, kwani inabeba abiria, iangalieni sana meli hii ili yasije yakatokea yaliyotokea Zanzibar,” alisema Mbarouk.

  Awali wakichangia bajeti hiyo, baadhi ya wabunge waliishangaa Serikali ya Tanzania kwa kutokuwa na usafiri wa uhakika wa ndege.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema haridhishwi na utendaji kazi wa Serikali kwa kutokuwa na ndege wakati Rwanda ambayo ukubwa wake ni sawa na Mkoa wa Kigoma ina ndege saba.

  Naye Mbunge wa Viti Maalum, Anamery Malaki (CHADEMA), alisema ni aibu nchi kama Tanzania kukosa ndege ya abiria wakati ina utajiri kuliko nchi nyingi duniani.

  Wakati hao wakisema hayo, Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), naye alisema haiingii akilini kwa nchi kama Tanzania kukosa ndege wakati Ethiopia ina ndege nyingi.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  Asante Mh. Rajab Mbarouk, hii inapaswa kufuatiwa Uchunguzi... kuokoa Maisha ya Wananchi wa Tanzania

  Unaona faida ya Kuchangia Hoja hata kama si-za Muungano? Hii hapa itaokoa Maisha ya Watanzania Wasio na Hatia

  Wakati sisi tunalalama na kwanini wanachangia hiki kwanini wanapewa hili...
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Wako wapi SUMTRA? Je waliikagua na kuipatia certification ya ubora hii SUMAR II.

  Jamani hutataki yatokee ya Mv. Bukoba please serikali do the needful, wananchi hawafahamu Sumar II ilikuwa meli ya mizigo!
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ingekuwa imesemwa na kiongozi wa Chadema usingeadika Negative, eti mbunge wa CUF adai..Pro-Chadema bana.
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,906
  Likes Received: 5,367
  Trophy Points: 280
  where is negativity in the statement?we unapenda ligi sana!!!!labda sijakuelewa,kila wakati chadema inakufanya uweweseke
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145

  Mimi nimeandika wapi ADAI? Umeona mimi nimesema ASANTE? na nimewakashifu watu wasiopenda wabunge wa Zanzibar

  Wasichangie HOJA zisizo za MUUNGANO? sasa Mimi wapi nimeandika ADAI? HAKUNA KIZURI UTAKACHO KIONA?

  YAANI MAWAZO YAKO NI UPWEKE NA UMIMI?
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Angalia Heading ya thread yako "Mbunge CUF adai kuna meli ya Mizigo imebadilishwa jina imebadilishwa jina inasafisha abiria katika Ziwa Victoria"

  Haya maneno unayakana?

  Halafu angalia Content...
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145


  Sio Mimi niliyeandika ADAI; Ni Waandishi wa HABARI hizo... Lakini Unajua kama HABARI imesemwa tu BUNGENI BILA YA

  UHAKIKA NA UCHUNGUZI HAWANA UHAKIKA KUWA HIYO MELI ILIKUYA YA MIZIGO NA KUBADILISHWA KUYA YA ABIRIA

  WATASEMA NI DAI (ADAI) ILI WASIJE WAKAPELEKWA MAHAKAMANI NA KUWA SUED NA WENYE MELI HIYO KAMA NI

  UONGO NADHANI UNAJUA SHERIA KIDOGO... NDIO MAANA WAMEANDIKA ADAI... SIO MBAYA...

  USIGUBWIKWE NA VITU VIDOGO; NIMEIPENDA HII HABARI KWELI... JINSI ALIVYOAMUA KUTOLEA HILI JAMBO MHANGA

  LAKINI KWANINI KUWA NA HASIRA HIVI???
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hilo kubwa tunaomba uchunguzi ufanyike haraka sana ili kuokoa maisha ya watanzania
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,152
  Trophy Points: 280
  nngu007,

  ..pamoja na mawazo mazuri ya mheshimiwa mbunge toka Znz mimi kama Mtanganyika bado siutaki muungano.

  ..hawa wabunge wanatugharimu kwa kiasi kikubwa sana wa-Tanganyika. the way I look at this ni kwamba posho tunazowalipa zingeweza kutupatia wa-Tanganyika meli mpya.

  ..majuzi Dr.Bilali amepewa bilioni 32 kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar. Juu ya hizo kuna bilioni nyingine 9 kwa matumizi ya ofisi yake. muungano ukivunjwa pesa hizo zinaweza kuwa allocated kwenye ujenzi wa shule, vyuo vya ufundi, au hata kununua meli na vivuko.

  ..MUUNGANO UNATUNYONYA NA KUTUTIA HASARA WATANGANYIKA. NAWAOMBA MSIDANGANYIKE KIRAHISI NAMNA HII.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145


  HATA MIMI SIUPENDI HUO MUUNGANO; WAZANZIBARI WAMEKUWA KAMA WATAWALA WETU...

  Lakini huyu Mwakilishi ameona kosa; kalisema kuliko kujinyamazia kimya na kusema waache na wao wafariki; kama

  Hajali Utu na Unajua WABUNGE wetu wako kazini kuangalia JINSI YA KUDONYOA VIPESA VYA TANESCO na KUZIMIA

  WANANCHI UMEME WAKATI WA USIKU ZIWA VICTORIA HAUWEZI KUKIONA HICHO CHOMBO...
   
Loading...